Featured Posts
Monday, 4 April 2022
HAKUNA CHAMA CHA MTU LAZIMA TUSIMAMIE HAKI. KINANA
Athman Hemed Sampa afariki dunia
Sunday, 18 March 2018
WATUMISHI WA AFYA WAASWA KUJIEPUSHA VITENDO VYA RUSHWA SEHEMU ZAO ZA KAZI
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
Urusi yashutumu mataifa ya Magharibi
Urusi imeyashutumu mataifa ya Magharibi kwa kuwasaidia waasi nchini Syria, baada ya mkutano na Iran na Uturuki kwenye awamu ya mazungumzo mapya ya kujaribu kutafuta ufumbuzi wa mzozo unaoendelea nchini humo.
Mawaziri wa mambo nje wa Urusi, Iran, Uturuki walikutana katika mji mkuu wa Kazakhstan, Astana, wakiangazia suala la Ghouta Mashariki ambayo ni ngome ya upinzani iliyoko nje ya mji wa Damascus, iliyoanza kushambuliwa mwezi mmoja uliopita na utawala wa rais Syria Bashar al-Assad.
Mkutano wa Astana ulilenga kuweka msingi wa kikoa cha marais wa mataifa hayo matatu kitakaochofanyika mjini Istanbul Aprili 4. Akiongea baada ya mazungumzo hayo waziri wa masuala ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov ameyalaumu Mataifa ya Magharibi kwa kuwakingia kifua waasi na hata kuimarisha uwezo wao wa kivita.
Mataifa ya Urusi na Iran yanamuunga mkono rais Assad, lakini Uturuki imetaka kusitishwa kwa mashambulizi Ghouta Mashariki ambapo takriban watu 1,260 wameuawa wengi wao wakiwa watoto tangu lianze kushambuliwa mwezi Februari tarehe 18.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelielezea janga la kibinadamu katika eneo hilo ambalo halina chakula, maji na mahitaji mengine ya kimsingi kuwa jehenamu ya duniani.
Lavrov ayakosoa mataifa ya Magharibi
Lakini Lavrov alisema kuwa mtazamo wa mataifa ya Magharibi ni wa upande mmoja na kuwashutumu wenzao kwa kujaribu kuwalinda waasi, akitoa mfano wa kundi la Hayat Tahrir al-Sham ambalo limeundwa na waliokuwa wapiganaji wa kundi la Al-Qaeda ambalo liko Ghouta Mashariki. Amesema kuwa kundi hilo linafuata maelekezo kutoka kwa mataifa ya Magharibi. Lavrov pia ameonya dhidi ya kitisho cha Marekani kuushambulia mji mkuu wa Syria Damascus haitakubalika.
Lavrov amesema, "tunapenda kukumbusha kwamba matumizi ya nguvu dhidi ya Damascus kwa visingizio hayakubaliki. Vitisho vilivyotolewa hivi karibuni na Marekani kuhusu mashambulizi ya upande mmoja dhidi ya Syria ikiwemo Damascus - kama tuhuma zisizo na msingi mwezi Aprili mwaka uliopita kuhusiana na matumizi ya silaha za kemikali na serikali ya Syria - hazikubaliki na hazitovumiliwa."
Urusi, Iran na Uturuki zaafikiana
Katika mwafaka uliotiwa saini na Lavrov, Mohammad Javad Zarif wa Iran na Mevlut Cavusoglu wa Uturuki- na kutolewa na wizara ya mambo ya nje ya Kazakhstan, mwishoni mwa mazungumzo, mataifa hayo matatu yaliamua kuvunja nguvu za makundi yanayohusishwa na Al-Qaeda.
Ghouta Mashariki ilistahili kulindwa na kuwa salama. Lakini utawala wa Syria na Urusi wametumia kisingizio cha waasi katika eneo hilo kutekeleza mashambulizi.
Wakati hayo yakiarifiwa shirika la uangalizi wa haki za biadamu nchini Syria linasema mashambulio ya angani ya Urusi na serikali ya Syria Ghouta Mashariki yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 46 katika muda wa masaa 24.
Ripoti ya kundi hilo inasema kuwa mji wa Kafr Batna ulishambuliwa na vilipuzi hii leo. Vikosi vya serikali vinaelekea katika ngome za waasi hali ambayo imechangia raia wengi kuhama.
Kwingineko katika mji wa Afrin ulioko kaskazini mwa Syria takriban raia 20 wameuawa, miongoni mwao kina mama na watoto huku wengine 30 wakijeruhiwa.
Picha zilizotumwa na wanaharakati wa Kikurdi zilionyesha watoto wakilia huku wakitokwa damu walipokuwa wakipelekwa katika hospitali ya Afrin kutibiwa.
Chanzo. Dw.de
Ujerumani sasa ina serikali mpya
Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha zaidi na mzozo kati ya Uingereza na Urusi kuhusiana na shambulio la sumu dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi nchini Uingereza, na pia kuhusu serikali mpya ya Ujerumani.
Mhariri wa gazeti la Rhein-Zeitung la mjini Koblenz anaandika kwamba uchaguzi mwingine wa majimbo utaonesha iwapo kile kinachoonekana kuwa ni kuaminika na wananchi kwa muungano wa vyama vya kihafidhina na SPD kuunda serikali kumefanikiwa. Mhariri anaendelea.
Mtihani wa kwanza utakuwa mnamo wakati wa kuelekea mwishoni mwa mwaka huu katika jimbo la Bavaria na kisha Hesse. Mwaka 2019 kutakuwa na mtihani mwingine wa uchaguzi wa bunge la Ulaya na kisha uchaguzi katika majimbo matatu ya mashariki mwa Ujerumani. Hali itakwenda vizuri , iwapo vyama ndugu vya CDU /CSU pamoja na SPD hadi wakati huo wataonesha kile walichofanikisha, kwamba wametatua matatizo ya wananchi.
Bila hivyo inawezekana katika majimbo ya mashariki wapiga kura watakimbilia katika chama mbadala kwa Ujerumani AfD.
Nae mhariri wa gazeti la Hannoversche Allgemeine la mjini Hannover anaandika kwamba Kansela Angela Merkel na waziri wa fedha Olaf Scholz sasa wana nafasi , kupitia sera muafaka za kubana matumizi katika sehemu kubwa ya eneo la kati nchini na kunyamazisha kile kilichoonekana kuwa ni ukweli katika majadiliano yaliyokuwapo katika miezi iliyopita. Mhariri anaandika.
Kwa mfano ni mara ngapi watu wamesikia nchini Ujerumani maneno kama "hali haiwezi kuendelea hivi" Kila mwananchi anaiangalia hali hii kwa njia tofauti. Baadhi yao ambao wanaona hali ya kiuchumi kuwa nzuri , wataendelea kupiga kura , linasema kundi linalochunguza maoni ya wapiga kura, ambao wanafikia ni karibu Wajerumani asilimia 60. Mtazamo wa wale wanaosema tuendelea hivyo hivyo kiukweli wanasema hivyo kwa misingi ya upatikanaji tu wa mahitaji ambao ndio unaowavutia zaidi.
Mzozo kati ya Uingereza na Urusi
Nalo gazeti la General-Anzeiger la mjini Bonn linaandika kuhusiana na mzozo kati ya Uingereza na Urusi kufuatia shambulio la sumu dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi nchini Uingereza. Mhariri anaandika.
Pande zote mbili zinapambana , nyuma lakini kuna hali ya kuigiza ya kutisha ambayo haieleweki. Shambulio dhidi ya jasusi wa zamani aliyeamua mwaka 2010 kukimbia kutoka Urusi haliingii akilini. Kitu kigani serikali ya Urusi itakipata kwa kufanya shambulio hilo, siku chache kabla ya uchaguzi ambao Putin anawania nchini Urusi? Kwa upande mwingine Uingereza inataka nini , kwa kufanya tukio hili ambalo si la kweli na kuweka hali ya wasi wasi kati ya Uingereza na Urusi, kama vile wanavyodai Warusi.? Hakuna, mhariri anaandika. Hali mpya mbaya ya uhusiano baridi kati ya mashariki na magharibi inaongezeka.
Mhariri wa gazeti la Stuttgerter Nachrichten akizungumzia mzozo huo kati ya Uingereza na Urusi anaandika kwamba Imegundulika hakuna ushahidi uliokwisha tolewa.Mhariri anaandika:
Kwamba waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ametoa sauti, lakini kwa mara ya kwanza ametoa adhabu ya hovyo hovyo hivi.
Na hili hata yeye binafsi analifahamu. Kutokana na hali ilivyo Uingereza pia inabidi kuwashirikisha pia washirika. Hii inahusu Ujerumani pamoja na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya na washirika wa NATO. Kuna ishara ya wazi kwamba wote wako upande wa Uingereza, bila kujali Brexit. Na utayari , wa kuimarisha vikwazo , iwapo serikali ya Urusi itagundulika kuwa nyuma ya shambulizi hilo.
Chanzo. Dw.de
Urusi imewafukuza Wanadiplomasia 23 wa Uingereza
Urusi imewafukuwa wanadiplomasia 23 wa Uingereza katika hatua ya kujibu uamuzi wa Uingereza kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi kufuatia kashfa ya kupewa sumu kwa jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal nchini Uingereza.
Urusi ambayo inadaiwa kuhusika na kitendo hicho cha kupewa sumu kwa Skripal, siku ya Jumamosi imetangaza kuwa inawapa muda wa wiki moja pekee wanadilpomasia 23 wa Uingereza kuondoka nchni humo na kusitisha shughuli za shirika la kimataifa la Uingereza la British Council nchini humo linalohusika na masuala ya elimu pamoja na ushirikiano wa kitamaduni.
Hayo yanajiri baada ya Urusi kumuita hii leo balozi wa Uingereza nchini humo Laurie Bristow ambapo pia wizara ya mambo ya nchi za nje ya Urusi imeonya kuwa serikali italazimika kuchukua hatua nyingine zaidi iwapo vitendo vingine visivyo rafiki vitafanyika dhidi yake.
Urusi yajibu hatua za Uingereza
Aidha Urusi pia imesitisha shughuli za ubalozi mdogo wa Uingereza ulioko katika mji wa St Petersburg. Alhamisi wiki hii, Uingereza ilitangaza inawafurusha wanadiplomasia 23 wa Urusi kutokana na kughadhabishwa na shambulizi la sumu dhidi ya Skripal mwenye umri wa miaka 66 na binti yake Yulia mwenye umri wa miaka 33 katika mji wa Salisbury. Wawili hao wako katika hali mahututi hospitalini.
Urusi ambayo kesho Jumapili inafanya uchaguzi wa Rais unaotarajiwa kumpa ushindi Rais Vladimir Putin imeonya kuwa iko tayari kuchukua hatua kali zaidi kujihami na kuilinda hadhi yao dhidi ya uhasama kutoka Uingereza na nchi nyingine za Magharibi.
Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema ilitarajia Urusi kuchukua hatua za kulipiza kisasi na kuongeza kuwa Baraza la kitaifa la Usalama litakutana mapema wiki ijayo kujadili hatua zaidi itakazochukua kuhusiana na shambulizi hilo la sumu nchini Uingereza.
Katika taarifa wizara hiyo ya mambo ya nje ya Uingereza imeongeza kusema wanachokipa kipaumbele hivi sasa ni kuwahudumia maafisa wake walioko Urusi na kuwasaidia wale waliorejeshwa nyumbani.
Urusi bado haijajieleza vya kutosha
Uingereza imesisitiza kuwa hatua ilizochukua Urusi haibadilishi ukweli kuwa jaribio la kuwaua watu wawili kwa kutumia sumu lilifanywa katika ardhi ya Uingereza na hakuna shaka Urusi ilihusika na jaribio hilo.
Urusi ambayo imekanusha kuhusika na shambulizi dhidi ya Skripal na binti yake imelalamika kuwa Uingereza imeshindwa kutoa ushahidi kuwa Urusi ndiyo ilihusika katika shamabulizi hilo la Salisbury na kuongeza kuwa imeshutushwa na wakati huo huo, kuchekeshwa na madai hayo yasiyo na msingi wowote na yasiyosameheka.
Siku ya Ijumaa, Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson alisema kuna uwezekano mkubwa kuwa Rais Vladimir Putin ndiye alitoa maamuzi hayo ya kumshambulia Skripal kwa kutumia sumu inayoathiri neva.
Uingereza, Marekani, Ujerumani na Ufaransa kwa pamoja zimeitaka Urusi kutoa maelezo kuhusu shambulizi hilo lililotokea tarehe 4 mwezii Machi. Wachunguzi wa Urusi wamesema wameanzisha uchunguizi wa uhalifu kuhusu jaribio la kumuua Yulia Skripal na kuongezea wako tayari kushirikiana na maafisa wa Uingereza.
Chanzo. Dw.de
Warusi wapiga kura
Warusi wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa rais Jumapili (18.03.2018) unaotarajiwa kumpa Putin ushindi mkubwa ambao unaweza tu kuchafuliwa iwapo watu wengi hawatajitokeza kupiga kura kwa sababu matokeo yanatabirika.
Katika eneo la mashariki mwa Urusi, katika mji wa pwani ya bahari ya Pacific wa Petropavlovsk-Kamchatsky, vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema saa tano usiku saa za Urusi, na upigaji kura utaendelea katika nchi hiyo kubwa hadi vituo vitakapofungwa katika eneo la magharibi kabisa mwa nchi hiyo katika jimbo la Kaliningrad , masaa 22 baadaye.
Uchunguzi wa maoni ya wapiga kura unampa Putin , rais wa sasa , uungwaji mkono wa kiasi ya asilimia 70, ama karibu mara 10 zaidi ya uungwaji mkono wa mgombea anayemkaribia. Muhula mwingine utamchukua karibu robo karne akiwa madarakani, muda mrefu zaidi miongoni mwa viongozi wa serikali ya Kremlin wapi tu kwa dikteta wa enzi wa Kisovieti Josef Stalin.
Wengi wa wapiga kura wanamsifu Putin, mwenye umri wa miaka 65 jasusi wa zamani wa shirika la kijasusi la Urusi , KGB, kwa kutetea masilahi ya Urusi katika dunia hii yenye uhasama, hata kama gharama ni mapambano dhidi ya mataifa ya magharibi.
Mzozo na Uingereza kuhusiana na madai kwamba Kremlin ilitumia sumu inayoathiri mishipa ya fahamu dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi katika mji mtulivu wa Uingereza , madai ambayo Urusi inakana , haujachafua uungwaji wake mkono.
Wengi wa wapiga kura hawaoni mtu mbadala kwa Putin, ana udhibiti kamili wa medani ya kisiasa pamoja na televisheni ya taifa, ambako watu wengi wanapata taarifa zao, na kutoa muda mkubwa kwa matangazo yanayomhusu Putin na muda mchache kwa wagombea wengine.
"Putin ndio rais wetu. Tunajivunia," amesema Marianna Shanina, mkaazi wa jimbo la Crimea. Urusi ililinyakua jimbo la Crimea kutoka Ukraine miaka minne iliyopita, na kumpa sifa Putin kutoka kwa Warusi wengi na shutuma kutoka mataifa ya magharibi.
Warusi hawana mbadala kwa Putin
"Tunamtakia ushindi katika uchaguzi. Familia yetu yote itampigia kura Putin. Putin ! Afya njema kwako, rais wetu mpenzi !," Shanina alisema katika mkutano wa kampeni wa Putin.
Uchunguzi wa maoni ya wapiga kura uliofanywa Machi 9 na kampuni inayomilikiwa na serikali ya VTsIOM ilimpa Putin ambaye alichaguliwa mara ya kwanza kuwa rais mwaka 2000, uungaji mkono wa asilimia 69. Mgombea aliyeko karibu nae Pavel Grudinin , mgombea wa chama cha Kikomunist , atapata asilimia 7.
Mjumbe wa tume ya uchaguzi nchini Urusi akiweka karatasi inayoonesha picha za wagombea katika uchaguzi nchini Urusi
Mwanasiasa wa kwanza katika miaka kadhaa kutoa changamoto kwa udhibiti wa serikali madarakani, Alexei Navalny, amezuiwa kushiriki katika uchaguzi huo kwasababu ya kuhumumiwa kwa madai ya rushwa, madai ambayo anasema alibambikiwa na serikali.
Anatoa wito wa kuususia uchaguzi huo, akisema ni kichekesho cha kitokuwa na demokasia, na kuwaweka waungaji wake mkono kukusanya ushahidi wa mtu yeyote atakayefanya udanganyifu katika uchaguzi kuweka idadi ya juu ya watu watakaoshiriki katika uchaguzi huo na uungwaji mkono wa Putin.
Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny ambaye amezuiwa kugombea katika uchaguzi huo akikamatwa na poilisi, Januari 28, 2018
Serikali ya Urusi pembeni inakiri kuwa na wasi wasi kwamba baadhi ya Warusi milioni 110 wenye haki ya kupiga kura hawatajisumbua kupiga kura kwasababu wanaamini Putin atashinda tu. Uchache wa watu watakaojitokeza kupiga kura utaathiri mamlaka yake katika muhula ujao, ambao , chini ya katiba, utakuwa wa mwisho.
Katika hotuba kwa taifa iliyotangazwa moja kwa moja na televisheni ya taifa siku ya Ijumaa, Putin alisema wapigakura wana mustakabali wa nchi hiyo katika mikono yao.
Chanzo Dw.de
Urusi yawafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza
Serikali ya Urusi imetangaza kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza na imetishia kuchukua hatua zaidi ikilipiza kisasi katika mgogoro unaoendelea kukua wa kidiplomasia kufuatia shambulizi la sumu lililofanywa dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi nchini Uingereza.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema katika tamko lake kuwa pia imeamrisha kufungwa kwa kituo cha utamaduni cha Uingereza nchini Urusi na kusitisha mkataba wa kufungua tena ubalozi mdogo wa Uingereza huko mji wa St. Petersburg.
Tayari imewaamrisha wanadiplomasia hao wa Uingereza kuondoka nchini Urusi katika kipindi cha wiki moja.
Wizara hiyo pia imemwita Balozi wa Uingereza nchini Urusi siku ya Jumamosi kabla ya kutangaza hatua hizo.
Tamko la Wizara hiyo limesema kuwa serikali ya Urusi inaweza kuchukua hatua zaidi iwapo Uingereza itaonyesha vitendo vyovyote “visivyo vya kirafiki” dhidi ya Urusi.
Hivi karibuni Uingereza iliwafukuza wanadiplomasia 23 wa Urusi baada ya Moscow kukataa kutoa maelezo vipi aina ya sumu iliyokuwa ikitumika wakati wa utawala wa Soviet iliweza kutumika katika mji wa Salisbury- Uingereza kumshambulia jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na binti yake, Yulia.
Kulipiza kisasi kuliko tangazwa na Waziri Mkuu Theresa May katika Bunge la Uingereza kumepelekea kuanza kwa vita ya kiuchumi dhidi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na kikundi cha watu wachache wenye maslahi ya pamoja cha maafisa wa serikali ya Kremlin na wafanyabiashara matajiri wenye ushawishi wa kisiasa.
Vikwazo hivyo ni pamoja na kuzuia rasilmali zao ambazo wanazimiliki Uingereza pamoja na kunyimwa viza kwa watu binafsi wote waliotajwa katika sakata hilo.
Waziri Mkuu anawashinikiza washirika wa kimataifa kufuata hatua iliyochukuliwa na Uingereza na kuanza kuangaza mabilioni ya dola ambazo Kremlin imewekeza katika rasilimali zake ulimwenguni kote.
Chanzo. VOA
Thursday, 8 February 2018
Tarehe sita muhimu zinazoeleza kwanini Zuma anakabiliwa na shinikizo
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma anakabiliwa na shinikizo ajiuzulu wakati wanachama wakuu wa chama chake walio na uwezo wa kumtimua wakitafakari hatua yao inayofuata.
Ameuhudumu kama rais kwa takribana thuluthi moja ya utawala wa nchi hiyo baada ya ubaguzi wa rangi, lakini uongozi wake umegubikwa kwa kashfa.
Kwa hivyo ni nini kilichotokea kutufikisha hapa tulipo? Haya ni matukio makuu.
14 June 2005: Afutwa kazi
Kwa wakati huu Zuma alikuwa naibu rais aliye na umaarufu na mkakamavu kwa miaka sita - lakini aliipoteza kazi yake baada ya kutuhumiwa katika kesi ya rushwa.
Kwa muda mrefu ameonakana kama mrithi wa rais aliyekuwepo - Thabo Mbeki.
Akiwa kijana alijiunga katika vita vya kupinga ubaguzi wa rangi katika chama cha African National Congress (ANC) na jeshi lake la chini chini kabla ya kufungwa huko Robben Island na Nelson Mandela.
Mnamo 1997, alikuwa naibu rais wa chama tawala ANC, na baadaye alitajwa kuwa naibu wa rais nchini Afrika kusini mnamo 1999.
Baadaye aligubikwa katika mzozo kuhusu biashara ya silaha yenye thamani ya $ bilioni 5 mnamo 2009 iliyohusisha kampuni kadhaa za Ulaya.
Mshauri wa fedha wa Zuma, Schabir Shaik, alipatikana na hatia ya rushwa na udanganyifu.
Katika kesi hiyo, Zuma alituhumiwa katika kesi hiyo ya rushwa na wakati amekana daima tuhuma hizo, aliipoteza kazi yake. Alishtakiwa mnamo 2007.
6 Aprili 2009: Wiki mbili
Jitihada za rais Zuma kuwania urais zilikuwa zimefika kikomo wakati waendesha mashtaka walipoamua kutomshtaki dhidi ya biashara hizo ya silaha.
Mwendesha mashtaka mkuu nchini amesema ushaihdi uliotokana na kunaswa mawasiliano ya simu unaonyesha kuwa mashtaka hayo mnamo 2007 yalichochewa kisiasa.
Upinzani mkuu waliishutumu hatua hiyo na kuitaja kuwa "utumiaji mbaya" wa jukumu la mwendesha mashtaka. Hatahivyo Zuma, ambaye wakatihuo alikuwa rais wa ANC aliishia kushinda urais wa nchi wiki mbili baadaye.
31 Machi 2016: Kidimbwi maridadi, lakini nani aliyekilipia?
Mahakama ya juu ya Afrika ksuini imeamua kuwa Zuma alikiuka katiba wakati aliposhindwa kuilipa serikali pesa alizotumia kwa ujenzi wa makaazi yake binfasi.
Shirika la kupambana na rushwa lilifichua kwamba ametumia $milioni 23 katika makaazi yake Nkandla katika jimbo la KwaZulu-Natal na kujenga kidimbwi cha kuogolea na na chumba cha kutizama filamu. Baadaye alizilipa pesa hizo.
Kwa mara nyengine akakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu. Na kwa mara nyengine hakujiuzulu.
13 Oktoba 2017: Mashtaka yarudi upya
Mahakama ya rufaa ya juu zaidi Afrika kusini iliamua kuwa ni lazima Zuma ajibu mashtaka 18 ya rushwa, udanganyifu, na biashara haramu ya fedha yanayohusiana na biashara ya 1999 ya silaha.
Yote haya yalitokana na kesi iliyowasilishwa na chama cha upinzani Democratic Alliance katika mahakama ya Pretoria kikitaka rais akabiliwe na mashtaka. Zuma alikata rufaa, lakini alishindwa.
13 Desemba 2017: Hukumu mbili, siku mbaya
Kwanza mahakama ya Pretoria ilimuamuru Zuma aunde jopo wanasheria la uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa dhidi yake na washirika wake , ambalo hatimaye aliliunda mnamo Januari.
Uchunguzi huo ni mojawapo ya mapendekezo yaliowasilishwa na tume ya kupambana na rushwa kuistisha maafisa wa serikali kuingilia kati katika kesi hiyo, hatua ambayo Zuma alijaribu kuipinga.
Jaji Dunstan Mlambo alitaja jitihada hizo za uma kujaribukuzuia hukumu kama ushauri m'baya na ukiukaji wa mfumo wa sheria.
- Ramaphosa aahidi kuimarisha uchumi wa Afrika Kusini
- Jacob Zuma na makamu wake walazimishwa kusalimiana
Kisha, kwa kando, jaji mmoja aliamua kuwa rais alikiuka mfumo wa sheria kwa kujaribu kuzuia ripotikuhusu rushwa.
Takwimu zinazojitokeza katika tuhuma dhidi ya Zuma ni familia tajiri ya Kihindi kwa jina GUpta wanaotuhumiwa kutumia urafiki wao na rais kushawishi uteuzi wa mawaziri bungeni na kujipatia kandarasi za serikali.
Familia ya Gupta na Bwana Zuma wamekana makosa yoyote lakini tuhuma hizo bado zinaglipo.
18 Disemba 2017: Mrithi wa Zuma ateuliwa
Katika ushindani wa kumrithi Zuma baada ya miaka 10 kama kiongozi wa ANC,Cyril Ramaphosa naibu rais wa Afrika kusini aliibuka mshindi. Alirithi uwenyekiti wa chama hicho katia wakati ambapo kinapoteza umaarufu chini ya utawala wa Zuma.
Alifanya kampeni kama mgombe aliye dhidi ya Zuma, na aliahidi kukabiliana na rushwa. Ushindi wake ulimueka katika nafasi ya nguvu dhidi ya rais, na kumfanya mgombea mkuu anayeweza kumrithi.
Chanzo. bbc
Hospitali mbili zapigwa mabomu nchini Syria
Majeshi ya serikali ya Syria na Mshirika wake Urusi yamezipiga hospitali mbili, jengo moja la ghorofa na sehemu zingine ambazo zililengwa na majeshi hayo katika jimbo la waasi la Idlib.
Wanaharakati leo hii Jumatatu, wameelezea kuwa mashambulio hayo yanafanyika hasa baada ya wapiganaji wa kundi la Al Qaida kuidungua ndege ya kijeshi ya Urusi mnamo siku ya Jumamosi iliyopita karibu na mji wa Saraqeb na kumuua rubani wa ndege hiyo. Na kutokea hapo mashambulio dhidi ya maeneo ya waasi yameongezeka.
Kwa mujibu wa wanaharakati wa haki za binadamu, takriban watu 23 wameuawa kutokana na mashambulizi hayo ya majeshi ya serikali ya Syria baada ya kuushambulia ngome za waasi katika vitongoji vya Ghouta Mashariki, karibu na mji mkuu wa Damascus.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa watoto wanne ni miongoni mwa wale waliouawa, Shirika linalofuatilia haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake mjini London, Uingereza limesema watu wengine tisa wameuwawa baada ya soko lililo katika mji wa Beit-Sawa kushambuliwa.
Wakati huo huo jeshi la Uturuki limesema msafara wa askari wake umeingia katika jimbo la Idlib kaskazini magharibi mwa Syria kwa ajili ya kuanzisha kituo kipya cha uchunguzi kwa lengo la kudhibiti vurugu chini ya makubaliano na Urusi. Jeshi hilo limesema kuwa kituo hicho ni cha nne kufunguliwa katika jimbo la Idlib kulingana na mazungumzo ya amani ya mjini Astana, Kazakhstan.
Idlib, ambayo kwa kiasi kikubwa inadhibitiwa na vikosi vya waasi wa Kiislamu, ipo upande wa magharibi mwa eneo la Afrin ambalo linadhibitiwa na Wakurdi ambalo linalengwa zaidi katika operesheni kubwa ya kijeshi inayofanywa na jeshi la Uturuki.
Jamii ya kimataifa imeelezea wasiwasi wake kuhusu hatima Ghouta Mashariki wakati ambapo majeshi ya serikali ya Syria na washirika wake Urusi wanaendelea kuushambulia mji huo na kusababisha upungufu mkubwa wa chakula pamoja na madawa hali ambayo imesababisha utapiamlo.
Assad na washirika wake wameongeza kasi katika vita hivyo vya miaka saba, na wameweza kuyateka maeneo kadhaa na kuwafurusha waasi kutoka kwenye maeneo mengi na miji mikubwa, hali iliyoyalazimisha baadhi ya makundi kujisalimisha mnamo mwaka jana.
Wakati hayo yakijiri Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alikutana leo hii na kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis katika mji wa Vatican. Polisi walikuwa na kibarua kigumu cha kuwadhibiti waandamanaji wakati ambapo hisia zinaendelea kuwa kali kutokana na operesheni ya Uturuki dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi ndani ya Syria. Papa Francis alimpa Erdogan kisanamu kilichokuwa na picha ya malaika anayemkaba shetani - ikiwa ni ishara ya kukumbushia amani na haki.
Mwandishi: Zainab Aziz/APE/AFPE
Mhariri: Gakuba Daniel
Chanzo. Dw.de