- Hiyo ni hatua ya kwanza ya utekelezaji wa azimio lake la kuivamia Syria kijeshi wakati ikiendelea na mkakati wa kutafuta “ushirikiano wa kimataifa” ili kutimiza adhma ya kuivamia Syria na kudhibiti matumizi ya silaha zinazodaiwa kuwa za sumu.
New York. Marekani imeanza kupeleka meli za kivita katika eneo la Mashariki mwa Bahari ya Mediterania, kama sehemu ya maandalizi ya hatua za kijeshi dhidi ya Serikali ya Syria.
Hiyo ni hatua ya kwanza ya utekelezaji wa azimio lake la kuivamia Syria kijeshi wakati ikiendelea na mkakati wa kutafuta “ushirikiano wa kimataifa” ili kutimiza adhma ya kuivamia Syria na kudhibiti matumizi ya silaha zinazodaiwa kuwa za sumu.
Wakati meli hizo za kivita zikiwa na makombora na vifaa vya kisasa zikirandaranda kwenye bahari hiyo, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Chuck Hagel alisema jana kwamba hiyo ni sehemu muhimu katika mpango wa kukabiliana na suala la matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria, licha ya wabunge wa Uingereza kupiga kura dhidi ya hatua za kijeshi.
“Mpango wetu ni kuendelea kutafuta ushirikiano wa kimataifa utakaochukua hatua kwa pamoja,” Hagel alisema katika mkutano na wanahabari.
Alisema Rais Barack Obama ameendelea kuomba ushirikiano wa Ufaransa, baada ya wabunge wa Uingereza wa kukataa kuhusika katika mashambulizi yoyote ya kuadhibu Syria.
“Kila taifa lina jukumu la kufanya uamuzi wake,” Hagel alisema wakati wa ziara nchini Ufilipino. Tunaendelea kushauriana na Uingereza na washirika wetu wote. Mazungumzo hayo yanajumuisha mbinu za pamoja kukabiliana na shambulizi hili la kemikali nchini Syria,” alisema.
Alisema anaona taifa lake linawajibika zaidi katika matumizi ya silaha za kemikali dhidi ya watu wasiokuwa na hatia.
Mipango ya Marekani kuunda ushirikiano wa kimataifa ili kutekeleza shambulizi la kijeshi dhidi ya Syria ilitibuka wakati wabunge mjini London walipopiga kura Alhamisi dhidi ya matumizi ya mabavu kuadhibu shambulizi la kemikali wiki iliyopita nje ya Damascus
Chanzo :- Mwananchi.
No comments:
Post a Comment