Timu za Bagamoyo Stars na Rungwe Veterani jana zilipambana katika mchezo wa fainali uliozikutanisha timu hizo, katika mchezo huo ambao ulikuwa mgumu na timu zote zilionekana kucheza kwa tahadhari kubwa, mbele ya Mgeni rasmi wa mchezo huo Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Crispin Meela.
Matokeo ya mchezo huo yalikuwa ni kufungana goli 1-1, timu ya Rungwe Veterani ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata goli la kuongoza katika dakika ya 20, goli liliofungwa na Furaha Peter baada ya kutokea piga nikupige katika goli la Bagamoyo Stars.
Baada ya kufungwa goli hilo vijana wa Bagamoyo Stars walikuja juu na kulishambulia goli la Rungwe Veterani kama nyuki huku wakishangiliwa kwa nguvu na mashabiki wao waliojaa katika uwanja wa Tandale, ilikuwa ni katika dakika ya 35 ya kipindi hicho hicho cha kwanza ndipo mchezaji wa Bagamoyo Stars, Kabuje Niyonzima alipoisawazishia timu ya hiyo kwa goli la kichwa baada ya krosi nzuri ilichongwa toka upande wa kulia wa uwanja.
Mpaka kipenga cha kumaliza mpira kinapulizwa na mwamuzi wa mchezo huo Enzi Mwasambili, Bagamoyo Stars 1 na Rungwe Veterani 1. Timu hizo zinarudiana leo jioni katika uwanja wa Tandale Ili kukamilisha mchezo huo ambao jana ilishindikana kuongeza dakika 30 za ziada baada giza.
Chini ni picha za matukio mbalimbali ya mchezo huo.
Mgeni rasmi katika mchezo wa fainali, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Crispin Meela, mwenye miwani akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Bagamoyo Stars kabla ya mchezo kuanza hapo jana.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Crispin Meela mwenye miwani akiwa na kikosi cha timu ya Rungwe Veterani kabla ya mchezo wa fainali kuanza.
Mgeni rasmi katika mchezo huo, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Crispin Meela akitoa nasaha zake kwa wachezaji kabla ya mchezo kuanza.
Wachezaji wa timu za Rungwe Veterani na Bagamoyo Stars wakisalimiana kabla ya mchezo kuanza
Wachezaji wa timu ya Rungwe Veterani wakiwa na mtoto Madodi Bashiru Madodi ambaye ni mtoto wa Diwani wa Kata ya Bagamoyo Bashiru Madodi
Wachezaji wa timu zote mbili walimuomba mungu kabla ya mchezo kuanza
Mashabiki na vioja vyao katika mchezo huo
Polisi wakiwadhibiti mashabiki wa timu ya Bagamoyo Stars.
Mashabiki wa timu ya Bagamoyo Stars, Sikujua Ahmad Pontia na Gas Mwamakamba wakifuatilia kwa karibu mpambano huo.
Diwani wa kata ya Bagamoyo Bashiru Madodi naye alikuwepo uwanjani ili kukipa moyo kikosi cha timu ya Bagamoyo Stars.
Picha zote na Basahama blog.
No comments:
Post a Comment