Sunday, August 25, 2013
JE BAGAMOYO STARS ITATUVUSHA HAPA?.....
MHESHIMIWA DIWANI, BASHIRU MADODI (BASAHAMA-KUSHOTO KABISA) AKIWA NA KIKOSI KAMILI CHA BAGAMOYO STARS. (MAJINA MENGINE BADO YANASHUGHULIKIWA) |
Swali kubwa kwa wanabagamoyo, ni nini kifanyike ili waweze kucheka ZAIDI ya walivyocheka siku za Timu za zamani kama Mwenge, Chai na Kurugenzi, ama zaidi TUKUYU STARS maarufu kama Banyambala walioweza kupanda daraja na kutwaa ubingwa wakiwa na wachezaji na Kocha mzawa wa Tanzania. Tanki lina hili la kuchangia.
Mi si wa enzi za mwenge, Ila namjua Mwenge.
Alipenda atupange, Kwa pamoja tujijenge.
Mbiu yetu tuitunge, Tuijue tuichunge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.
Umoja si tuujenge, Lengo kuu lake Mwenge.
Kurudi enzi za mwenge, Kwa hitaji tujipange.
Chai pia kama Mwenge, Kurugenzi kama Mwenge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.
Aje diwani tupange,Waje wabunge turinge.
Ni nini hasa tupange? Na Tukuyu tuijenge.
Wazo bora tulitunge, Tukuyu yetu tujenge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.
Wazo langu mlipinge, Mkiliona si tenge.
Moja Uchumi tujenge, Tuubebe kama Mwenge.
Tupende kwetu tujenge, Tupeleke na vitenge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.
Wageni pia wajenge, Tuwafanye wasipange.
Chai yetu tuichunge, Timu yetu iijenge.
Pili shule tuipange, Michezo yetu ichunge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.
Iwe moja kama mwenge, Tuipende tuijenge.
Akili yangu ya kenge, Najihisi siko tenge.
Na jihisi nikapenge, Niwaache muyapange.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.
Madiwani na wabunge, Mawazo ,wapi? Tujenge.
Tuanzie kwake Page, Tusimuache Kapange.
Walio kwa Kaijage, Mje wote tuyapange.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.
Na mlio kwa Kitenge, Hima njooni tujenge.
Msaidie tupange, Nyumbani tusikutenge.
Na Vijana tujipange, Wazee wawashe mwenge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.
Na Udini tuupinge, Ukabila tuutenge.
Mbeleni sana tusonge, Kwa mwanga wa wetu mwenge.
Wa vijembe tuwatwange, Hata awe Mwakitwange.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.
Ania tusimpinge, Kwa pamoja tumkinge.
Cha mno sisi tuchunge, La asiwe na Ukenge.
Hakika aliye bwege, Tuje hima tumtwange.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.
Muhimu vyetu vihenge, Kaka kuuwasha mwenge.
Timu mpya muipange, Mawazo yake mchunge.
Aseme vipi tupange, Turudi enzi za Mwenge.
Tukuyu na tujipange, Turudi enzi za mwenge.
No comments:
Post a Comment