Social Icons

Monday, 2 September 2013

MADODI, AWAONYA VIJANA JUU YA MATUMIZI YA NGUVU YA UMMA.....

 






















 Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Mbeya Bashiru Madodi akimwaga Sera za chama chake.
  






















Sambwee Shitambala akipiga saluti mbele ya jiwe la Msingi la vijana wakereketwa wa CCM tawi la Sogea mjini Tunduma alilolifungua jana.

  Wanachama wapya wa chama hicho wakila kiapo Ndalambo baada ya kukabidhiwa kadi zao za CCM
 






















Viongozi wakitamka kiapo cha chama hicho.























 Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM wa kata ya Ndalambo wakisikiliza hotuba.
 






















Kada wa CCM Sambwee Shitambala akiipa tafu CCM mjini Tunduma.























                          Viongozi wa CCM wakipata maelezo Ndalambo.

Na mwandishi wetu.

Katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya Bwana Bashiru Madodi, amesema Nguvu ya umma inaendelea kuiliza ikiwa ni pamoja na Tanzania.

Hayo ameyaeleza jana katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika juzi katika mji mdogo wa Tunduma uliopo wilaya ya Mbozi mkoani hapa, ambako ni ngome ya Chadema.

Madodi aliwaambia wananchi na wanachama wa chama hicho waliokuwa wamekusanyika katika viwanja vya CCM kuwa kauli mbiu ya Chadema ya nguvu ya umma imeendelea kuiliza ulimwengu kabla ya vyama hivyo kuwapo Tanzania.

Alisema kuwa watu wasiokuwa na nia njema na watenda mema hutumia vibaya neno nguvu ya umma kwa kuhamasisha maovu katika jamii ili kujipatia umaarufu bila kujali athari zinazoweza kujitokeza katika Taifa.

Hivyo aliwaasa wananchi wa Tunduma kuwa makini na kauli mbiu ya nguvu ya umma kwasababu ikitumika vibaya inaweza kuliingiza Taifa katika machafuko.

Kwa upande wake Kada wa chama hicho Sambwee Shitambala aliyekuwa ameongozana na Katibu mwenezi huyo, alisema yeye aliamua kukihama Chadema kutokana na kile alichodai kuwa kutaka kuuawa.

Alisema hawezi kuja kuyasema hayo akiwa kaburini na ndiyo maana aliamua kuweka wazi suala hilo na kuongeza kuwa chama hicho kilimmaliza Chacha Wangwe lakini yeye hawezi kumalizwa kirahisi kama wabaya wake walivyokuwa wakifikiri.

Kabla ya kufika eneo hilo la Tunduma, chama hicho kilifanya mkutano wake katika kata ya Ndalambo wilayani humo na kuwasihi wananchi kujitokeza kuchangia maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Sekondari na maendeleo mengine.

Baada ya kumaliza kuhamasisha maendeleo hayo wanancwakapewa fursa ya kuuliza maswali ambapo kati ya maswali yaliyoulizwa ni pamoja na suala la matibabu kwa wazee wenye umri zaidi ya miaka 60.

Mwananchi Michael Tweve (75) ambaye alisema ni mwasisi wa chama hicho aliuliza iweje Serikali iendelee kuhamasisha michango kwa wananchi kuchangia mwakati wazee waliojenga nchi wanashindwa kuthamniniwa ikiwa ni pamoja na kulipishwa fedha katika matibabu?

Akijibu swali hilo, Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Mbeya Bashiru Madodi alisema Serikali imetoa taratibu za wazee wote wenye umri wa miaka 60 kutibiwa bure hivyo alimuomba mwananchi huyo kuwasiliana na Ofisa mtendaji wa kijiji chake huku akimsimamisha Ofisa huyo ambaye alisema atampa barua mzee huyo ya kutibiwa bure katika zahanati iliyopo katika Kijiji chake.

Ziara hiyo ililenga kuhamasisha maendeleo katika kata hizo za Ndalambo na Tunduma huku chama hicho kikishukuru kwa kupewa kura ambazo hazikutosha katika nafasi za udiwani na Ubunge Jimbo la Mbozi Magharibi. 

Chanzo :- Mbeya yetu.

No comments:

 
 
Blogger Templates