Msanii wa muziki wa kizazi kipya, ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga za muziki huo,Neylee akiimba kwa hisia jukwaani kuu wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea kwa shangwe ndani ya uwanja wa Sokonine.
Wakazi wa jiji la Mbeya wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Sokoine,ndio kwanza shoo inaanza ambapo msanii aliyewahi kuiwakilisa shindano la BSS,Walter Chilambo ndiye aliyefungua pazia la onesho hilo.
Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea kwenye uwanja wa Sokoine,Mkoani Mbeya
Mama wa miduara ya Kibongofleva,Shilole akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Sehemu ya umati wa watu.
Mkali mwingine wa hip hop (bongofleva), Ney wa Mitego akikamua jukwaani ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013,kwenye uwanja wa Sokoine, mjini Mbeya.
Wakazi wa jiji la Mbeya wakitoa heshima kwa baadhi ya wasanii waliotangulia mbele za haki, kwa kuwasha tochi za simu zao.
Rich Mavoko na skwadi lake wakilishambulia jukwaa.
Shilole akiimba jukwaani.
Wasanii mahiri katika miondoko ya hip hop, Stamina na Young Killer wakilishambulia jukwaa la Serengeti fiesta 2013, ndani ya uwanja wa Sokoine.
Ni shangwe tu kwa wakazi wa jiji la Mbeya ndani ya uwanja wa Sokoine.
Mmoja wa msanii mahati wa kizazi kipya,Ommy Dimpo akiwaimbia mashabiki wake singo yake mpya iitwayo Tupogo ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013.
Mkali wa kukamua mangoma kutoka Clouds FM,Dj Zero akiwarusha maelfu ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wanaondelea kumiminika kwenye uwanja wa Sokoine.
Msanii aliyewahi kuwakilisha shindano la BSS,Walter Chilambo ndiye aliyefungua pazia la onyesho hilo, pichani akitumbuiza mbele ya mashabiki wake.
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia yanayojiri kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Mkali wa Mahaba,a.k.a tajiri wa Mahaba kutoka mwambao wa Pwani,Cassi Mganga akiwaimbisha mashabiki wake ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013,kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Chanzo :- Michuzijr
No comments:
Post a Comment