Akitoa maelezo katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Crispin Meela, alisema amesoma kablasha lote la hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kuna hoja ambazo hazikutakiwa kuwa hoja lakini zimekuwa hoja kwa sababu ya uzembe wa baadhi ya watendaji wetu.
Akitoa mfano alisema kuna hoja ameiona inahusu kutokuwepo risiti ya malipo, lakini baada ya mkaguzi kuhoji risiti ilipatikana, kwa hiyo hayo ni matatizo ya watendaji wetu kutokuwa makini na kusababisha hoja zisizo na msingi, alisema Mhe. Meela.
Hivyo mkuu wa wilaya aliwataka watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kuwa makini wakati wote wa kazi zao za kila siku.
Picha chini ni matukio mbali mbali wakati wa kikao cha baraza maalumu la Halmashauri ya Rungwe.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Alfred Mwakasangula akifungua kikao cha
Baraza Maalumu la Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Noel Mahyenga akitoa maelezo
Ya awali kabla ya kumkalibisha Mwenyekiti wa Halmashauri kufungua kikao.
Mtunza Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Ndugu. Shirima akikiongoza Kikao wakati
wa kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali katika Halmashauri hiyo kwa mwaka
2011-2012
Mjumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Bashiru Madodi
akisoma nyaraka za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali katika Halmashauri hiyo
Kwa mwaka 2011-2012
No comments:
Post a Comment