YALIYOJIRI KWENYE MECHI YA MAN U NA LIVERPOOL.....
Kipigo tu: Liverpool wameanza vizuri ligi kuu soka nchini kwa kushinda mechi zote tatu za kwanza baada ya leo hii kuwafunga Man United bao 1-0 katika uwanja wao wa Anfield.
David Moyes ameshindwa kupata ushindi wa kwanza Anfield kufuatia kushindwa kushinda katika mechi 12 alizocheza katika dimba hilo akiwa na klabu yake ya zamani ya Everton.
Hali ni mbaya zaidi kwa Moyes, kwani Wayne Rooney atakaa nje ya dimba kwa wiki chache zijazo kutokana na kuumia kichwa katika mazoezi ya jana, na dirisha la usajili linafungwa kesho usiku na Moyes bado anahitaji kusajili kwa mara ya kwanza.
Sehemu sahihi: Sturridge alimalizia kazi nzuri ya beki Daniel Agger
Kwenye kiwango cha juu: Sturridge amefunga katika mechi zote nne za Liverpool msimu huu
Mwanzo mtamu: Daniel Sturridge aliipatia Liverpool baada la kuongoza kwa njia ya kichwa katika dakika ya 4
Endelea kutizama picha zaidi kwa kubofya hapa chini
Chanzo:- Pamojapure
No comments:
Post a Comment