Social Icons

Friday, 11 October 2013

MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO AFUNGUA MAFUNZO YA WANA HABARI NYANDA ZA JUU KUSINI.


Mkuu wa mkoa Mbeya Abasi Kandoro akifungua mafunzo ya siku nne kwa waandishi wa habari wanyanda za juu kusini ya namna ya kuripoti habari za unyanyasaji wa kijinsia mafunzo hayo yanatolewa na chama cha waandishi wa habari Wanawake (TAMWA) 
Martha Ngwila mwezeshaji toka TAMWA  akimwelezea mkuu wa mkoa mbeya Abasi Kandoro  jinsi wanahabari watakavyo pata mafunzo hayo
Wanahabari wakiwa makini kumsikiliza mkuu wa Mkoa wa Mbeya

 

Jesse Kwayu mwezeshaji katika mafunzo hayo
                                                   Picha ya pamoja

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kinatoa mafunzo kwa wanahabari zaidi ya 20, wa nyanda za juu kusini ambao wanaandaliwa kwa lengo la kuripoti habari za unyanyasaji wa kijinsia (GBV) 

Wanahabari hao watapata mafunzo hayo ikiwa ni hatua ya kuandaa kundi maalumu la wanahabari ambalo litakuwa likiripoti kwa kina habari dhidi ya vitendo vya kikatili kwa wanawake na wasichana ambao ndio waathiriwa wakubwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Chanzo:- Mbeya yetu.

No comments:

 
 
Blogger Templates