Social Icons

Tuesday, 12 November 2013

CHADEMA INAPUMULIA MASHINE


Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na mtindo wa kurushwa kwa shutuma mbali mbali kutoka kwa viongozi wajuu wa CHADEMA wakitumia majina bandia kumuelekezea ndugu zitto kabwe. 

Kwa makusudi kabisa viongozi hao wakiongozwa na mwenyekiti, katibu mkuu na wakurugenzi kadhaa wamekuwa wakirusha kila aina ya shutuma humu mtandaoni lakini kwa hofu kubwa ndio maana wanajificha kwa kutumia akaunti bandia.
Jana na juzi nimepokea sms, emails na simu nyingi sana kuhusu hiki kinachoitwa ripoti ya siri ya SLAA, MBOWE NA WAGAZA WENGINE dhidi ya ZITTO zikisema namie nimetajwa humo kuwa ninashirikiana na Zitto kukihujumu CHADEMA.

Bahati mbaya sana, hakuna ripoti ama shutuma zozote anazopelekewa Zitto kutoka kwa hawa majamaa ambazo hazinitaji, na kwentye hii nayo nimeshuhudia nikitajwa mara nyingi kupokea pesa kutoka kwa Zitto kukihujumu chama.

Bahati mbaya zaidi ni kwamba wafadhili wa mkakati huu ''OPERESHENI ONDOA ZITTO KWENYE HOJA ZENYE MASLAHI YA TAIFA'' wamekosa njia sahihi ya kutumia, wamekuwa wakiwatumia watu wale wale ambao kwa zaidi ya miaka na miaka tumekuwa tukikitetea chama kuwa si cha namna hiyo.
  
Kitendo cha MBOWE na SLAA kuwatumia JOSHUA NASSARY, GODBLESS LEMA, MAMUYA na wengine, kinauthibitishia umma wa watanzania kuwa sio kweli kwamba zitto ni tatizo kwenye CDM, kitendo hiki cha kuwatumia watu wanaolalamikiwa kuwa wanabebana kimisingi ya ASILI ya wanakotokea kinatuthibitishia watanzania kwamba CHADEMA ni chama cha watu wa eneo hilo. 
lakini wamefeli zaidi kumtumia LEMA kuwa eti ni KAMANDA mwenye uchungu na CHADEMA kuliko ZITTO, hiki pia ni kielelezo cha upeo mdogo wa kufikiri kwa watu hawa.
  
ZITTO ni mjenzi wa NYUMBA inayoitwa CHADEMA, Zitto ameshiriki mpaka kuijenga CHADEMA tangu ikiwa nyumba ya nyasi, mpaka ikawa ya udongo, ikaja ikawa ya tofali za kuchoma na sasa CHADEMA ni nyumba ya VIGAE, LEMA ni mpangaji tu kwenye hii nyumba CHADEMA, hakuna jinsi yoyote mpangaji akawa na uchungu na nyumba kuliko mwenye nyumba, hakuna na haitaka itokee.
  
LEMA ni mpita njia tu kwenye CHADEMA, Kamwe hawezi kuwa na uhalali wa kumsema na kumtukana mtu aliyekijenga chama kilichomsaidia kumfikisha hapo alipo.
  
Nani humu jukwaani alikuwa anamfahamu LEMA mwaka 2006, NANI?. nani alikuwa anafahamu lolote kuhusu lema 2007,2008,2009 mpaka 2010 kabla ya uchaguzi mkuu?
  
Nani anayemfahamu Lema kipindi hicho kwenye CHADEMA?. LEMA ni TUNDA LA KAZI NZURI YA KISIASA ILIYOFANYWA NA ZITTO KABWE. 
Wakati Zitto anahangaika kushirikiana na viongozi wenzake kuijenga CHADEMA, LEMA alikuwa ni KIBARAKA wa MZEE AUGUSTINO MREMA wa TLP.
  
Wakati Zitto anaibua hoja za msingi zenye maslahi kwa Taifa kama BUZWAGI na nyinginezo, LEMA bado alikuwa hata hajui chaguo lake la kisiasa katika nchi hii, yaani lema hakuwa akijua aende chama gani cha siasa.
  
Wanaokumbuka na wenye akili timamu watakubaliana nami kuwa ni zitto aliyekwenda Arusha kumnadi mgombea wa TLP wa udiwani wakati wa uchaguzi wa marudio 2008 huku lema akiwa mpiganaji kibaraka wa augustino mrema wa TLP. 
Wanachadema wanafahamu kuwa wakati tunafanya uchaguzi wa ndani ya chama mwaka 2009 LEMA ndio kwanza alikuwa ana siku 4 za uanachama wake ndani ya CHADEMA
 
LEMA anapita tu njia CHADEMA kwa kuwa yeye ni msaka tonge tu kama wasaka tonge wengine, ndio maana alipita NCCR, ILIPOKUFA AKAKIMBIA, AKAPITA TLP ilipokufa akakimbia na sasa yupo CHADEMA nayo ikiyumba sidhani kama hataacha kukimbia. LEMA hana hadhi ya kukubali kutumiwa na kina MBOWE na GENGE lake kumshambulia ZITTO, hana hiyo moral authority. mpangaji hawezi kuwa na uchungu sawa na mwenye nyumba, 

Leo CHADEMA ikipasuka, leo CHADEMA ikiyumba, ikitetereka atakayeumia ni ZITTO aliyeijenga na si LEMA aliyeidandia. 
Nasisitiza hapa kuwa Hakuna namna yoyote ile inayoweza kumshusha Zitto kwenye heshima yake aliyojijengea kwa kusambaza uwongo wa namna hii, hakuna na hitakaa itokee. 

Hakuna namna yoyote ile ya kumshusha zitto kwenye orodha ya wanasiasa bora na makini kwa kuwatumia watu kama kina lema na nassary ambao wakati wanaomba kura waliomba wakisema WATUMWE WAENDE BUNGENI WAKAWE KAMA ZITTO.
  
Again, ni rahisi sana kumshusha zitto kama kuna lolote baya amelifanya lisilo na maslahi kwa umma wa watanzania. ni Rahisi sana kumshusha na kumchafua zitto kama njia anazopita sio sahihi, LAKINI SIO KWA UWONGO WA KIPUUZI NAMNA HII. 

Pamoja na kukiri kuwa Zitto ndiye mwanasiasa ninayemuamini na anayenivutia kuliko mwanasiasa yoyote Tanzania, na pamoja na ukweli kwamba zitto sio rafiki kwangu bali ni kaka yangu. Lakini sijawahi hata siku moja kupokea pesa kutoka kwake ama kwa MPESA au kwa TIGO PESA tangu nimefahamiana nae mpaka leo. 

Ndio maana ninawapa pole MBOWE na vijakazi wake wanaotunga uwongo wa namna hii bila hata kujifikiria mara mbili mbili. 
Uchaguzi mkuu wa ndani ya chama unawatia homa kundi la Mbowe na wagaza wenzake, uchaguzi huo unawafanya waweweseke kutwa kucha, mchana usiku.
  
Hakuna sababu ya kuhangaika na Zitto, wanachadema wapo na wataamua kwa yale mliyoyafanya, Zitto yeye ameshawaacha mile 2000 kwenye siasa zenye tija kwa Taifa.
  
Nimelazimika kuandika maneno haya baada ya kuona kuna huu ujinga unaofumbiwa macho na viongozi wa CDM kwa makusudi kabisa.  iliwahi kuandikwa humu mtandaoni kuwa ''Zitto ni maporomoko ya Nile, hayazuiliki kwa kifusi'' amewashinda na anaendelea kuwashinda. 

Narudia tena kusema KWENYE HILI TAYARI ZITTO AMESHASHINDA.
  
1. Aliwashinda kwenye uwongo wenu mliokuwa mkiusambaza wa kupokea rushwa TANESCO lilipobumbuluka wakina mnyika, lissu na nassary wote waliufyata.  
2. Aliwashinda mlipounda tume ya kumchunguza kuasisi migogoro ndani ya chama. 
3. Alishinda kwenye hoja ya Buzwagi 
4. Alishinda kwenye hoja ya kuwatimua mawaziri vilaza kwa kutoa hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu 
5. Amewashinda kwenye hoja ya kuficha mali nje ya nchi (kama mabilioni ya uswisi) leo mnatapa tapa kwa kuwa bossi wenu anamiliki mali uarabuni. 

Naomba niwakumbushe kuwa zitto ndiye mwanasiasa pekee wa upinzania anayeweza kuilazimisha serikali ikafanya maamuzi kutokana na hoja yake hata kama haipendi kufanya hivyo kwa wakati huo. Mfano ni hiyo hapo juu. 

Naomba nihitimishe kwa kusema, ni kweli kwamba uwongo unapanda ghorofa kwa kutumia klifti, lakini hauwezi kubadilisha ukweli wa mambo daima dumu. uwongo utabaki kuwa uwongo tu na utaendelea kupuuzwa milele na milele. 

Ndimi,  
Habibu Mchange
mchangehabibu@yahoo.com


No comments:

 
 
Blogger Templates