Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipungia wananchi wakati akirejea kijiji cha Lituhi kwa kuvuka mto Ruhuhu kwa mtumbwi, baada ya kutoka kuwasalimu wakazi wa kijiji cha Kipingu wilayani Ludewa,wengine pichani ni Dk.Asha-Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho.
Sehemu ya eneo la mto Ruhuhu,kivuko cha mto huo kimeshindwa kufanya kazi kutokana na kina chake cha maji kupungu,Ndugu Kinana alisema kuwa kivuko hicho hufanya kazi kwa muda wa miezi minne tu kwa mwaka,miezi mingine yote halifanyikazi kutokana na kina cha maji kupungua,hata hivyo Ndugu Kinana alieleza kuwa Serikali itajenga daraja kufuatia ahadi aliyoitoa Mh Rais Jakaya Kikwete kwa wakazi wa kijiji hicho.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Lituhi wakiwa ndani ya Mtumbwi wakitokea katika kijiji cha Kipingu wilayani Ludewa,shoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Ndugu Ernest Kahindi wakivuka kwa mtumbwi mto Ruhuhu kuelekea kijiji cha Kipingu wilaya ya Ludewa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya jinsi ya kutumia vifaa vya maabara katika kufanikisha kutambua kemikali kutoka kwa wanafunzi wa kidato cha nne Erasto Ndumba na Stella Hyera wa shule ya sekondari ya Kata ya Mtakatifu Paul kata ya Liuli wilaya ya Nyasa.
Wakazi wa kijiji cha Lituhi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Lituhi ambapo wanachama zaidi ya 400 wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi nyumba za madaktari zilizochini ya mradi wa Taasisi Benjamini Mkapa katika kituo cha afya Mkili kata Liundi wilayani Nyasa.
Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba akimtambulisha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kama Ndugu yake wa karibu kwani mafanikio yake yametokana na mchango mkubwa wa Marehemu Mzee Nnauye ,Pia Komba alimuelezea Kinana kama mmoja wa walimu wake wazuri wa masomo ya kijeshi pamoja na siasa.
nyumba za madaktari zilizochini ya mradi wa Taasisi Benjamini Mkapa katika kituo cha afya Mkili kata Liundi wilayani Nyasa.
Chanzo:- Michuzijr
No comments:
Post a Comment