Social Icons

Wednesday, 13 November 2013

WAKULIMA WA CHAI RUNGWE WAAMBIWA HAKUNA RUKSA YA KUNG'OA CHAI

KIWANDA CHA CHAI KATUMBA KINACHOMILIKIWA NA WAKULIMA WADOGO KWA HISA  YA 30% LAKINI MATARAJIO NI KUFIKIA HISA 49%  KUFIKIA MIAKA MIWILI IJAYO
  
BAADHI YA WANACHAMA WA RSTGA WAKISIKILIZA MAADA KWA MAKINI
KWAKUWA NI MWAKA WA UCHAGUZI RSTGA NI UMOJA UNAOENDESHWA KWA DEMOKRASIA YA KUCHAGUA VIONGOZI KILA BAADA YA MIAKA MINNE HIVYO HAPA WAJUMBE WA SKIMU INAYOUNDWA NA VIJIJI WAKIWA KATIKA CHAGUZI ZA KUCHAGUA VIONGOZI WAO HUKU WAKIENDELEA NA MAFUNZO YA JINSI YA KUTUNZA MASHAMBA KUTOKA KWA WATAALAM WA WATCO
MKULIMA BORA WA CHAI TANZANIA JOSEPHEN NJUNUSI AKIWA SHAMBANI KWAKE SHAMBA ALILOKUWA ANAMILIKI NA MUMEWE ZEFRINI NJUNUSI ILA KWA BAHATI MBAYA BAADA YA MASHINDANI NA WAO KUCHAGULIWA KUWA WASHINDI WAKISUBIRIA ZAWADI AMBAYO HUKABIDHIWA KATIKA SHEREHE YA NANENANE NA RAIS BASI KWA BAHATI MBAYA MZEE ZEFRIN NJUNUSI AKAFARIKI DUNIA 14/06/2013 NA ZAWADI TSH MILION MOJA KUKABIDHIWA MKEWE
NA HILI NDILO KABURI LA ZEFRINI NJUNUSI AMBAYE NDIYE MSHINDI WA SHAMBA BORA LA CHAI TANZANIA NA ZAWADI YAKE YA TSH MILIONI MOJA KUKABIDHIWA MKEWE

JOSEPHEN NJUNUSI AKIELEZA MAFANIKIO YA CHAI AMBAPO ANASEMA KUWA SHAMBA HILI WALINUNUA MWAKA 1991 YEYE NA MUMEWE LAKINI LIMEWAWEZESHA KUINUA KIPATO CHA FAMILIA KWA KUJENGA NYUMBA BORA, KUSOMESHA WATOTO SABA HADI NGAZI YA CHUO KUFUNGUA BIASHARA MBILI DUKA LA BIDHAA ZA NYUMBANI NA GROSALI ZOTE ZIKIWA NI MALI ZINAZOTOKANA NA SHAMBA LA CHAI, HIVYO AMEWATAKA WATU WANAOBEZA KILIMO CHA CHAI KUWA HAKINA MANUFAA NI UONGO ULIOPINDUKIA NA AMEWATAKA BAADHI YA WAKULIMA WANAOMMILIKISHA MASHAMBA YAO MWEKEZAJI MKUBWA KWA MIKATABA ISIYO NA FAIDA KWA MKULIMA KUACHA MAANA MKULIMA UNAGEUKA KUWA MANAMBA KATIKA SHAMBA LAKO MWENYEWE NA FAIDA ZA CHAI HUZIONI KWA KUWA UNAKOSA PEMBEJEO NA VIFAA VYA KUHUDUMIA SHAMBA PIA MKULIMA ANAKOSA HUDUMA WA WAGANI ZITOLEWAZO NA WATCO AMBAO NDIO WABIA WA KIWANDA CHA KUZALISHA CHAI WILAYANI RUNGWE

ILI KUONGEZA UZARISHAJI MPYA WATCO INAMIPANGO ENDELEVU YA KUANDAA VITALU VYA ZAO LA CHAI  KIKIWA TAYARI KWA KUPANDA AMBAPO KWA MWAKA HUU MICHE 1,500,00 HIVYO UONGOZI WA RSTGA UNATAMKO LA KUPINGA KUWA WAKULIMA WA CHAI RUNGWE WANAMPANGO WA KUACHA KULIMA CHAI NA NA MASHAMBA CHAI KUBADIRISHA ZAO LINGINE HIVYO MIKAKATI HII INAONYESHA WAKULIMA WA CHAI RUNGWE WALIVYO JIANDAA KUJIKOMBOA NA KUONGEZA KIPATO KUPITIA ZAO LA CHAI HIVYO TAMKO LA KUNG"OA ZAO LA CHAI NI LA WAKULIMA WACHACHE WENYE MASLAHI YAO KATIKA KULUDISHA NYUMA MAENDELEO NA JUHUDI ZA KILIMO CHA CHAO AMBAPO WAKULIMA HAO WALIOJITENGA NA UMOJA WA WAKULIMA WADOGO WA CHAI HAWAZIDI HATA 500, UKILINGANISHA WAKULIMA 15,000, WALIOUNDA UMOJA WAO NA KUFAIDIKA NA MAMBO MENGI YAPATIKANAYO NDANI YA UMOJA WA RSTGA

KITALI KIPYA CHA ZAO MBADALA LA MAPARACHOCHO KIKIWA TAYARI KWA KUPADIKIZA

ILI KUMUONGEZEA MKULIMA KIATO CHA UHAKIKA WATCO AMBAO NI WABIA WA WAKULIMA WAMEANZISHA ZAO MBADALA LA KUONGEZA UCHUMI NA KIPATO KWA MKULIMA LA KUZALISHA MAPARACHICHI AMABAYO YANA SOKO LA UHAKIKA NCHINI UINGERAZA
HUKI NI KIWANDA CHA KUSINDIKA MAPARACHICHI CHA WAKULIMA WADOGO AMBAPO NI WABIA WA WATCO


MOJA YA SEHEMU YA MASHINE YA KUSAGA CHAI KATIKA KIWANDA CHA CHAI CHA KATUMBA WILAYANI RUNGWE

SEHEMU YA CHAI ILIYOZALISHWA KIWANDA CHA KATUMBA TAYARI KWA KUSAFIRISHWA KWENDA SOKONI AMBAPO SOKO KUU LA CHAI HII NI NCHI ZA ULAYA NA AFRIKA PIA TANZANIA  NA KWA KUJALI SOKO LA NDANI WATCO IMEANZISHA KIWANDA CHA KUSINDIKA CHAI KAVU CHA KYIMBILA TEA PACKING KINACHOTENGENEZA CHAI TAUSI


MTENDAJI MKUU WA RSTGA AKIELEZA JINSI CHAI WILAYANI RUNGWE KUWA NI ZAO KUBWA LA KIUCHUMI KWA KUWA NDILO ZAO PEKEE AMBALO MKULIMA ANAKUWA NA UHAKIKA WA KIPATO KWA KILA MWEZI HIVYO KUWA NA SHAMBA LA CHAI NI SAWA NA MTU ALIYEAJILIWA AMBAPO UMOJA WA WAKULIMA WADOGO WA CHAI WILAYANI RUNGWE RSTGA UNA WANACHAMA WAPATAO 15,000, AMBAPO WAKULIMA HAWA WANAHISA KATIKA VIWANDA VIWILI KATUMBA NA MWAKALELI KWA 30% NA MKAKATI NI KUWA IFIKAPO MIAKA MIWILI IJAYO WAKULIMA WATAKUWA NA HISA 49%

KWA KUTAMBUA FULSA ZA KUWEZESHA WAKULIMA KATIKA KAYA WAKULIMA WAMEPEWA MILIDI MBALIMBALI UKIWEMO MLADI WA UFUGAJI NGULUWE AMBAPO RSTGA IMETOA NGULUWE 350 KWA WAKULIMA NA MKULIMA AKIZALIWA WATOTO WATATU WA NGULUWE NA KUGAWA KWA WAKULIMA WENZAKE NGULUWE NA WATOTO WANAOBAKI WANAKUWA NI MALI YAKE MKULIMA NA KAWAIDA YA NGULUWE AKITUNZWA VYEMA ZAO LA KWANZA HUZAA WATOTO WASIPUNGUZA 12 NA BEI YA KUUZA WATOTO WANAOFIKIA MIEZI MITATU YA KUJITEGEMEA NI TSH 60,000/= HIVYO WAKULIMA WANANUFAIKA NA MARADI  HUU WA NGULUWE KWA KUONGEZA KIPATO CHA FAMILIA NA MATARAJIO YA MWAKA UJAO NI MRADI WA KOPA NGOMBE LIPA NGOMBE.
MWENYEKITI WA WAKULIMA WADOGO WA CHAI WILAYANI RUNGWE JOHNSON  MWAKASEGE  AKITOA TAMKO LA KUWA WAKULIMA WA CHAI RUNGWE HAWAWEZI KUNG'OA CHAI KWA SABABU AMABAZO HAZIELEWEKI AMBAPO AMASEMA KUWA ZAO LA CHAI NI NGUZO YA UCHUMI WILAYANI RUNGWE KWA SABABU NI ZAO PEKEE LINALO MFANYA MKULIMA KUPATA PESA KILA MWEZI KWA UHAKIKA HIVYO AMEWATAKA WAKULIMA WACHACHE WALIOJITENGA KWA MASLAHI YAO BINAFSI KUACHA KUTAMKA KUWA WAKULIMA WA CHAI RUNGWE WANATAKA KUNGOA CHAI NA KUBADILISHA ZAO LINGINE HIVYO TAMKO HILO SIO LA RSTGA AMBAPO RSTGA NI UMOJA IMARA ULIO NA WANACHAMA WAPATAO 15,000, NA UNA HISA 30% YA UZALISHAJI KATIKA KIWANDA CHA CHAI, WANACHAMA WA RSTGA WANA BIMA ZA AFYA, RSTGA WANAMILIKI SACCOS YAO AMBAYO INA MATAWI YAKE LWANGWA, MWAKALELI NA USHIRIKA PIA RSTGA NI MMILIKI MBIA WA KIWANDA CHA MAPARACHICHI, PIA RSTGA SASA IMEJENGA JENGO LA OFISI NA MAFUNZO AMBALO LIMEFUNGULIWA NA MAKAMU WA RAISI WA TANZANIA DR G BILALI NA SASA RSTGA INA KITUO CHA RADIO AMBACHO KIMEKAMILIA HATUA ZA UJENZI NA MITAMBO BADO TU KIBALI CHA TCRA ILI KIANZE KAZI, ZAIDI RSTGA IMECHANGIA TSH 1.7 BILION TANGU MWAKA 2002 HADI SASA KATIKA UJENZI WA SHULE , ZAHANATI, NYUMBA ZA WALIMU, MAJI SAFI, NA BARABARA HIVYO ZAO LA CHAI WILAYANI RUNGWE LINA FAIDA KUBWA KWA UCHUMI KWA FAMILIA NA WILAYA NZIMA PAMOJA NA TAIFA KWA UJUMLA.




Chanzo:- Kingotanzania

No comments:

 
 
Blogger Templates