Aisha alipofika nyumba ya nne aliingia kwa rafiki yake mmoja anaitwa Diana. Akamsimulia hali ilivyo nyumbani kwake na kile anachokifikiri…
“Hivi hapa siendi kwenye shughuli zangu, baada ya nusu saa narudi, najua tu kama kuna kitu nitawakuta katika mazingira tata,” Aisha alimwambia Diana.
JIACHIE MWENYEWE…
“Mh! Makubwa shoga. Hata mimi naungana na wewe, nenda kwa siri, fika kwa siri na chunguza kwa umakini, kama kweli wana lao jambo lazima utaliona,” alisema Diana.
***
Beka na shemeji yake baada ya kushikanashikana kwa muda mrefu huku wakihema kwa kasi, walipanda kitandani, chumbani kwa shemeji mtu huyo wakaendelea kula raha ya mahaba mazito kiasi kwamba, hakuna aliyekumbuka kwamba mwenye nyumba anaweza kuzuka wakati wowote kwani hawakuona hata sababu ya kufunga mlango.
Muda huo walikuwa kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo ambapo dada wa Aisha alikuwa amejiachia kwa lolote lile na maneno mengi ya kumfanya Beka kuweka akili zake zote kwake na kuachana na mkewe.
Hata staili za mwanamke huyo zilikuwa za kumteka akili Beka kwani kuna wakati alimlaza Beka chali halafu yeye akapanda baiskeli na kuanza kuzungusba pedeli kwa spidi ya ajabu hali iliyomfanya mwanaume huyo kupiga kelele yeye badala ya shemejiye…
“Basi mume wangu, usipige kelele sana,” alisema shemeji mtu akimwambia Beka kwa sauti yenye mahaba mazito huku akimwangalia kwa macho ya mlegezo na mahaba.Beka alishindwa kuvumilia kupekechewa baiskeli, akatangaza lakini shemeji mtu alipinga tangazo lako, ikabidi asitishe kupiga pedeli, akabadili mapozi, akajitegesha na ile ya mbuzi kupinga kutembea halafu Beka akamfuata kwa nyuma.
***
Aisha alikaa kwa Diana kwa muda halafu akaaga na kurudi nyumbani kwake akihakikisha anaingia ndani bila kujulikana labda kama atakuta mlango umefungwa.Ufungwe wapi! Aliukuta upo wazi, akazama ndani kwa kunyata. Alikuta sebule ipo kimya, akapita hadi jikoni ambako hakumkuta mtu, akakatiza hadi chumbani kwake, akafungua mlango, akakuta kitanda tu.
Aisha alibaini kuwa mume wake yupo ndani baada ya kuliona begi lake analopenda kulibeba begani. Akajua atakuwa ndani ya chumba cha dada yake, akasimama na kujipanga aingieje sasa!“Nikisema niingie kwa pupa naweza kusababisha makubwa, mimi nina hasira zangu. Dada ni mtu anayeweza kufanya lolote lile. Beka yeye hajui kupiga lakini pia ni mkorofi, hasa akikasirika…
“Lakini atakasirikaje wakati anayestahili kukasirika ni mimi? Hii si sawa, yaani nitendewe halafu niwe mpole! Haiwezekani.”Alitembea bila kusababisha kutambulika hadi kwenye mlango wa chumba cha dada yake ambapo aliweza kusikia minong’ono na mihemo ya kimahaba kutoka pande zote mbili. Tena aliweza kumsikia dada yake akiomboleza mapenzi.
Mwisho wa yote aliamua kugonga mlango ili kuwajulisha kwamba kuna mtu amesimama hapo mlangoni…
“Ngo ngo ngooo…”
Kule ndani, wote walishtuka kusikia hodi. Beka akamsukuma shemejiye kutoka kwake, akaanza harakati za kupanda juu ya kidirisha cha kuzamia darini ili atembee hadi akatokee kwenye bafu la chumba chake kama alivyofanya siku ya nyuma.
Aisha alishika kitasa cha mlango akazama ndani na kumkuta dada yake akihangaikia kanga, mumewe amejiingiza kwenye kidirisha nusu, yaani kuanzia kiunoni kwenda juu kumeingia lakini sehemu nyingine iliyobaki ikiwa nje.
Aisha aliachana na dada yake, akapanda kitandani na kumshika mumewe ili asimalizikie kuingia…
“Nimekuona, unakwenda wapi Beka?” alisema Aisha akiwa ameing’ang’ania miguu ya mumewe.
Ilibidi Beka ajiachie na kurudi kitandani. Hakuwa na nguo hata moja kiasi kwamba hata kama angefanikiwa kuchomoka, bado nguo zake zingekuwa ushahidi mkubwa kwamba alikuwemo ndani ya chumba hicho.
Dada mtu kuona hivyo, alitimua mbio hadi nje akiwa amejifunga kanga moja tu! Alikuwa akihema kwa kasi…
“Ooo…ooph…oooh!”
Baadhi ya majirani kule nje walianza kuingiwa na shaka kwa jinsi dada wa Aisha alivyotoka na kanga moja jambo ambalo si la kawaida.
Na yeye alipobaini kwamba amesimama nje na kanga alirudi ndani mbio, akafikia sebuleni. Bado Aisha na mume wake walikuwa chumbani kwake wakizozana…“Mimi ndoa basi tena. Wewe umeona dada yangu ni bora kuliko mimi, si ndiyo? Basi ishi naye,” alisema akilia Aisha. Beka alimshika mkono kwa sababu alikuwa akitaka kutoka…
“Nisamehe sana mke wangu, ni shetani tu alinipitia.”
“Shetani yupi? Shetani yupi!”
“Shetani wa vishawishi. Sasa na mimi ndiyo nimetambua ubaya wa huyu shetani, lengo lake lilikuwa kuvunja ndoa yangu na wewe.”
“Nimesema mimi ndoa na wewe basi tena,” alisisitiza Aisha.
Alifanikiwa kuchomoka kutoka kwenye mikono ya Beka alipofika sebuleni akamkuta dada yake amesimama akitetemeka…
“Mdogo wangu nisamehe sana mimi dada yako. Ni shetani tu alinipitia, naamini haitajirudia,” alisema dada mtu.Aisha hakumjibu, aliifuata simu yake aliyoiacha kwenye sofa na kubonyeza namba. Wakati huo, Beka naye alishatoka na kuwakuta sebuleni, mkewe na shemejiye. Aisha alikuwa ameipeleka simu sikioni akiashiria kutaka kuongea. Si Beka wala dada mtu aliyehisi anataka kuongea na nani.
Mara akaongea…
“Shikamoo shemeji…sijambo…si nzuri sana shemeji…shemeji nimemfumania mkeo na mume wangu…amini nakwambia…shemeji kumbe mkeo kaja kwa ajili ya…” kabla hajamaliza kusema Aisha huku akilia, Beka alimpokonya simu kwa kuikwapua…
“Ha! Dada ako amefikia huko?” uliuliza upande wa pili lakini sasa simu alikuwa nayo Beka…
“Haloo mkubwa…” alianza kusema Beka…
No comments:
Post a Comment