Dodoma/Dar/Mwanza. Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta jana alitoa dakika tano kwa Mjumbe wa Bunge hilo, Hamad Rashid Mohamed ‘kujibu mapigo’ dhidi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad.
Sitta alitoa fursa hiyo baada ya wenyeviti wa kamati kadhaa kumaliza kuwasilisha ripoti za vikao vyake.
“Tumefikia mwisho wa uwasilishaji wa ripoti za kamati lakini Hamad Rashid ana kitu cha kusema, karibu,” alisema Spika Sitta akimkaribisha na kuongeza kwamba
anatumia Kanuni ya 27(1) (e) ya Bunge hilo ambayo inampa mamlaka kuingiza shughuli yoyote anayoiona inafaa kushughulikiwa kwa wakati huo.
“Nimepata malalamiko kutoka kwa Hamad Rashid Mohamed kwamba hakutendewa haki katika moja ya vipindi vya TV. Nampa dakika zisizozidi 10,” alisema Sitta kabla ya kuahirisha Bunge hadi leo.
Hata hivyo, kitendo hicho kimekosolewa na mwanazuoni wa sheria na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, James Jesse, akisema: “Hatua hiyo si sahihi lazima ikemewe kwa kuwa hapa nchini hatuna sheria inayotoa haki ya kujibu mapigo bungeni kama ilivyo kwa nchi za wenzetu ambao mtu akishambuliwa bungeni anapata nafasi ya kujibu na majibu yake yanaingia kwenye hansard (kumbukumbu rasmi za Bunge).”
Alisema pamoja na kwamba kanuni inasema inatoa mamlaka hayo kwa mwenyekiti, kitu chochote lazima kiwe na mipaka.
“Kwa kuwa kitu kinachojadiliwa pale ni Katiba na si kitu kingine, hiyo nafasi ya kuzungumzia mambo mengine haikuwapo. Siungi mkono na suala kama hilo lazima likemewe.
Alichosema Hamad Rashid
Mbunge huyo wa Wawi (CUF), alisema katika mahojiano yaliyorushwa na Kituo cha Televisheni cha Star TV juzi kuwa Maalim Seif alimshambulia yeye binafsi, kamati yake na Bunge la Katiba.
“Amesema mimi ni dalali wa CCM na kwamba nimepewa fedha ili kuwahonga watu ili waje kwenye kikao hiki (Bunge). Hili nimemwachia mwanasheria wangu,” Mohamed alimnukuu Maalim Seif na kuongeza:
Chanzo Mwananchi
No comments:
Post a Comment