Social Icons

Sunday, 5 October 2014

Yaliyojitokeza wakati wa kuuangusha utawala wa Gaddafi Libya

Majeshi ya Marekani yaliyoko nchini Libya yameanza kutumia mabomu na makombora yenye urani dhidi ya wananchi wa nchi hiyo. Taarifa kutoka Tripoli zinaeleza kuwa, majeshi ya Marekani katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, yametumia makumi ya mabomu na makombora ya Cruise yenye mada za urani kwenye miji kadhaa ya nchi hiyo. Taarifa zinasema kuwa, utumiwaji wa makombora na mabomu hayo yenye urani, utasababisha kujitokeza maradhi ya saratani, magonjwa ya ngozi pamoja na athari hiyo mbaya kubakia kwa muda mrefu kwa watu wa maeneo hayo. Maafa hayo yanajitokeza katika hali ambayo, vikosi vya nchi za Magharibi vinavyoongozwa na Marekani nchini Libya vinadai kuwa, viko nchini humo kwa shabaha ya kuwalinda raia wa nchi hiyo. Wakati huohuo, serikali ya Libya imetangaza kuwa, mashambulio ya majeshi ya kigeni nchini humo yamepelekea watu wasiopungua 114 kuuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa.

——————————————-

From bbc/swahili

Eneo la asili la Gaddafi lashambuliwa

Muasi Libya

Uvamizi wa anga unaofanywa na majeshi ya muungano umeshambulia eneo alipozaliwa Kanali Muammar Gaddafi huko Sirte, eneo muhimu linalolengwa na waasi lililopo upande wa magharibi.

Msemaji wa serikali ya Libya alisema raia watatu wa Libya waliuliwa kwenye bandari ya nchi hiyo.

Uvumi ambao haukuthibitishwa kuwa waasi waliudhibiti mji wa Sirte ulisababisha waasi kufyatua risasi kwa minajil ya kushangilia kwenye mji walioukhodhi wa Benghazi.

Waandishi wa kigeni Sirte walisema walisikia milipuko mikubwa kwenye mji huo huku ndege zikipita angani.

Msemaji wa waasi huko Benghazi alisema Sirte sasa ilikuwa mikononi mwa majeshi ya waasi- lakini hakujakuwa na uthibitisho binafsi kutokana na madai hayo, na waandishi wa habari wa kimataifa ndani ya mji huo walisema bado unadhibitiwa na serikali.

Wakati huo huo, Qatar ni taifa la kwanza la kiarabu kutambua uongozi wa waasi- Baraza la Taifa la Mpito- kama wawakilishi rasmi wa watu wa Libya

——————————————————

From Dw radio

Vikosi vya jeshi la muungano vyaishambulia Libya bila huruma

Vikosi vya jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani vimeongeza shinikizo kwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi kutokana na mfululizo wa mashambulio ya anga bila huruma.

Miripuko ilisikika kwenye mji mkuu wa Tripoli mapema leo na walioshuhudia wamesema kuwa eneo la rada ya kijeshi lilikuwa likiwaka moto.

Ndege za kivita za jeshi la muungano zilifanya mashambulio 150 zaidi dhidi ya vikosi vya jeshi la Kanali Gaddafi, ukiwemo mji wa mashariki wa Adjabiya. Mashambulio hayo yamewawezesha waasi kuudhibiti tena mji huo.Baadhi ya ndege za kijeshi zinazoshiriki katika operesheni nchini LibyaBildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift:  Baadhi ya ndege za kijeshi zinazoshiriki katika operesheni nchini Libya

Kuna taarifa kwamba mtoto wa kiume wa Kanali Gaddafi, Saif al-Islam ameondoka kwa siri nchini humo ikiwa ni katika kuchukua hatua za kidiplomasia kwa ajili ya kuzuia mapigano zaidi na kuidhibiti hali iliyopo sasa ya kisiasa na kijeshi ambayo inazidi kuwa mbaya.

Marekani na Jumuiya ya Kujihami ya NATO zinafikiria kuwapatia silaha wapinzani, zikisema kuwa azimio la Umoja wa Mataifa linaruhusu uwezekano huo.

NATO hatimaye pia imekubali kuchukua jukumu la kuongoza operesheni za kutekeleza marufuku ya ndege kuruka katika anga ya Libya. Operesheni hiyo itakuwa chini ya Jenerali Charles Bouchard kutoka Canada

————————————————

From dw radio

Waasi Libya washindwa kuuteka Sirte

Wanajeshi watiifu kwa kiongozi wa Libya Muammar Gadadafi wamelizuwia jaribio la waasi kuingia mjini Sirte anakotoka kiongozi huyo. Mji huo ulishambuliwa jana usiku na ndege za kivita za majeshi ya muungano baada ya Jumuiya ya kujihami ya  NATO kuchukua uongozi wa operesheni za kivita nchini Libya. Mwaandishi habari wa Shirika la AFP alisema waasi ambao kwa siku mbili zilizopita wamekua wakisonga mbele upande wa magharibi walishambuliwa kwa makombora na wanajeshi wa Gaddafi, katika barabara itokayo Bin Jawad kuelekea Nofilia. Waasi waliuteka mji wa Bin Jawad ulioko kilomita 140 mashariki mwa Sirte jana, baada ya kuuteka mji wa mafuta wa Ras Lanuf,  wakati wakisonga mbele kwa msaada wa ndege za kivita za majeshi ya  muungano  zinazoyashambulia majeshi ya Kanali Gaddafi kutoka angani

———————————————

BBC/SWAHILI

Wapiganaji wanaikomboa Ajdabya

Wapiganaji wa LibyaWapiganaji wa Libya 

Wapiganaji wa mashariki mwa Libya, wameuteka tena mji muhimu wa Ajdabiya, kutoka kwa majeshi ya Muammar Gaddafi.
Ndiyo mji wa kwanza kukombolewa na wapiganaji, tangu kuanza shughuli za kuzuwia ndege za serikali kuruka katika anga ya Libya.

Waziri mmoja wa serikali, Khaled Kaim, alisema jeshi la serikali liliondoka Ajdabiya, baada ya kupigwa kwa mabomu na ndege za jeshi la kimataifa.

WaasiWapiganaji wa Libya 

Mwandishi wa BBC mjini humo, anasema wapiganaji walicheza mabara-barani, kusherehekea.

Piya anasema, aliona vifaru kama 20 vya serikali, magari ya deraya na mizinga, ambayo iliharibiwa au kuachwa.

Na mashambulio ya ndege, yalitikisa kitongoje kimoja cha mji mkuu, Tripoli, leo alfajiri.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema, mtambo wa jeshi wa radar uliwaka moto

————————————

NA DW RADIO

Vikosi vya jeshi la muungano vyaishambulia Libya bila huruma

Vikosi vya jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani vimeongeza shinikizo kwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi kutokana na mfululizo wa mashambulio ya anga bila huruma.

Miripuko ilisikika kwenye mji mkuu wa Tripoli mapema leo na walioshuhudia wamesema kuwa eneo la rada ya kijeshi lilikuwa likiwaka moto.

Ndege za kivita za jeshi la muungano zilifanya mashambulio 150 zaidi dhidi ya vikosi vya jeshi la Kanali Gaddafi, ukiwemo mji wa mashariki wa Adjabiya. Mashambulio hayo yamewawezesha waasi kuudhibiti tena mji huo.Baadhi ya ndege za kijeshi zinazoshiriki katika operesheni nchini LibyaBildunterschrift: Großansicht des  Baadhi ya ndege za kijeshi zinazoshiriki katika operesheni nchini Libya

Kuna taarifa kwamba mtoto wa kiume wa Kanali Gaddafi, Saif al-Islam ameondoka kwa siri nchini humo ikiwa ni katika kuchukua hatua za kidiplomasia kwa ajili ya kuzuia mapigano zaidi na kuidhibiti hali iliyopo sasa ya kisiasa na kijeshi ambayo inazidi kuwa mbaya.

Marekani na Jumuiya ya Kujihami ya NATO zinafikiria kuwapatia silaha wapinzani, zikisema kuwa azimio la Umoja wa Mataifa linaruhusu uwezekano huo.

NATO hatimaye pia imekubali kuchukua jukumu la kuongoza operesheni za kutekeleza marufuku ya ndege kuruka katika anga ya Libya. Operesheni hiyo itakuwa chini ya Jenerali Charles Bouchard kutoka Canada.

——————————

RADIO IRAN/SWAHILI

Walibya wasiopungua 114 wauawa katika mashambulio ya anga ya Wamagharibi Imeelezwa kuwa, raia wasiopungua 114 wameuawa nchini Libya na wengine karibu 500 kujeruhiwa kufuatia mashambulio ya anga ya Wamagharibi dhidi ya Libya yanayoongozwa na Marekani. Khalid Omar, Waziri wa Afya wa Libya amesema katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Tripoli kwamba, watu wasiopungua 114 wameuawa nchini humo kuanzia tarehe 20 hadi 23 za mwezi huu wa Machi. Taarifa ya serikali ya Libya imebainisha kuwa, idadi kubwa ya raia hao wameuawa katika mji mkuu Tripoli ambayo ni ngome ya dikteta wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi. Mji wa Misrata ambao una jumla ya wakazi nusu milioni unashikilia nafasi ya pili baada ya Tripoli kwa kuwa na wahanga wengi wa mashambulio ya anga ya nchi za Magharibi.

————————————-

radio dw

Afrika na Gaddafi: “Hatuwezi kuwa wizi wa fadhila”

Huku mataifa ya Ulaya yakiizuia akaunti za fedha za kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, kiongozi huyo ana hazina nyengine ya mamilioni kwenye nchi kadhaa za Afrika; na ambayo haionekani kuwa itakauka kwa karibu.

Kwa miongo kadhaa sasa, kiongozi huyo amekuwa akiwekeza katika miradi mikubwa mikubwa ya ujenzi wa miundombinu, huduma na usafiri katika bara hilo. Kampuni ya taifa ya mafuta ya Libya, peke yake, ina mtandao wa matangi 2000 ya mafuta katika nchi 20 za Afrika.

Ni rahisi kwenye nchi za Afrika kukuta barabara inaitwa mtaa wa Gaddafi, au msikiti wa Gaddafi, au jengo la Gaddafi, maana nchi nyingi za bara hilo zinamtukuza kiongozi huyu.

Na hili, hapana shaka,  linaonesha namna ambavyo Gaddafi amekuwa na ushawishi katika sehemu kadhaa za bara hilo.

Kwenye Benki ya Maendeleo ya Afrika, Libya peke yake ina mtaji wa euro milioni 260, jambo ambalo mwakilishi wa benki hiyo kwa kanda ya Afrika ya Kaskazini, Emanuele Santi, anaona kuwa halitabadilika.

In this photo taken Monday, Nov. 3, 2008, Libya's leader Moammar Gadhafi attends a wreath laying ceremony in the Belarus capital Minsk. Gadhafi's security forces unleashed the most deadly crackdown of any Arab country against the wave of protests sweeping the region, with reports Monday Feb. 22, 2011 that demonstrators were being fired at from helicopters and warplanes. After seven days of protests and deadly clashes in Libya's eastern cities, the eruption of turmoil in the capital, Tripoli, sharply escalated the challenge to Gadhafi. (AP Photo/Sergei Grits)Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift:  In this photo taken Monday, Nov. 3, 2008, Libya’s leader Moammar Gadhafi attends a wreath laying ceremony in the Belarus capital Minsk. Gadhafi’s security forces unleashed the most deadly crackdown of any Arab country against the wave of protests sweeping the region, with reports Monday Feb. 22, 2011 that demonstrators were being fired at from helicopters and warplanes. After seven days of protests and deadly clashes in Libya’s eastern cities, the eruption of turmoil in the capital, Tripoli, sharply escalated the challenge to Gadhafi. (AP Photo/Sergei Grits) “Libya ni mshirika muhimu kwenye benki yetu. Sifikirii kuwa Gaddasi atazitoa fedha zake, maana daima amekuwa akionesha mshikamano na bara la Afrika na kwa hivyo hawezi kubadilika. Na sisi pia hatukusudii kuzizuia fedha zake.”

Kwa ujumla, thamani ya vitega uchumi mbalimbali vya Libya kwenye nchi mbalimbali za Afrika inafikia euro bilioni sita. Miradi na makampuni kadhaa makubwa yanafaidika na mkopo wa kifedha kutoka Libya.

Mfano ni kampuni ya simu za mkononi ya Uganda Telecom, ambayo mbili ya tatu ya hisa zake inamilikiwa na Mamlaka ya Uwekezaji ya Libya, ambayo thamani yake ni karibuni euro milioni 10.

Na kama hilo halitoshi, katika miaka ya hivi karibuni, Gaddafi, ambaye mwenyewe aliwahi kujiita mfalme wa wafalme, aliahidi mabilioni zaidi ya euro kuwekezwa kwenye uchumi wa bara la Afrika.

#b#Miongoni mwa wanufaikaji wakubwa wa uwekezaji huu ni nchi ya Burkina Faso iliyoko magharibi mwa Afrika. Hapa Gaddafi amejenga miundombinu na hospitali kubwa kabisa.

Tangu zamani, serikali ya nchi hii imekuwa na mahusiano makubwa sana Gaddafi, jambo ambalo hata kiongozi wa Muungano wa Upinzani, Hama Arba Diallo, hana sauti ya kupingana nalo sana.

“Kuna uwekezaji mkubwa kama ule wa chuo kikuu, ambao serikali yetu peke yake isingeliweza kuumudu, lakini Muammar Gaddafi ametusaidia. Na hajawekeza hapa Burkina Faso tu, bali pia kwenye nchi nyengine nyingi za Afrika, na kwa hilo tunamshukuru sana. Kinachotokea Libya hivi sasa, kinatusikitisha sote. Lakini hakuna nchi ya Afrika ambayo Gaddafi ameisaidia kifedha, ambayo leo itakuwa mwizi wa fadhila kwake.”

Kwa umoja na utegemezi huu wa kiuchumi uliopo, si jambo la ajabu kwamba nchi za Kiafrika hazinyanyui sauti sana kupinga yale yanayofanywa na Gaddafi dhidi ya raia wake.

Wataalamu wa mambo ya siasa za Afrika, wanaona kuwa isitegemewe kwa siku za karibuni, viongozi wa Afrika watamuwacha mkono Gaddafi.

“Gaddafi amejijenga sana Afrika, kupitia anavyozungumzia uzalendo wa Kiafrika, kupitia ujenzi wa misikiti Afrika nzima. Na kusema kwamba hili linaweza kubadilika kwa haraka, bado ni suala la kuangaliwa.” Anasema Helmut Asche, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mambo ya Afrika ya mjini Leipzig

——————————————————–

radio dw

Mashambulizi yaanga yameingia siku ya 6 nchini Libya

Mashambulizi ya anga yanayofanywa na Majeshi ya Muungano nchini Libya, eo hii yameingia siku ya 6, huku maafisa wa Uingereza wakisema wamefanikiwa kuuvuruga kabisa mfumo wa jeshi la anga la nchi hiyo.

Mashambulizi ya hivi karibuni yamefanyika alfajiri ya leo, ambapo milio ya makombora imekuwa ikifyatuliwa kwa mfululizo.

Operesheni hiyo inatekelezwa, wakati ambapo wajumbe kutoka nchi 28 za jumuiya ya Kujihami ya NATO, wakiendelea na mkutano wao nchini Ubelgiji, wenye lengo la kujadili namna jumuiya hiyo itakavyoshiriki katika operesheni hiyo.

Kaimu kamanda wa Kikosi cha Anga cha Uingereza, Greg Bagwell amesema, NATO hivi sasa wamekwisha sikia taarifa za mafanikio ya operesheni inayoendelea.

Afisa huyo ambae ni miongoni mwa waratibu wa operesheni hiyo kwa upande wa Uingereza, amesema kikosi cha anga cha kiongozi wa Libya, kanali Muammar Gaddafi, hakipo katika mfumo wa kivita.

Ndege ya kivita ikijiandaa kushambulia Libya

Ndege ya kivita ikijiandaa kushambulia LibyaMarekani imeanza kutabiri kwamba kuendelea kwa shinikizo lililipo sasa kunaweza kumuondoa madarakani Kanali Gaddafi ambaye amekuwa madarakani kwa miongo minne sasa.

Nae Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kuiwekea vikwazo Libya,kauli aliyoitoa ya kabla ya kufanyika mkutano huo mjini Brussels.

Katika tukio lingine walioshuhudia wamesema wameona miripuko kadhaa usiku wa kuamkia leo katika kambi moja ya jeshi iliyopo karibu na eneo la makazi ya watu ya Tajura umbali wa kilometa 32 mashariki mwa mji mkuu, Tripoli.

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari nchini Libya, JANA, mashambulizi hayo ya vikosi vya anga vya muungano yameua idadi kubwa ya watu katika eneo hilo.

Taarifa za shirika hilo limesema ndege za kivita zilifyatua makombora matatu yote yenye athari kwa wakaazi, lakini la mwisho kati ya hayo, lililenga watu waliokuwa wakijaribu kuwaokoa wenzao waliofunikwa na vifusi vya majengo.

Tajura ni ngome muhimu ya kijeshi nchini Libya, na ni eneo la kwanza kushambuliwa na vikosi vya muungano Jumamosi iliyopita, baada ya Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kuzuia ndege kuruka katika anga ya nchi hiyo.

Pamoja na tamati ya opereshini ya Libya kutofahamika, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Robert Gates alipokuwa Misri hivi karibuni alisema kuongezwa kwa shinikizo zaidi dhidi ya Gaddafi kunaweza kuwafanya hata watu wake wa karibu wamgeuke.

Alisema kuna mambo kadhaa ambayo yatajitokeza ingawa siyo rahisi kwa sasa kuyatabiri.

Hata hivyo taarifa kutoka jeshi la Marekani zinasema hivi sasa wapo katika operesheni ya kudhibiti vikosi vya ardhini vya Gaddafi kwa kuwa vimekuwa tishio katika miji inayokaliwa na waasi.

Nguvu mpya ya majeshi ya muungano nazo zimeingia vitani, ambapo usiku wa kuamkia leo ndege ya kivita ya Canada imefanya mashambulizi katika mji unaoshikiliwa na waasi wa Misrata.

Mji huo ambao ni wa tatu kwa ukubwa nchini Libya upo umbali wa kilometa 214 mashariki mwa Tripoli

——————————————–

radio dw

Nani kuongoza operesheni za kijeshi Libya?

Mataifa ya Magharibi yanayoshiriki katika kikosi cha Umoja wa Mataifa kutekeleza marufuku ya ndege kuruka kwenye anga ya Libya, yanajadiliana jinsi ya kuihusisha Jumuiya ya Kujihami ya NATO katika juhudi za kijeshi.

Lakini bado haijajulikana wazi jinsi muungano huo utakavyohusishwa na nani atakayeongoza operesheni hizo za kijeshi. Rais Barack Obama wa Marekani ana matumaini ya kukabidhi kikosi cha Marekani katika kusimamia operesheni hizo hivi karibuni.

Jana jioni, Rais Obama alisema ana imani kwamba makubaliano yatapatikana katika siku chache zijazo. Baadhi ya nchi ikiwemo Ufaransa na Uturuki zina wasiwasi kuwa kikosi kinachoongozwa na NATO huenda kikaonekana kina sifa mbaya katika ulimwengu wa nchi za Kiarabu. Hata hivyo, muungano huo umekubali kutekeleza vikwazo vya silaha nchini Libya.

Viongozi wa ngazi ya juu wa Ujerumani, akiwemo Kansela Angela Merkel

Viongozi wa ngazi ya juu wa Ujerumani, akiwemo Kansela Angela Merkel Wakati huo huo, Ujerumani imetangaza kujiondoa katika operesheni za Jumuiya ya Kujihami ya NATO katika eneo la Mediterranean kutokana na jeshi la muungano kushiriki katika mzozo wa Libya. Msemaji wa wizara ya ulinzi amesema manowari mbili na meli nyingine mbili zitarejea katika kikosi cha Ujerumani.

Manowari hizo za Lübeck na Hamburg ni sehemu ya operesheni za juhudi za NATO katika kupambana na ugaidi kwenye eneo hilo. Kiasi wanajeshi 70 wa Ujerumani wanaoshiriki katika operesheni za NATO pia wataondolewa.

——————————————–

radio dw

Jeshi la anga la Libya lazidi kurudi nyuma

Kamanda wa juu wa Uingereza amesema kuwa vikosi vya jeshi la muungano vimekiangamiza kikosi cha jeshi la anga la Libya. Jemadari Greg Bagwell amesema ndege za vikosi hivyo sasa zinaruka kwa uhuru kuzunguka Libya.

Mashambulizi yanawalazimisha wanajeshi watiifu kwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi kurudi nyuma, ingawa bado wanashambulia kambi za waasi katika miji ya Misrata ulioko magharibi na Adjabiya ulioko mashariki.

Kituo cha televisheni cha Al-Jazeera kimetangaza kuwa kikosi hicho cha muungano wa kimataifa kinaendelea na mashambulizi yake dhidi ya vikosi vya Kanali Gaddafi kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli.Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron

Wakati huo huo, Uingereza imetangaza kuandaa mkutano wa kimataifa utakaojadili maendeleo ya kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Libya. Mkutano huo utakaofanyika Jumanne ijayo mjini London, utalenga zaidi kuhusu maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na mahitaji ya kibinaadamu ya watu wa Libya.

Bado haijafahamika jukumu ambalo Jumuiya ya Kujihami ya NATO italitimiza katika kutekeleza operesheni ya kuzuia ndege kuruka kwenye anga ya Libya, ambayo kwa sasa inaongozwa na Marekani. Rais Barack Obama wa Marekani anataka kukabidhi jukumu hilo haraka iwezekanavyo. Wiki iliyopita, Ujerumani haikupiga kura katika baraza hilo la usalama.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Thomas de Maiziere

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Thomas de MaiziereAidha, juzi Jumanne Ujerumani ilijiondoa katika operesheni za NATO kwenye Bahari ya Meditteranean kutokana na jumuiya hiyo kujiingiza katika mzozo wa Libya na kurejesha udhibiti wa meli nne za kijeshi chini yake. Lakini katika hatua ya kukisaidia kikosi cha muungano nchini Libya, baraza la mawaziri la Ujerumani jana lilipitisha mipango ya kupeleka wanajeshi wa kurusha ndege za uchunguzi za NATO nchini Afghanistan.

————————————

From bbc/swahili

Gaddafi ashambulia miji muhimu ya waasi

Libya 

Mapigano baina ya waasi na majeshi yanayomtii kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi yamekuwa yakiendelea katika miji muhimu baada ya mashambulio ya anga yanayoendelea kwa mfululizo wa siku ya tano sasa yanayofanywa na majeshi ya kimataifa.

Milio mingi ya milipuko ilisikika usiku kwenye mji mkuu wa Tripoli.

Katika mji unaoshikiliwa na waasi Misrata, mashariki mwa Tripoli, vifaru vya serikali vimekuwa vikishambulia eneo karibu na hospitali.

Kumekuwa pia na ripoti juu ya mapigano makali baina ya waasi na majeshi yanayomwuunga mkono Gaddafi mjini Ajdabiya.

Wakazi waliokimbia mji huo wameelezea kuwepo kwa makombora, milio ya risasi na nyumba kuwashwa moto.

Mashambulio Ya Anga

Kulingana na vyanzo vya jeshi vya Libya na vyombo vya habari vimesema, kuna ripoti za kuwepo mashambulio ya anga yaliyofanywa na nchi za magharibi kwenye mji wa Tajura.

Na jeshi la Ufaransa limesema mashambulio ya anga yaliyofanywa na Ufaransa yamelenga kituo cha anga cha Libya ndani ya nchi hiyo nyakati za usiku.

Siku ya Alhamis, ndege za kijeshi za nchi za magharibi zimeripotiwa kushambulia mji wa Sebha kusini mwa Libya, kulingana na wakazi na taarifa kutoka vyombo vya habari.

Sebha, uliopo kilomita 750 kusini mwa Tripoli, ni eneo lililodhibitiwa vilivyo na ni kitovu cha kijeshi cha Kanali Gaddafi.

Pia kumeripotiwa kuwepo kwa mlipuko nyakati za usiku kwenye kituo cha kijeshi eneo la Tajura mashariki mwa Tripoli

———————————————-

FROM BBC/SWAHILI

Mugabe, Zuma walaani mashambulio Libya

Libya 

Viongozi kadhaa kutoka nchi za Afrika, ikiwemo Uganda, Afrika Kusini na Zimbabwe, wamelaani mashambulio ya angani nchini Libya.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameandika makala ndefu kwenye gazeti akizishutumu nchi za magharibi kwa kuwa ndumilakiwili.

Alikuwa ni mmoja miongoni mwa viongozi watano wa Afrika waliopewa jukumu la kutafuta suluhu la mgogoro Libya, ambapo safari ya ujumbe huo mjini Tripoli uliahirishwa baada ya mashambulio kuanza.

Bw Jacob Zuma wa Afrika Kusini naye alikuwepo kwenye jopo la Umoja wa Afrika.

Licha ya Afrika kusini kupiga kura ya azimio la umoja wa mataifa mwaka 1973, iliyoidhinisha hatua za kijeshi kulinda raia, Bw Zuma naye amelaani mashambulio hayo ya anga, akisema ni sehemu ya “sera za mabadiliko ya uongozi.”

Viongozi wa nchi za magharibi walisema mashambulio hayo hayatomlenga kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi lakini wanataka aachie madaraka.

Bw Zuma alitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano haraka iwezekanavyo na “kukataa kuingiliwa na nchi yeyote ya kigeni, hata iwe katika muundo upo”.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, mkosoaji mkuu wa nchi za magharibi, naye amelaani mashambulio hayo ya anga, akisema mgogoro wa Libya ni kuhusu utajiri wake wa mafuta.

Hifikepunye Pohamba, Rais wa Namibia naye amekubaliana na hilo, akiita shambulio hilo ni “kuingilia masuala ya ndani ya Afrika.”

Umoja wa Afrika nao umetoa wito wa kumaliza uvamizi wa kijeshi nchini Libya

—————————————————————————————
FROM DW-WORLD.DE

Tafauti baina ya Waarabu na Magharibi zaanza juu ya Libya

Wakati mataifa ya Magharibi yakiishambulia Libya kutoka angani, inaonekana ya Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu juu tafsiri ya marufuku ya anga inagongana na ile ya hatua za kijeshi ya mataifa ya Magharibi.

Tangu mwanzo ilikuwa wazi, kwamba hatua za kijeshi dhidi ya utawala wa Muammar Gaddafi ni jambo la hatari na kwamba matokeo yake hayafahamiki.

Ukweli huo ndio uliopo hadi sasa. Dikteta huyu wa Libya hajasalimu amri, badala yake anawashajiisha wafuasi wake kupigana vita dhidi ya malengo ya mataifa ya magharibi.

Vikosi vya Muungano wa Kimataifa yameanza hatua zake za kijeshi. Zinaushambulia utawala wa Gaddafi, lakini si kwa vikosi vya ardhini.

Vipi na lini vita vya anga na ardhini vitaletwa pamoja, bado haijulikani, lakini tusifanye kosa kudhani litakuwa jambo rahisi. Hivi vitakuwa vita vya muda mrefu na vitakavyogharimu maisha ya watu wengi.

Ndege ya kijeshi ya Ufaransa ikielekea kushambulia LibyaBildunterschrift: Ndege ya kijeshi ya Ufaransa ikielekea kushambulia LibyaHata hivyo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikuwa limelichukulia jambo hili vyema, pale liliposema kwamba, haliwezi kukubaliana na vitendo vya dikteta kuwaua raia wake mwenyewe.

Lakini jumuiya ya kimataifa ilipaswa kuonesha kuwa, mshikamano wake na umma unaodai uhuru na haki katika ulimwengu wa Kiarabu si maneno matupu.

Kwa hivyo, jumuiya hii ilikuwa imekabiliwa na wakati mgumu sana kimaadili, ndio maana ilikuwa lazima kwake kufanya maamuzi makubwa na magumu pia.

Hatari inakuja pale Marekani, Ufaransa na Uingereza zinapolazimisha ushiriki na uwepo wa moja kwa moja mataifa ya Kiarabu katika operesheni hii.

Ni kweli kuwa ni Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu iliyokuwa kimbelembele kutaka Libya iwekewe marufuku ya anga, na ni kweli kuwa baadhi ya wanachama wa Jumuiya hiyo, kama vile Qatar na Imarat, zimejishirikisha moja kwa moja kijeshi kwenye operesheni hii.

Lakini hili nalo lisichukuliwe kijuujuu tu, maana uendeshaji wa operesheni nzima uko chini ya makamanda wa mataifa ya magharibi, na bado haijulikani ni lini mataifa ya Kiarabu yenyewe na peke yake yanaweza kukabidhiwa dhamana ya kuendesha operesheni hii.

Matokeo ya mashambulizi ya Marekani, nchini LibyaBildunterschrift: Matokeo ya mashambulizi ya Marekani, nchini LibyaNa hapa hasa dipo inapokuja hiyo shaka ya uhalali wa misheni hii ya kijeshi katika eneo hili. Ikilinganishwa na uvamizi wa majeshi ya ushirika nchini Iraq na Afghanistan, misheni hii dhidi ya Libya ilipata uungwaji mkubwa zaidi kutoka ulimwengu wa Kiarabu kuanzia mwanzoni. Watu wengi walionesha mshikamano wao na waasi dhidi ya utawala wa Gaddafi.

Lakini hali hii inaweza kubadilika haraka, baada ya picha za maafa ya kiraia yanayotokana na mashambulizi ya Marekani, kurushwa kwenye televisheni au mtandao wa YouTube.

Japokuwa bado haujaonesha mbadala wa hatua za kuchukuliwa, tayari Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu umeshaanza kupingana na mashambulizi ya majeshi ya Muungano wa Kimataifa, kwa madai kuwa hicho sicho kitu walichokubaliana.

Jambo hili linagonga kengele ya tahadhari, kwamba muda si mrefu kuanzia sasa, zile hasira ambazo Waarabu walizionesha dhidi ya tawala zao, zitageuka na kuelekezwa dhidi ya mataifa ya magharibi. Na kuanzia hapo wataziona tawala zao kuwa ziko sawa—————————————————————————————————-

NA DW-RADIO

Maamuzi ya Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Libya yanatajwa kuwa ni hisabati yenye mambo mengi yasiyofahamika, na kwamba nchi washirika zimeingia kwenye mgogoro zisiojua namna ya kuutoka.

Ndege ya kivita ya Marekani

Kile kinachoitwa “Muungano wa Kimataifa”, chini ya uongozi wa Ufaransa, umeanza harakati zake za kijeshi dhidi ya utawala wa Libya, lakini bila ya shaka ni jambo lenye gharama zake.

Japokuwa pana vituo vichache vya jeshi la anga ambavyo unaweza kuvishambulia nchini Libya, huko hakutamaanisha kwamba nguvu za kijeshi za nchi hiyo zimemalizwa kabisa.

Muungano huu wa kimataifa unaweza kuingia kirahisi, na yumkini ndani ya wiki moja tu, ukawa umeweza kuwasaidia watu wa Benghazi kupata huduma zote muhimu, yakiwemo maji na umeme.

Lakini Muammar Gaddafi anadhibiti asilimia 80 ya Libya, na ana mkono wake juu ya kila rasilimali ya nchi hiyo. Ikiwa Muungano huu hauko tayari kukabiliana na ukweli huu, basi mashambulizi ya angani na udhibiti wa mipakani, hautakuwa chochote zaidi ya ushindi kwa Gaddafi, na sio kinyume chake.

Rais Barack Obama wa Marekani

Rais Barack Obama wa Marekani

Marekani yenyewe bado ipo kwenye njia panda: upande mmoja inataka ijiingize kabisa kabisa, upande mwengine inataka iwe kando kando tu.

Rais Barack Obama ameondoa uwezekano wa kupeleka majeshi ya ardhini au hata kujiingiza kwenye mzozo huu kwa kipindi kirefu, lakini yeye na wenzake wanataka Gaddafi apate funzo.

Ikiwa hivyo ndivyo, basi lengo la kile kinachoitwa hatua za kijeshi dhidi ya utawala wa Gaddafi halifahamiki sawa sawa.

Maana ikiwa lengo lake ni kuwalinda raia tu dhidi ya mashambulizi ya vikosi vya Gaddafi, basi vikosi vya Muungano vina, kwa uchache, muda wa mwezi mmoja, kulifanikisha hilo. Kwa hivyo, Gaddafi anao muda wa kungojea.

Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi

Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi

Lakini ikiwa lengo la hatua hizo ni kuuondosha utawala wa Gaddafi, basi majeshi ya Muungano lazima yafanye mashambulizi makali, tena ndani ya kipindi kifupi dhidi ya vituo vya kijeshi vya Gaddafi.

Bila ya mashambulizi hayo, kuuondoa utawala wa Gaddafi ni jambo lisilowezekana. Na huko kutakuwa ni kujiingiza kamili kamili kijeshi.

Ila ikumbukwe kuwa, hilo halikuwa azimio Namba 1973 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lililoidhinisha marufuku ya anga dhidi ya Gaddafi hapo juzi, na pia haukuwa uamuzi uliotajwa wazi na viongozi wa mataifa makubwa yaliyokutana mjini Paris, Ufaransa, hapo jana (19.03.2011).

Na kwa vita hivi, kuna suali jengine la kujibiwa: Umejua kuvianza, lakini je unajua lini na vipi utavimaliza?

Inatarajiwa kuwa Muungano huu wa Mataifa haujapitikiwa bado na mafunzo ya vita vya Balkan, vya Iraq na kadhia inayoendelea hadi sasa nchini Somalia. Mwisho wa hili la Libya nao, hauonekani kuwa mzuri.

Mtu angeliweza kusema kuwa, ule uamuzi wa mwanzo wa Ujerumani kujiepusha kuingia kwenye mgogoro wa kijeshi na Libya ulikuwa sahihi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle

Huo ulitakiwa uwe mtazamo wa Umoja wa Ulaya pia. sio kuchukuliwa na andasa za siasa za ndani za Nicolas Sarkuzy wa Ufaransa, ambaye anaukimbia mbinyo wa kisiasa ndani ya nchi yake kwa kujibebesha dhima ya kuongoza shinikizo dhidi ya Libya.

Ikiwa Muungano huu wa Mataifa utakuwa na bahati njema, basi utaweza kumdhibiti Gaddafi kijeshi na kisha kuushawishi Umoja wa Mataifa umuwekee vikwazo vya silaha. Lakini ukikumbwa na bahati mbaya, basi ujitayarishe kwa hasira za mkizi kutoka kwa Gaddafi mwenye silaha.

Je Ufaransa na Italia zimejitayarisha kuyakaribisha makombora ya Gaddafi kwene miji ya Neapal au Marseille? Maana anaweza kuwa tayari kuyatuma huko.

Na kwa upande mwengine, ikiwa mashambulizi ya majeshi ya Muungano yataleta maafa makubwa kwa raia, basi si vigumu kwa maoni kwenye nchi za Kiarabu na Kiislamu kubadilika haraka sana, yakazigeukia nchi washirika.

Kwa kila hali, safari ya mkasa na yenye mwisho usiojuilikana ndio imeanza.

————————————————————————————-

NA RADIO IRAN

Marekani yaanza kuvurumisha makombora dhidi ya ngome za dikteta Gaddafi Msemaji wa Komandi ya Kijeshi ya Marekani nchini Libya amesema kuwa, jeshi la nchi hiyo limeanza kufanya shambulizi la kwanza la makombora kwenye maeneo na ngome za vikosi vitiifu kwa dikteta Muammar Gaddafi wa Libya. Luteni James Stockman ameongeza kuwa, makombora hayo yameelekezwa karibu na Tripoli na Sirte. Aidha taarifa nyingine zinasema kuwa, makumi ya mizinga. vifaru na zana nyingine za kivita za vikosi vya Kanali Muammar Gaddafi vimeangamizwa kwenye mashambulizi ya anga yaliyofanywa na majeshi ya nchi za Magharibi huko magharibi mwa Benghazi. Taarifa zinasema kuwa, makumi ya wapiganaji waliokuwa wamevaa sare za kijeshi wameonekana wakiteketea kwa moto kwenye eneo hilo. Kwa upande mwengine, Basmat Izzuddin mwanasiasa mashuhuri nchini Libya amesema kuwa, Gaddafi pamoja na familia yake ya karibu wamejificha, wakihofia mashambulizi ya vikosi vya kigeni. Izzuddin ameongeza kuwa, Gaddafi ambaye alikuwa akiwafananisha wanamapinduzi mithili ya panya wa jangwani, hivi sasa yeye anaonekana kuwa ndiyo panya wa jangwani. Ameongeza kuwa, utawala wa Gaddafi utaanguka haraka iwezekanavyo, kinyume na watu walivyokuwa wakifikiria. Wakati hayo yakijiri, Msemaji wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu amesema kuwa, wananchi wa Libya hawana usalama wa kutosha kufuatia mashambulizi yaliyoanzishwa na majeshi ya nchi za Magharibi dhidi ya utawala dikteta Gaddafi. Ameongeza kuwa, pande mbili zinazopigana lazima zitoe mwanya kwa wafanyakazi wa kutoa misaada wafikishe huduma zao kwa majeruhi wa vita na hatimaye kuwahifadhi kwenye maeneo ya usalama zaidi

————————————————————————————–

NA RADIO IRAN

Wanajeshi 94 wa Gaddafi wauawa katika mji wa Benghazi Wanajeshi 94 wa kiongozi wa Libya wameuawa katika mji wa Benghazi huku mashambulio ya nchi za Magharibi yakiendelea nchini humo. Mamluki wa Kanali Muammar Gaddafi wasiopungua 94 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa kufuatia kushadidi kwa mashambulizi ya nchi za Magharibi dhidi ya vikosi vitiifu kwa Gaddafi dikteta wa Libya huko mashariki mwa mji wa Benghazi. Siku mbili zilizopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio nambari 1973 linapopiga marufuku kupaa kwa ndege katika anga ya Libya. Nchi za Magharibi yaani Marekani, Ufaransa na Uingereza zimeanzisha hujuma zake huko Libya kwa kuvishambulia vikosi vya anga vya Gaddafi baada ya kupasishwa azimio hilo. Ufaransa ambayo ni nchi ya kwanza kuanzisha mashambulio ya anga huko Libya jana alasiri ndiyo iliyoratibu na kuandaa mpango wa kupiga marufuku kupaa ndege katika anga ya Libya. Huku hayo yakiripotiwa, Muammar Gaddafi ameahidi kulipiza kisasi akisema kuwa atawafungulia wananchi maghala ya silaha ili wapambane na vikosi hivyo vya nchi za Magharibi. Amesema Walibya wataendesha vita vya muda mrefu visivyo na mipaka

——————————————————————————————

NA DW RADIO

Mashambulizi dhidi ya Gaddafi yazidishwa

Hujuma za kijeshi za Marekani, Ufaransa na Uingereza dhidi ya vituo muhimu vya kijeshi vya kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, zinaendelea, huku Marekani ikisema hatua ya kwanza imekua ya mafanikio.

Kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Marekani, Michael Mullen, amesema majeshi ya kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, sasa hayasongi tena mbele kuelekea mjini Benghazi.

Mullen amesema kuwa sehemu ya kwanza ya operesheni hiyo ya kimataifa kulazimisha upigaji marufuku urukaji ndege katika anga ya Libya imekua ya mafanikio.

Kwa upande mwengine, mapema leo (20.03.2011), Shirika la Utangazaji la CBS News liliripoti kwamba ndege tatu za kivita za  Marekani aina ya B-2 zilidondosha mabomu 40 katika uwanja  mkuu wa ndege za jeshi la anga la Libya, katika jaribio la kuziharibu ndege zake za kivita.

Taarifa nyengine za jeshi la Marekani zinasema kwamba, magari kadhaa ya kijeshi ya Gaddafi yameharibiwa. Kiasi ya ndege 19 za kijeshi za Marekani zilishiriki katika mashambulizi ya pamoja na  Ufaranasa na Uingereza dhidi ya ngome za Gaddafi hivi leo (20.03.2011).

Kituo cha kijeshi cha NATO, nchini Italia

Kituo cha kijeshi cha NATO, nchini Italia

Duru za huduma ya afya mjini Tripoli zinasema idadi ya Walibya waliouawa katika hujuma hizo imepanda kutoka 48 hadi 64 baada ya baadhi ya majeruhi kufariki dunia.

Kwa upande wake, Gaddafi amesema kwamba sasa Walibya wote wamepewa silaha na kwamba wanajiandaa kwa vita virefu alivyoviita “vya kishujaa”.

Katika  hotuba yake iliyotangazwa na vyombo vya habari vya serikali, Gaddafi amesema Walibya watapigania nchi yao na kutetea utu na heshima yao, akizitaja nchi za magharibi kuwa ni wahalifu.

Kwa upande wao, waasi wameonya kwamba  majeshi ya Gaddafi yanaweza kutumia silaha za kemikali dhidi ya wakaazi wa  mji wa Benghazi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido WesterwelleMjini Berlin, Waziri wa Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle ameyapuuza madai kwamba Ujerumani inatengwa kimataifa kwa kukataa kujiunga na washirika wake wa Shirika la Kujihami la Magharibi (NATO) kuihujumu Libya.

Akiulizwa ni nchi gani  za Umoja wa Ulaya zinakubaliana na uamuzi wa Ujerumani, Westerwelle alisema ni Poland. Uamuzi wa serikali ya Ujerumani kutoshiriki katika hatua ya kijeshi nchini Libya umezusha shutuma kali hapa nchini.

Gazeti moja liliilaumu serikali kwa kile ilichokiita “kuwa upande wa madikteta kuliko washirika wake muhimu wa NATO”.

Westerwelle amesema Ujerumani ina wanajeshi 7,000 katika harakati za kusimamia amani nchi za nje, wakiwemo 5,000 nchini Afghanistan. Kwa hivyo inatimiza wajibu wake kimataifa.

#b#Wakati huo huo, Urusi imetangaza itawahamisha raia wake na wafanyakazi wa ubalozi wake mjini Tripoli. Zoezi hilo litafanyika kwa kutumia magari kupitia nchi jirani ya Tunisia.

Hapo jana (19.03.2011), Urusi ilisema inasikitishwa kuona hatua ya kujiingiza nchini Libya imepitishwa bila kipimo. Pia vyombo vya habari nchini Urusi vimeinukuu duru moja ya Ikulu ya nchi hiyo ikisema kwamba, balozi wake mjini Tripoli amefukuzwa kazi,  bila ya kueleza sababu hasa ya hatua hiyo.

Urusi  na China, ambazo sawa na Marekani, Ufaransa na Uingereza zina kura ya turufu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zilijiunga na Ujerumani, India na Brazil, kujizuwia kupiga kura juu ya azimio lililopitishwa na Baraza hilo kufungua njia ya kuchukuliwa hatua za kijeshi dhidi ya Gaddafi.

—————————————————————————————-

NA RADIO IRAN

Iran yapinga hujuma inayofanywa na Magharibi dhidi ya Libya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali hujuma ya kijeshi inayofanywa na vikosi vya Magharibi dhidi ya Libya. Ramin Mehmanparast, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran kamwe haitachoka kuwaunga mkono wananchi wanaotaka mabadiliko na kutetea haki zao katika nchi yoyote ile. Mehmanparast amewataka wananchi wa Libya kuwa macho na kutoruhusu mataifa ya kigeni kuingilia siasa zake na kutatiza mambo ya ndani ya nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo operesheni hiyo ya kijeshi ya nchi za Magharibi dhidi ya Libya imepingwa na Umoja wa Afrika, Russia na China. AU imesema hujuma hiyo ya nchi za Magharibi dhidi ya Libya inapaswa kusitishwa mara moja na kuutaka utawala wa Kanali Gaddafi kuhakikisha kuwa misaada ya kibinaadamu inawafikia wahitaji. Umoja wa Afrika pia umesema kuna haja ya kufanyika marekebisho ya kisiasa nchini Libya ili kusitisha mgogoro uliojitokeza.

———————————————————————————————

Wafuasi wa Gaddafi kuandamana kwa amani

Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, amewatolea wito wafuasi wake kufanya maandamano ya amani katika mji unaodhibitiwa na waasi wa Benghazi. Duru zinaeleza kuwa jengo moja katika uwanja wake limeshambuliwa na kombora wakati mipango hiyo ikiendelea.Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, Kanali Gaddafi alikutana na kamati maalum ya maandalizi ili kuyapanga maandamano hayo.

Taarifa za kituo cha televisheni cha Al Jazeera zinaeleza kuwa ndege za kivita za Ufaransa zimevishambulia vifaru vingi vya vikosi vya serikali vilivyokuwa karibu na mji wa Benghazi. Maandamano hayo ya amani yatawaleta pamoja raia wa kawaida wasiokuwa na silaha pamoja na wabunge watakaobeba vitagaa vya zeituni. Hata hivyo, watasindikizwa na kundi la raia watakaojihami kwa sababu wapinzani wa serikali katika eneo hilo wana silaha.

Yote hayo yanatokea baada ya vikosi vya kigeni vya shirikia kuanzisha mwishoni mwa wiki operesheni ya Odyssey New Dawn ya kuwalinda raia, kadhalika kushinikiza marufuku ya ndege kuruka kwenye anga ya Libya

—————————————————————————————–

Makaazi ya Kanali Gaddafi yashambuliwa

Ndege zake za kijeshi, zimeshambulia makaazi ya Kanali Gaddafi mjini Tripoli na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye jengo moja.

Viongozi wa muugano wa majeshi hayo wanasema jengo lililoharibiwa lilikuwa linatumika kuamrisha majeshi ya Libya yanayopigana na waasi.

Waandishi wa habari wametembezwa kwenye eneo hilo lakini hakuna taarifa ikiwa maafa yalitokea baada ya shambulizi hilo.

Naibu mkuu wa jeshi la wanamaji wa marekani Bill Gortney anasema mashubulizi hayo hayaja mlenga kanali Gaddafi.

vifaru vya serikali vinateketea

Televisheni ya Libya imeonesha maiti na magari ya kijeshi yaliyoteketea kwenye barabara ya kuelekea mji wa Benghazi, shina la wapinzani wa serikali

Msemaji wa serikali ameeleza kuwa watu 64 wameuwawa katika mashambulio yaliyofanywa na mataifa ya magharibi, lakini hakuna njia ya kuthibitisha taarifa hiyo.

Awali afisa mkuu wa jeshi la Marekani, , Mike Mullen, alisema ndege kutoka Qatar zinapelekwa huko, kuwa tayari kushiriki katika operesheni dhidi ya Libya, na nchi nyengine piya zimetoa ahadi kusaidia.

Adimeri Mullen alieleza kuwa agizo la Umoja wa Mataifa, la kuzuwia ndege za serikali kuruka katika anga ya Libya, sasa limetekelezwa, na majeshi ya Kanali Gaddafi, katika mji wa Benghazi, unaodhibitiwa na wapinzani, sasa hayawezi kusonga mbele.

Alisema hakuona taarifa, kuwa raia wameuwawa.

mpinzani na bunduki yake karibu na Benghazimpinzani na bunduki yake karibu na Benghazi 

Urusi imetoa wito kwa Uingereza, Ufaransa na Marekani, ziache kushambulia maeneo yasiyokuwa ya kijeshi, na kwamba raia wameshambuliwa.

Mkuu wa Jumuiya ya Kiarabu, Amr Moussa, amesema mashambulio yamekwenda mbali, kushinda lile lengo la kulinda tu anga ya Libya, ambavyo ndivo jumuiya yake ilivotaka

No comments:

 
 
Blogger Templates