Social Icons

Monday, 26 January 2015

Kinana aweka wazi sifa za atakaeteuliwa kugombea urais


Alisema CCM tayari imejipanga kuhakikisha rushwa inapingwa vita kwa vitendo katika mchakato wa kuwapata wagombea kuanzia kura ya maoni hadi vikao vya mwisho.

Zanzibar. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema, wagombea wa nafasi mbalimbali wasiona mvuto na kukubalika hawatoteuliwa na chama kuwania nafasi yoyote ikiwamo urais katika kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.

Tamko hilo alilitoa juzi alipozungumza na wanachama wa CCM wa Donge, Kilombero na Kitope, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika ziara yake ya kukagua uhai wa chama visiwani hapa.

Kinana alirejea Zanzibar baada ya kwenda Arusha kwenye mkutano wa usuluhishi wa mgogoro wa Sudan ya Kusini.

Alisema siri ya CCM kupoteza majimbo katika Uchaguzi wa Mwaka 2010 yakiwamo majimbo matatu ya Mtoni, Nungwi na Magogoni ni kutokana na makosa yaliyofanywa na viongozi kusimamisha wagombea ambao hawakuwa chaguo la wanachama.

Kinana alisema kwa kuzingatia kasoro hiyo chama hakitokubali kurudia makosa hayo katika mchakato wa kuwapata wagombea wake katika uchaguzi wa mwaka huu.

“Chama kitahakikisha kinapitisha wagombea wenye mvuto, wanaokubalika na wenye upendo kwa wananchi,” alisema Kinana na kuibua shangwe kwa wanachama wake.

Alisema CCM tayari imejipanga kuhakikisha rushwa inapingwa vita kwa vitendo katika mchakato wa kuwapata wagombea kuanzia kura ya maoni hadi vikao vya mwisho.

Aliwataka wanachama wa CCM kuacha kuwakumbatia watu walionyesha nia ya kuwania nafasi hizo kabla ya wakati wakiwamo wagombea wa urais badala yake wasubiri wakati mwafaka.

azima wawe makini na wanasiasa waliopoteza mwelekeo na kuanza kuwayumbisha misingi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuhatarisha Umoja wa kitaifa kwa wananchi wake.

chanzo mwananchi

No comments:

 
 
Blogger Templates