Social Icons

Thursday, 9 April 2015

Askofu ataka viongozi wa dini waache upambe kwa wagombea

Arumeru/Morogoro. Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evengalist, Arumeru – Arusha, Elihudi Isangya amewataka viongozi wa dini nchini, kuviachia vyama vya siasa kuwateua wagombea wao wa urais katika Uchaguzi Mkuu ujao badala ya kuwa wasemaji wa wanasiasa.

Kauli ya Isangya ni mfululizo wa matamko mbalimbali yaliyotolewa na maaskofu na viongozi mbalimbali wa dini wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Pasaka.

Pia, viongozi wa kisiasa akiwamo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiwa mjini Mpanda Januari 9, mwaka huu aliwataka viongozi wa dini kuacha kutumia mimbari kuwa majukwaa ya siasa.

Akizungumza juzi katika Ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Sakila, Askofu Isangya alisema kazi ya viongozi wa dini ibaki kuliombea Taifa amani na utulivu kuelekea uchaguzi huo.

“Viongozi wa dini tuache upambe na tuviachie vyama vya siasa kuteua wagombea ambao wana sifa na wanaokubalika na watu wengi ili wakati ukifika wananchi wachague kiongozi wanayemtaka,” alisema.

Alisema katika siku za karibuni, kumekuwa na baadhi ya viongozi wa dini kugeuza nyumba za ibada majukwaa ya siasa.

“Hii haipendezi. Kazi tuliyonayo viongozi wa dini ni kufanya mahubiri, kutoa neno la Mungu na ikifika wakati tunafanya kazi ya kuliombea Taifa liwe na amani na utulivu, lakini siyo kufanya siasa,” alisema.

Akizungumzia kusitishwa kwa Kura ya Maoni, Askofu Isangya aliipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa hatua hiyo na kusema itatoa fursa wananchi wengi kujiandikisha.

“Tutumie basi fursa hii tujitokeze kujiandikisha ili tuje kupiga kura katika uchaguzi ujao,” alisema. Alisema uamuzi wa NEC umekuwa wa busara kwani kwa hali ilivyokuwa, isingewezekana Watanzania wenye sifa kujiandikisha kupata fursa ya kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa.

Akizungumzia kuahirishwa kwa kura hiyo katika Ibada ya Pasaka iliyofanyika Kanisa la Mtakatifu Patrick, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Telesphor Mkude aliipongeza NEC akisema imefanya jambo jema kusitisha mpango huo baada ya kuona changamoto mbalimbali.

Alisema moja ya jambo katika tamko la maaskofu ni kusitishwa kupiga kura hiyo ya maoni baada ya kuona kuna kasoro mbalimbali ikiwamo katiba kutowafikia wananchi kwa wakati.

Aliwataka wananchi wajitokeze kupiga kura kwa wingi huku wakitambua kuwa kura ya kila mmoja ana nafasi kubwa ya kuiweka nchi katika hali salama na yenye maendeleo pindi.

Chanzo: mwananchi

No comments:

Blogger Templates