
SIKU chache baada ya Jeshi la polisi kupitia IGP Ernest
Mangu kupiga marufuku vikundi vya ulinzi vilivyoanzishwa na vyama vya siasa
hapa nchini, Kiongozi wa mafunzo wa kikundi cha Red Briged (CHADEMA) wilaya ya
Momba (TUNDUMA), mkoani Mbeya, Methius Mwafongo, @ RASTA, amekamatwa akiwa na
vifaa vya Jeshi la ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Taarifa zilizoufikia mtandao huu wa www.kalulunga.blogspot.com tangu
jana jioni, zilisema kuwa, Katibu Mwenezi CCM Mkoa wa Mbeya,
Ndugu, Bashiru Madodi
kiongozi huyo wa Red briged, alikamatwa na vyombo vya dola baada ya kuwepo taarifa za kwenda kutoa mafunzo kwa wafuasi wa chama hicho cha siasa.
Ndugu, Bashiru Madodi
kiongozi huyo wa Red briged, alikamatwa na vyombo vya dola baada ya kuwepo taarifa za kwenda kutoa mafunzo kwa wafuasi wa chama hicho cha siasa.
Mbali na vifaa vya kijeshi ambavyo alikamatwa navyo zikiwemo
sare za Jeshi hilo,
pia alikutwa na mapanga, Manati na mawe yake.
Wakati tunaenda mitamboni, kuna taarifa kuwa, Katibu wa
Itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi,
amekutana na waandishi wa habari mchana wa leo na kuzungumzia tukio hilo na
kuitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina zaidi.
Alipotafutwa kwa njia ya simu, Madodi amekiri kukutana na
waandishi wa habari na kwamba amethibitisha taarifa za kuwepo kwa tukio hilo ambalo linahusisha
mafunzo ya vijana 600 kila wilaya ya mkoa wa Mbeya kwa nia ovu.
“Chadema mara kadhaa wamenukuliwa kuwa nchi hii haitakalika,
haya bila shaka ndiyo mafunzo wanayoyaandaa hivyo naitaka serikali kupitia
vyom,bo vyake vya ulinzi na usalama vifanye uchunguzi wa kina kila mkoa na
kuwachukulia hatua stahiki za kisheria kwa yeyote anayetaka kuharibu nchi”
alisema Madodi.
Aidha alieleza kuwa kuna taarifa chama chake kimezipata pia
kuwa, mafunzo hayo ya vijana wa Chadema, yanalenga kuwatisha wapiga kura kila
Jimbo ili wasiweze kujitokeza kujiandikisha na kupigia kura kura ya maoni
katiba inayopendekezwa vinavyotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Baadhi ya viongozi wa Chadema ambao hawakutaka majina yao
kuandikwa, wamekiri kuwepo kwa mafunzo mbalimbali na kukamatwa kiongozi huyo na
kwamba viongozi wa ngazi za juu wanafanya mpango wa kuwasiliana na vyombo vya
dola ili kufahamu tatizo kubwa la Mwafongo.
Mpaka sasa, kiongozi huyo wa mafunzo wa Chadema (RASTA),
anahojiwa na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mbeya.
Mtandao huu unaendelea kufauatilia na
kesho utazungumza na ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kwa ajili
ya kufahamu taratibu za kumfikisha mahakamani ama ataachiwa mikononi mwa
Polisi.
No comments:
Post a Comment