Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiwasilia katika mkutano wa hadhara wa kampeni,Korogwe vijijini.

MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk.John Magufuli akifafanua jambo kwa msisitizo huku akibainisha kuwa iwapo atachaguliwa kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu, basi Serikali yake itahakikisha inaboresha maslahi ya watumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini kutokana na kutambua mchango wao katika kulinda amani ya nchi yetu.
Dkt Magufuli alisema kuwa anataka kuona watumishi wa jeshi hilo wanakuwa na mishahara mizuri na hiyo itawezesha kufanya kazi ya ulinzi na usalama wa nchi kwa ufanisi zaidi huku akitumia nafasi hiyo kuomba Watanzania kudumisha amani ya nchi kwani ikipotea hakutakuwa na maendeleo ya aina yoyote.
Dk.Magufuli alitoa kauli hiyo leo katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Korogwe, Mkinga na Lushoto ikiwa ni sehemu ya mikutano ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa rais ambapo alisema anatambua kazi nzuri inayofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama na kuongeza kuwa serikali yake itaboresha maslahi ya wanajeshi wa majeshi yote Nchini .
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli wakiwaaga wananchi wa Bumbuli waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini humo jioni ya leo.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Lushoto kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jitegeme.
Lushoto ikiwa imefurika watu tayari kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Togotwe-Mponde wilayani Bumbuli kuwahutubia wananchi na kuwaomba ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Bumbuli Ndugu January Makamba kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Togotwe.
Mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli Ndugu January Makamba akisisitiza jambo kwa Wananchi wake katika jimbo la Bumbuli jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Togotwe.
Wakazi wa Jimbo la Bumbuli wakifuatilia kwa makini mkutano wa Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo.








No comments:
Post a Comment