Social Icons

Tuesday 24 November 2015

Uturuki yaitungua ndege ya kivita ya Urusi

Bofya hapa kwa habari za karibuni zaidi

15:57 Rais wa Urusi Vladimir Putin asema ndege ya kivita ya Urusi mpaka wa Uturuki na Syria imedunguliwa na "washirika wa magaidi." Amekuwa akiongea katika runinga ya serikali ya Urusi ya Rossiya 24.

15:54 Uturuki yadai ramani ya safari za ndege inadhihirisha ndege ya kivita ya Urusi iliingia anga ya Uturuki.

Image copyright

15:07 Kundi moja la waasi Syria limepakia mtandaoni video inayoonyesha mmoja wa marubani wa ndege ya Urusi iliyoangushwa Syria akionekana kuwa bila fahamu, akiwa labda ameumia vibaya au kufariki.

15:05 Shirika la habari la AFP laripoti kuwa Nato imeitisha "mkutano maalum" baada ya kuangushwa kwa ndege ya Urusi.

Mkutano huo umeitisha kufuatia ombi kutoka kwa Uturuki, lengo likiwa kufahamisha wanachama wa Nato kuhusu kuangushwa kwa ndege ya Urusi.

Hii ni mara ya kwanza kwa mwanachama wa Nato kuangusha ndege ya Urusi au uliokuwa Muungano wa Usovieti tangu miaka ya 1950, kwa mujibu wa shiriika la habari la Reuters.

15:00 Msemaji wa Wizara ya Kigeni ya Uingereza ametaja kisa cha kuangushwa kwa ndege ya Urusi kuwa “kibaya sana”. Amesema: “Tunatafuta maelezo zaidi. Ni wazi kwamba kisa hiki ni kibaya sana na haitakuwa busara kuzungumzia hadi tuwe na taarifa sahihi.”

14:44 Bei ya mafuta yaanza kupanda kufuatia habari kwamba ndege ya kivita ya Urusi imedunguliwa karibu na mpaka wa Syria na Uturuki. Kudorora kwa dola kumewapa wawekezaji kichocheo cha kununua mafuta zaidi.

"Kuanguka kwa ndege ya kivita Syria ni ukumbusho kwamba bado kuna hatari kubwa Mashariki ya Kati," amesema mtathmini mkuu wa bidhaa katika benki ya SEB anayeishi Norway Bjarne Schieldrop, akizungumza na Reuters.

14:39 Msemaji wa Rais Vladimir Putin, Bw Dmitry Peskov, ametaja kudunguliwa kwa ndege ya Urusi aina ya Su-24 kuwa "kisa kibaya sana", lakini ni mapema mno kusema mengi.

Image copyrightReuters
Image captionPicha mseto zikionyesha kuanguka kwa ndege ya Urusi

14:35 Afisa mmoja wa habari wa Nato amesema shirika hilo "limewasiliana na maafisa wa Uturuki" lakini kwa sasa hakutatolewa taarifa zozote zaidi.

14:30 Wizara ya ulinzi ya Urusi imethibitisha ndege iliyoangushwa ilikuwa muundo wa Su-24.

Image copyrightReuters
Image captionNdege za Su-24 zimekuwa zikitumiwa na Urusi dhidi ya waasi wanaompinga Rais Bashar al-Assad

14:28: Wanaharakati nchini Syria wamenukuliwa wakisema mmoja wa marubani wa ndege hiyo ya Urusi amekamatwa. Anadaiwa kuzuiliwa katika eneo lenye milima la Utayrah jimbo la Turkmen Mount, kwa mujibu wa Al-Jazeera Arabic TV.

14:20 Ndege za kijeshi za Uturuki zimeripotiwa kudungua ndege ya kijeshi ya Urusi karibu na mpaka wake na Syria.

NdegeImage copyrightANAD OLU
Image captionKituo cha Anad Olu kimetoa picha zinazoonyesha ndege hiyo ikianguka

Hujambo! Karibu kwa habari za moja kwa moja kuhusu ripoti za kuangushwa kwa ndege ya Urusi eneo la Syria.

Chanzo. BBC

No comments:

 
 
Blogger Templates