Social Icons

Tuesday 19 January 2016

Wahariri Mawio waswekwa rumande

Yatosha

Humhprey Shao, DAR ES SALAAM


Jeshi la Polisi nchini limeshindwa kuwaachilia wahariri wa gazeti la Mawio Simon Mkna na Jabir Idrisa na kuwaseka rumande mara baada ya mahojiano yaliyodumu kwa  saa 9 tangu walipojisalimisha majira ya saa 8 na dakika 56 mchana katika kituo cha polisi cha kati jijini Dar es salaam, ambapo mahojian yalimalizika majira ya saa tano usiku.

Mtembezi ambalo liliweza kupiga kambi kituoni hapo kuanzia saa 8 mchana mara baada ya wahariri hao kujisalimisha kituoni hapo hadi majira ya saa nne usiku mara baada ya mahojiano kumaliziKa na kufanikiwa kuzungumza na mmoja wa wamiliki wa gazeti hilo Saed Kubenea ambapo alisema kuwa kitendo cha kushindwa kuachiwa kwa wahariri hao ni hila za wazi zinazo fanywa na watawala wa nchi hii kupitia jeshi la Polisi

Alisema kuwa wameamua kurefusha mahojiano mpaka usiku ili mradi tu watu hawa walale ndani jambo ambalo si ungwana katika nchi ya utawala bora.

Hata hivyo alimaliza kwa kusema kuwa Polisi wamesema hawawezi kutoa dhamana kwa kuwa mkuu wa kitengo cha upelelezi (ZCO) hayupo hivyo wanalazimika kuwalaza watu hao mahabusu.

Kubenea Alitaja kuwa sababu za kuwanyima dhamana wahariri hao haziridhishi kulingana na hali ilivyokuwa kituoni hapo.

Chanzo. Mtembezi

No comments:

 
 
Blogger Templates