Social Icons

Friday, 20 May 2016

Hadithi. KIUMBE WA USIKU. 3



Aliingia moja kwa moja na mteja wake ndani na kufunga mlango, akapandisha kimini chake hadi usawa wa tumbo na kujilaza kitandani akimsikilizia mteja wake naye asaule. Hakutaka kufanya kosa kama la yule mzee wa mwanzo akadai hela yake mapema na kupewa kama walivyokubaliana.


Yule jamaa alionekana mzoefu wa biashara hiyo na alionekana anahamu kweli na hilo lilionekana wazi kwa jinsi mlingoti wake ulivyosimama. Moyoni Joy alifurahia wateja wa aina ya yule kaka kwa sababu hakuwa wa kupoteza muda kwenye kale kamchezo kwa sababu hata haikupita dakika mbili yule jamaa alikuwa tayari amefika kileleni.

Baada ya kumaliza, yule jamaa alisimama na kupandisha suruali yake aliyoishusha wakati wa kale kamchezo kachafu. Wakati wanavaa masikio ya Joy yalikuwa makini akasikia kishindo cha kitu kwenye sakafu ya kile chumba.

Alipotazama aligundua waleti ikiwa chini ya uvungu wa kile kitanda, akasimama na kuibana kwa mguu huku akimsubiri yule mteja wake aondoke .

Alipoondoka, haraka akaichukua ile waleti na kufungua ndani yake. Ama kweli mlango mmoja ukifunga mwingine unafunguka. Ndani ya ile waleti kulikuwa shilingi laki mbili taslimu.

Akazificha kwenye matiti yake na kutoka nje haraka, ili asije kukutana na yule jamaa akiwa ameshtuka kama amepoteza fedha zake. 

Haya ndiyo yalikuwa maisha ya machangudoa wote hapo kijiweni; siku unakosa, siku unapata. siku unadhurumiwa, siku unadhurumu.
  
Alisimama na kuchukua upande wa khanga na mkoba wake kutoka kwenye kilinge cha ‘babu’(mmiliki wa gesti) na kujifunga vizuri, hiyo ikiwa ni kuhitimisha kazi yake aliyoifuata usiku huo ambayo iliisha mapema kweli kwa sababu wenzake ndiyo kwanza walikuwa wakianza kazi.

Alichukua kila kitu chake na kupanda bajaji, haraka akiondoka eneo hilo kuelekea mtaani kwake, maeneo ya Tandale. Hakika zari lilimdondokea kiasi kwamba fedha ambazo angepaswa kuzipata kwa kuzihangaikia kwa siku tatu au nne alizipata kwa usiku mmoja tu.
Akamshukuru Mungu wake, akashuka salama na kwenda moja kwa moja kuugonga mlango wa chumba chake, lakini kulikuwa kimya. Akafungua busati la mlango wake na kupapasa chini akachukua ufunguo na kuingia ndani akawa amewahi kabla ya shoga yake, Batuli ambaye muda wake wa kurudi ni saa 10 za usiku.

Wote wawili walikuwa wamepanga ndani ya nyumba hiyo kwa kuchangia chumba kimoja, ni marafiki wa tangu utotoni na wote wametokea Dodoma na kukimbilia Dar kwa sababu ya ugumu wa maisha, mwenzake kazi zake ilikuwa ni kuuza baa huku yeye akiuza mwili.
Kabla usingizi haujampitia aliamua kupekua tena ile waleti yake ili atazame vitu vingine vilivyosalia mle ndani, akagundua kitambulisho cha yule mwanaume jina lake likiwa ni Joseph Gabriel. kimeandikwa CRDB Azikiwe Branch Manager yaani meneja wa tawi la Azikiwe benki ya CRDB.

Akakagua tena, akagundua business card ambayo ndani yake kulikuwa na namba zake za simu na mawasiliano mengine. Akahakikisha hamna kitu tena. Akaviweka vile vitu juu ya dressin tebo na kulala.
Itaendelea wala usikose

Chanzo. Fredynjeje

No comments:

 
 
Blogger Templates