Social Icons

Friday, 26 August 2016

Haya ndio majibu kwa Mhe. Kitwanga Kuhusu Ndege mpya za Magufuli

Na Rashid Chilumba

Gazeti moja la kila siku limemkariri Kitwanga akikosoa uamuzi wa serikali ya John Magufuli wa kununua Ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q400 kwa lengo la kufufua Shirika la Ndege la Taifa.



#HOJA

Q400 ni Ndege zisizo na Mwendo

#JIBU
Kwanza lazima Kitwanga aelewe kuwa serikali imepanga kununua Ndege tatu kwa mwaka huu wa fedha, mbili ni Q400 (anazoponda) na moja ni C300.

Ndege mbili ndogo za Q400 zinanunuliwa mahsusi kwa ajili ya safari za ndani ni eneo jirani kama visiwa vya Comoro na Moja kwa ajili ya masafa marefu.

Hivyo ili kujua kama Q400 ni Ndege sahihi kwa matumizi yaliyopangwa ni lazima kuzifahamu Ndege zenyewe na kuzifananisha na Ndege nyingine za aina na mtindo wa Q400.

SASA Q400 NI NDEGE YA AINA GANI?

Q400 ni Ndege ya abiria yenye uwezo wa kubeba abiria 70 hadi 84. Q400 ina uwezo wa Kwenda umbali wa nautical miles 1000 Sawa na 1852 Km bila kutua kwa safari moja ikiwa na Tani Saba za Mizigo (Kilogram 7000).

Pia ina uwezo wa Mwendokasi wa hadi 360 knots (maili 414 kwa saa).

Sasa kwa mujibu wa tovuti ya Forbes, Spidi hiyo ya Q400 ni kubwa kwa zaidi ya knots 110 dhidi ya Ndege nyingine za aina yake zinazotumia pangaboi ikiwemo ATR zinazotumiwa na kampuni kama Precision Air ambazo Spidi yake ni Kati 200-250 knots kwa saa.

Sifa za hapo juu za Q400 zinaifanya kuwa na uwezo unaokaribiana wa Upinzani na Ndege aina ya Jets kama Airbus 319 inayotumiwa na Fastjet ambazo Spidi yake ni 400-450 knots pekee. 

Q400 haishindani na Ndege za wajihi wake bali Ndege kubwa kama Airbus 319.

Pia jambo la nyongeza ni kwamba Q400 inatoa unafuu mkubwa katika matumizi ya mafuta na matengenexo ikilinganishwa na jets kama Airbus za Fastjet kwa safari inayofanana.

Hivyo kutumia Q400 kwa safari za ndani ni bora kwa Ufanisi na gharama ndogo mno kuliko aina nyingine yoyote ya Ndege katika soko la dunia.

Na kwa sisi tunafufua shirika letu la Ndege taratibu kwa kuanza na huduma za ndani zilizoboreka, kisha unajenga imani ya shirika katika usalama na uhakika kwa abiria na unafuu wa uendeshaji kabla hujakimbilia kununua Ndege kubwa ambazo ni ghali kuziendesha na kuzihudumia Q400 ni chaguo sahihi kabisa kwa kila sifa.

#HOJA2

Kampuni ya Bombardier ni ndogo na ya mtu binafsi hivyo ni kosa kununua Ndege huko.

#JIBU2

kampuni zote kubwa duniani za Ndege kwa maana ya Boeing, Airbus na Bombardier zilianzishwa Na zinamilikiwa na mabwenyenye wenye fedha, hivyo ni kituko kuwa hatupaswi kununua Ndege Bombardier kwa sababu inamilikiwa na mtu binafsi. 

Na Hoja kuwa Bombardier ni kampuni ndogo ni ya aibu, Bombardier ilianzishwa mwaka 1942 huko Canada Miaka Karibu 20 kabla Airbus moja ya kampuni kubwa duniani za Ndege haijaanzishwa mwaka 1970 (Yaan wakati Bombardier inaanzishwa mwanzilishi wa Airbus pengine alikuwa Ndiyo anachora chora picha za Ndege kwenye makaratasi.

Ukubwa wa kampuni ya Bombardier Sio tu unatibitishwa kwa ukongwe wake bali pia unaweza kuthibitishwa na wingi wa wafanyakazi ambao unalingana na kampuni nyingine kama Airbus.

Bombadieir kitengo cha Ndege pekee kina wafanyakazi 65,698 kwa takwimu za mwaka 2011 wakati Airbus na vitengo vyake vyote ikiwemo na kile cha treni ina jumla ya wafanyakazi 73978.

Linganisha mwenyewe hapo kabla sijaweka kitengo cha treni cha Bombadieir wafanyakazi wake. Sasa ni udogo upi.

#HOJA3

ATCL Ndiyo itakuwa kampuni ya kwanza ya Ndege kutumia Ndege aina ya Q400

#JIBU3
Tangu Q400 izindulewe mwaka 1983 Ndege za aina hiyo zaidi ya 1000 zimeundwa. Takwimu za karibuni zinaonesha kuwa kampuni 43 za Ndege duniani ikiwemo American Airways, shirika la Ndege la taifa la Marekani linatumia q400.

Air Tanzania itakuwa ni mteja wa 44 tena mwenye order ndogo ya Ndege mbili tu. Jazz Air kampuni ya usafiri wa anga ya nchini Canada imetoa odred ya Q400 10 mwaka Jana.

Lakini wakati huo huo kampuni nyingine 29 za Ndege duniani zimetoa oda ya kutengenezewa

Q400 zinazofikia 102 ikiwemo kampuni kubwa ya Ethiopian Airlines na Westjet ya Marekani. 



No comments:

 
 
Blogger Templates