Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amosi Makala
akiwa katika Halmashauri ya Busokelo.
Wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Mkoa aligundua nyumba za watumishi 14 zimekamilika kujengwa lakini hakuna watumishi wanaoishi kwenye nyumba hizo, kutokana na nyumba hizo kukosa umeme na maji.
Mkuu wa Mkoa alitoa agizo kwa TANESCO kupeleka umeme kwenye nyumba hizo ndani ya wiki mbili.
Pia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ameitaka Idara ya maji na mamlaka ya maji Mkoa wa Mbeya kuweka kambi Busokelo na kuhakikisha nyumba hizo zinapata maji haraka iwezekanavyo.
Mhe. Amosi Makala pia alikutana na wananchi wanaopinga ujenzi wa barabara ya Lupaso kwenda Bujesi kwa kiwango cha lami, kutokana na madai ya kutolipwa fidia yao inayokadiliwa kufikia shilingi milioni 479.
Mkuu wa mkoa aliwaomba wananchi waruhusu ujenzi wa barabara hiyo kuendelea na fedha ya fidia wataipata baada ya muda mfupi ujao kwani suala hilo yeye mwenyewe analishughulikia ili wananchi hao wapate fidia yao.
Barabara ya Lupaso kwenda Bujesi ilikuwa ikamilike toka mwezi Aprili 2015, lakini imeshindwa kukamilika kutokana na mgogoro wa fidia kwa wananchi, barabara hiyo yenye urefu wa Kilomita 10 sasa inategemewa kukamilika mwezi Machi 2017.
Imetolewa na Bashiru Madodi.
No comments:
Post a Comment