Social Icons

Thursday, 1 September 2016

Kupatwa kwa jua, hali ilivyokuwa Tukuyu tarehe 1, Septemba, 2016

Na Bashiru madodi.

Tarehe 1, Septemba, 2016, ni siku ambayo jua lilipatwa na mwezi, tukio hilo lilitokea karibu sehemu kubwa ya dunia. Sehemu ambayo kupatwa kwa jua kulionekana kwa zaidi ya asilimia 90, ilikuwa ni eneo la mji wa Rujewa katika wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya.

Kwa Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya, Mjini Tukuyu ilipofika saa 5:00 asubuhi jua lilikuwa limepatwa kwa zaidi ya Robo tatu, na hali ya hewa ilikuwa ni kama wakati wa jua linapotaka kuzama jioni. Pia kulikuwa na hali ya ubaridi mkali uliojitokeza ghafla, hali hiyo iliwalazimisha wakazi wa mji wa Tukuyu kwenda kutafuta makoti na kuyavaa.
 Jua lilipokuwa linaendelea kupatwa majira ya saa 5:15 asubuhi Mjini Tukuyu

Ilipofika saa 5:45 asubuhi hali ya hewa ikawa haijulikani Mjini Tukuyu kwani ilikuwa baridi kali na kutokujua kama ni asubuhi, jioni au mchana na baadhi ya watu wakaanza kuingiwa na hofu kutokana na walichokuwa wanakiona. Kutokana na kuwa na baridi kali vichwa vikaanza kuwauma baadhi ya watu na hapo ndipo hofu zilipozidi kuongezeka kutoka miongoni mwa watu, pia macho yakawa hayaoni vizuri.
Jua lilivyokuwa linaonekana saa 5:50 asubuhi, ni kama mwezi ulioandama siku
tatu zilizopita.

Ilipofika saa 5:50, jua lilikuwa limepatwa kwa kiwango cha kuonekana kama mwezi uliokuwa umeandama siku tatu zilizopita, na hali ya baridi ikazidi kuwa kali, saa 5:55, ni robo ya mwezi tu ndio ilikuwa imebaki kuzama ndani ya Jua.
Saa 6:05 jua linaanza kutoka upande wa mwezi ulikotokea wakati wa kupatwa 
kwa Jua.

Ilipofika saa 6:05, jua likawa tayari limegeukia upande wa pili na kuwa kama mwezi unaoandama mwezi wa Ramadhani, hali ya hewa ikawa bado ni baridi na haileweki kama ni asubuhi, mchana ama jioni.
Saa 7:05 Jua liko huru kuangaza duania baada ya kuachiwa na mwezi na hali
ya hewa inaludia kuwa ya kawaida.

Ilipofika saa 7:05, Jua lilikuwa tayari limeisha uacha mwezi na kuwa huru kuangaza dunia, hali ya joto ikajirudia na hofu kwa waliokuwa wanaogopa ikawatoka. Na ndio ukawa mwisho wa kupatwa kwa Jua kwa hapa Tukuyu.

                                  
                              





No comments:

 
 
Blogger Templates