Kituo cha Afya cha Tukuyu Lutheran Health Centre, kinachomilikiwa na Kanisa la KKKT-Dayosisi ya Konde, ni kituo cha afya kinachotegemewa kwa kiasi kikubwa na wakazi wa Mji wa Tukuyu kwa huduma za matibabu ya afya zao.
Kituo hiki kiko katika eneo la Bagamoyo, pembezoni mwa barabara itokayo Mbeya na kuelekea Kyela, mpaka nchi jirani ya Malawi.
Hakuna mkazi wa Tukuyu au jamaa yake wa karibu ambaye hajawahi pata matibabu katika kituo hiki cha afya, huduma zinazopatikana katika kituoni hicho ni huduma za wagonjwa wa nje na kulazwa, kwa wale ambao hali zao zinakuwa mbaya na wanahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari.
Kila unapokwenda katika kituo hiki utakuta wagonjwa wengi wakiwa wanapatiwa huduma ya matibabu, wingi wa wagonjwa wanaokwenda kutibiwa pale ni dalili tosha kuwa huduma zinazotolewa pale ni za uhakika na wananchi hawana shaka nazo.
Picha chini ni shughuli mbalimbali zinazofanywa na wataalamu wa afya katika kituo hicho.
Jengo la Kituo cha Afya cha Lutheran Health Centre, kilichoko Bagamoyo, Tukuyu Mjini.
Dr. Samson Mwanjala akimpatia matibabu mgonjwa katika kituo hicho.
Dr. Samson Mwanjala akimhudumia mtoto Goodluck Isaya ambaye amelazwa katika kituo hicho
Cha Afya.
Mama wa mtoto Gooluck Isaya akimwangalia mtoto wake akiwa amelazwa kituoni hapo
Ulimboka Tuja Uswege 'Lab Ass Technologist' akiwa kazini katika Maabala ya Kituo cha Afya
Muuguzi Sophia Mwamulenge akimpima mtoto kwenye Kliniki ya kituo cha Afya
Dr.Samson Mwanjala akiwa pamoja na muuguzi mkuu wa kituo Bi Chiripa akiwa pamoja na wauguzi wengine wakipita kuwaangalia wagonjwa waliolazwa katika kituo hicho
Wauguzi, Rachel na Nuru wakimuhudumia mgonjwa aliyelazwa katika kituo cha Afya
No comments:
Post a Comment