Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika mji wa Tunduma na kuwafurahisha vijana na wananchi wa mji huo kwa hotuba yake iliyokuwa na utetezi mkubwa kwa wananchi wa mji huo.
Umati wa wananchi wa Tunduma wakiwasikiliza viongozi wa wa CCM Taifa waliokuwa wakiwahutubi katika mkutano wa hadhara.
Katibu wa NEC Siasa na Uenezi Nape Nnauye akihutubi wananchi wa mji wa Tunduma.
Katibu Mkuu wa CCM akishiriki ujenzi wa Shule ya Msingi Uhuru Mjini Tunduma
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akitembea kuelekea uwanja wa mkutano mjini Tunduma akiwa ameongoza na viongozi wengine wa CCM
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa amepewa uchifu wa kabila na kupewa jina la chifu Pampukanji wa Wanyamwaga. Hapa anaonekana akiwa amevaa joho la uchifu.
Vijana wa Tunduma walioachana na CHADEMA kujiunga na CCM wakishangilia mara baada ya kujiunga na CCM
Mwenyekiti CCM wa Kata ya Majengo Ndugu Danny Mwashuya akiwa na katibu msaidizi wa CCM Wilaya ya Momba bi Getruda Sinyinza wakiwa pamoja na wanaccm wenzao mara baada ya mkutano wa hadhara mjini Tunduma
WanaCCM wakijipongeza baada ya mkutano wa mjini Tunduma, Mwenye kofia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Mkoa wa Mbeya Ndugu. Bashiru Salumu Madodi.
Picha na habari na
Bashiru S. Madodi
No comments:
Post a Comment