Wakati wa mahojiano na GPL.
Kuhusu kubakwa, Felista ambaye pia hutumia majina ya Leylat au Leila, alisema: “Kapuya hakunibaka ila nimezaa naye mtoto mmoja.”
ILIKUWAJE AKAFUNGUKA?
Timu ya waandishi wa habari wa Global Publishers hutekeleza majukumu yake kisayansi, baada ya kurukaruka sana, Felista akidai hahusiki na skandali hiyo na kwamba yeye ni shahidi tu wa mtu anayeitwa Leylat, hatimaye alibanwa kwa maswali magumu, akajikuta akisema ambayo hakuyapanga.
MWANDISHI: Hizi namba 0753 7…7…28 na 0713 7...20…0 (tarakimu mbilimbili zimefichwa), ni za nani?
FELISTA: Ni namba zangu.
MWANDISHI: Hizi namba ndizo ambazo Kapuya ametutumia kwamba ndiyo za mtu ambaye huwasiliana naye na humtumia pesa, na ndiye anayejidai ni denti aliyebakwa na kuambukizwa naye Ukimwi.
FELISTA: Siyo kweli, huyo Kapuya anatafuta njia za kujinasua kwenye hili tatizo lake. Anajua mimi namjua Leylat ambaye ndiye denti aliyebakwa.
MWANDISHI: Wewe unaitwa nani?
FELISTA: Naitwa Felista.
MWANDISHI: Unamjua Halima Hamad?
FELISTA: Halima Hamad simjui.
MWANDISHI: Kapuya kasema denti anayedai kubakwa anaitwa Halima Hamad na ndiye mwenye hizo namba ambazo wewe unakiri ni zako.
FELISTA: Nimesema simjui Halima, mimi naitwa Felista. Aliyebakwa ni Leylat, siyo mimi.
AKUMBUSHWA ALIYOSAHAU
Miaka ya nyuma Felista akitumia mwavuli wa uyatima, aliwahi kuomba hifadhi kwa mmoja wa waandishi wetu wa kike, aliyeishi naye kwa muda mrefu kidogo nyumbani kwake kabla ya kumgundua kwamba ni tapeli, hivyo kuamua kuachana naye.
MWANDISHI: Wewe Felista umesahau kwamba umeshawahi kukaa nyumbani kwangu na kipindi hicho chote, ulikuwa ukiniletea ripoti za shule zenye jina la Halima Humudy. Vilevile ulishawahi kutolewa kwenye gazeti moja la kila siku (halizalishwi na Global), ukiomba msaada kwamba wewe ni yatima, jina ulilotumia ni hilohilo la Halima Humudy.
Hizohizo namba zako, usajili wake wa laini na katika Tigopesa zimesajiliwa kwa jina la Halima Hamad. Haya kataa mbele ya macho yangu!
FELISTA: …. (kimya).
MWANDISHI: Wewe siyo Halima, sema nikusikie.
FELISTA: Ni kweli, Halima Hamad ni mimi, ila hilo jina silitumii sana.
MWANDISHI: Haya sasa, baada ya kukiri Halima Hamad ni wewe, unaweza kutuambia ukweli kuwa wewe ndiye huyo Leylat au Leila unayemtaja.
FELISTA: (Kwa sauti ya chini iliyopoteza ujasiri), ni kweli mimi ndiye mhusika.
MWANDISHI: Sasa kwa nini ulikuwa unakataa?
FELISTA: Nilikuwa sipendi ninyi Global mjue.
MWANDISHI: Haya tuambie ukweli sasa kuhusu wewe na Kapuya.
FELISTA: Nimezaa naye mtoto mmoja.
MWANDISHI: Mbona unatubabaisha? Mara alikubaka, mara umezaa naye mtoto mmoja, ukweli ni upi?
FELISTA: Ukweli ni kwamba yeye ndiye baba wa mtoto wangu.
MWANDISHI: Wewe hujazaa na Kapuya, huu nao ni utapeli mwingine.
FELISTA: Kama hamtaki basi.
MWANDISHI: Kama ni kweli yule ni mzazi mwenzako, mbona unaamua kumchafua na unataka kumharibia maisha yake?
FELISTA: Amekataa kunihudumia ndiyo maana namchafua.
MWANDISHI: Unafikiri hii vita mwisho wake ni nini?
FELISTA: Atakapoanza tena kunihudumia.
MWANDISHI: Haya turudi kwenye pointi ya Ukimwi, kwa nini unamshushia madai mazito kiasi hicho?
FELISTA: Ni kweli nina Ukimwi.
MWANDISHI: Na mtoto wako naye ni mzima?
FELISTA: Mtoto naye ni mgonjwa.
MWANDISHI: Unatumia dawa?
FELISTA: Bado sijaanza kutumia dawa, CD4 zangu bado zipo vizuri.
MWANDISHI: Mbona ulisema mwanzoni kwamba unatumia dawa?
FELISTA: Ni kweli natumia dawa.
MWANDISHI: Mbona unatuchanganya? Mara hutumii dawa, mara unatumia dawa, sasa hivi umesema CD4 zako zipo vizuri.
FELISTA: Nimekwambia natumia dawa. Hata kama CD4 zangu zipo vizuri, natumia dawa hivyohivyo.
MWANDISHI: Katika maisha yako yote umewahi kupata matatizo ya akili? Maana naona kama haupo sawa.
FELISTA: Mimi ni mzima kabisa. Mtaniona kama ni mzima siku nitakaposimama na Kapuya mahakamani.
MWANDISHI: Wewe Felista umewahi kudanganya unasoma Turiani Sekondari, Mugabe Sekondari na Jangwani Sekondari kumbe ni uongo mtupu.
FELISTA: Nimesoma Turiani tu, sijawahi kusoma Mugabe wala Jangwani.
MWANDISHI: Nimeshawahi kukuona umevaa sare za Jangwani, leo unabisha? Na uliniambia unasoma huko.
FELISTA: Siyo kweli.
MWANDISHI: Kwa nini uliwatapeli Dk. Kimei na Mama Salma Kikwete?
FELISTA: Kuhusu Kimei ni uongo, Mama Salma ni watu walitaka kuniharibia, nikapelekwa Segerea lakini nilitoka.
MWANDISHI: Ilikuwaje ukamtapeli Mama Salma kuwa wewe ni yatima?
FELISTA: Nilitaka nipate nafasi ya kusoma Mkuranga, sasa ili nipate nafasi kule ilibidi nionekane nasoma Jangwani, kwa hiyo nilitengeneza nyaraka zinazoonesha nasoma Jangwani ndiyo baadaye ikaonekana nimefanya utapeli.
MWANDISHI: Umeona sasa? Mwanzoni ulikataa kuhusu kujidai unasoma Jangwani, sasa hivi unakiri. Haya sasa twende tukapime Ukimwi.
FELISTA: Sipimi.
MWANDISHI: Sisi tunaamini hauna Ukimwi. Hata mwanzoni ulishatuthibitishia kuwa ulishapima na upo salama. Kama una uhakika wewe ni mwathirika basi twende tukapime.
FELISTA: Sipimi nimesema.
NI SKANDALI LA VIGOGO
Katika mahojiano hayo, Amani limeweza kubaini kuwa wapo wanasiasa kadhaa ambao wapo nyuma ya Felista na ndiyo wanaompa kampani kwenye harakati zake za kumchafua Kapuya.
Mmoja wa wabunge wa Mkoa wa Tabora (CCM), sauti yake imenaswa mara mbili kwenye simu ya Felista, ya kwanza akimuelekeza binti huyo: “Njoo Dodoma, nitakuitia waandishi wa habari, ufanye mkutano nao uwamwagie kila kitu.”
Sauti nyingine ya mbunge huyo, inasikika ikihoji: “Nimesikia Kapuya anatangaza wewe una watoto wawili, ni kweli?” Felista anasikika akipinga na kusema hana mtoto hata mmoja.
Wapo wanasiasa wengine ambao wamebainika kumuunga mkono Felista, hivyo kuzidi kulifanya ‘saga’ hilo lionekane la kisiasa zaidi.
CHANZO:- AMANI VIA GPL
No comments:
Post a Comment