Social Icons

Wednesday, 11 December 2013

WANAJESHI WA UN WAPAMBANA NA FDLR


Wanajeshi wa UN wakisaidiana na wanajeshi wa DRC waliweza kuwashinda vita waasi wa M23

Kamanda wa wanajeshi wa Umoja wa mataifa katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, anasema kuwa wanajeshi wake wameanza kupambana na waasi wa Kihutu kutoka Rwanda pamoja na makundi mengine ya waasi Mashariki mwa nchi.

Kamanda huyo, Generali Carlos Alberto dos Santos Cruz, anasema kwamba wanajeshi wake wanajiandaa kupambana na waasi wa FDLR walio Katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kundi hilo, lilianzishwa na wapiganaji wa kihutu waliokimbilia Congo Mashariki kutoka Rwanda wakati wa mauaji ya kimbare mwaka 1994.

Mwezi jana wanajeshi wa UN kwa kutumia nguvu waliweza kuwashinda waasi wa M23 waliokuwa wanaendesha harakati zao Mashariki mwa Congo.


Chanzo:- BBC

No comments:

 
 
Blogger Templates