Social Icons

Friday, 12 September 2014

HADITHI: Missed call ya shemeji -12


Uzuri wake, dada mtu huyo alipoona simu ya Beka hakuminya batani yoyote ile ya simu yake hivyo ilionekana kweli hakuiona.
Dada huyo hakuwa na sababu ya kwenda kwenye meseji, akaiweka simu kitandani…
“Dada…”
“Abee.”

SASA JIMWAGE MWENYEWE…

asa dada mtu alianza kuwa mpole fulani hivi aliitikia kwa upole. Yeye alijua dada yake ameona meseji zake kwa mumewe maana hajawahi kufuta.

“Beka na wewe mkoje? Niambie ukweli dada yangu.”
“Sisi?”

“Ninyi ndiyo, si ndiyo nakuuliza wewe!”
“Hatuna ugomvi mbona!”
“Sijasema mna ugomvi dada, ila nahisi kama mienendo yenu haiko sawa.”
“Kivipi mdogo wangu Aisha?”
“Kwa nini akubipu?”

“Sasa hilo ungemuuliza wewe mumeo kwa nini alinibipu wakati mimi sibipiki.”
Aisha alishindwa kujizuia, akajikuta akicheka mwenyewe kwa majibu ya dada yake kule kusema ‘mimi sibipiki’.

Alisimama akaondoka kurudi chumbani kwake akiwa na mawazo sana.
Alikaa kitandani, akajiinamia akiwaza mambo mbalimbali kuhusu dada yake na maneno yake…
“Lakini iko sababu ya kuangalia vizuri ukaribu wa Beka na dada, mimi kama siuelewi. Juzi Beka ametoka chumbani asubuhi, nimemtafuta kote hayupo, eti mwisho nakuja kumwona akiwa bafuni. Inawezekana kweli?”

“Haya, leo tena ndiyo hivyo. Namtafuta kote, baadaye eti alitoka uani na dada nakutana naye anatoka chooni! Mh! Hapa naweza kuliwa bila mwenyewe kujijua,” aliwaza sana Aisha kisha akapanda kitandani kulala akiwa ameamua jambo moja moyoni mwake.

***

Asubuhi kulipokucha, Aisha alitoka kwenda jikoni, akamkuta dada yake ameshaamka amebandika maji kwenye sufuria kubwa…
“Maji anaoga nani dada?” Aisha aliuliza.
“Hiyo ndiyo salamu mdogo wangu?”
“Ah! Sorry, shikamoo.”

“Mumeo haogi leo?” Dada mtu huyo alidakia mambo mengine badala ya kujibu salamu hiyo.
“Alikwambia anaoga maji ya moto? Maana mi sijawahi kumwona au kumsikia akioga maji ya moto hata siku moja.”

“Basi mjaribu kumtengea leo uone kama atachomoa.”
Aisha hakuongeza maneno, aliendelea na mambo mengine huku akiwa hana amani ya moyo. 
“Lazima kuna kitu, lazima kabisa,” alisema moyoni Aisha.

Siku hiyo mumewe Beka alikuwa ameanza likizo ya siku ishirini na nane kazini, kwa hiyo alikuwa haendi kazini lakini yeye Aisha alitakiwa kwenda kwenye biashara yake.
Nyumbani alimwacha dada yake na mumewe lakini wakati anaondoka aliuliza…
“Darling leo utatoka?”

“Yeah, baadaye sana lakini.”
“Utaenda wapi?”
“Misele yangu tu.”
“Oke, nilitaka kujua tu,” alisema Aisha na kutoka zake.

***

“Baby vipi?” Dada mtu alimsemesha Beka shemeji yake kwa sauti yenye mvuto wa kimahaba.
“Poa, niambie.”
“Nimefurahi sana.”
“Kwa nini?”
“Kuwepo nyumbani leo. Najua leo ndiyo ile ndoto yangu ya mimi kuwa mke, wewe mume itatimia.”
“Utaitimizaje?”

“We utaona mwenyewe.”
Dada mtu huyo akaondoka kwenda jikoni ambako alikaanga mayai manne, akatengeneza na kachumbari kwa pembeni kisha akampelekea Beka mezani akiwa ameambatanisha na maji ya kunawa yenye uvuguvugu…

“Mh! Hii kali leo, ndiyo kifungua kinywa au?”
“Kifungua kinywa kinakuja mume wangu wala usijali. Mimi ni mkeo na wewe ni mume wangu.”
Beka alicheka tu huku akimkazia macho shemejiye wakati anaondoka kwenda jikoni. Alivaa gauni la kawaida na juu yake akatupia khanga moja.

“Da! Si mchezo,” alisema moyoni Beka akijiweka vizuri. Tayari mwili ulishaanza kusisimka kwa kuona tu na kuvuta picha anavyokuwa naye kwenye uwanja wa sita kwa sita.
“Huyu dawa yake ni kufunga milango mchana kutwa, mpaka ikifika jioni mdogo wake anarudi, sisi hatuna hamu tena,” aliendelea kujisemea mwenyewe moyoni mwake.
Mara, sinia ilifikishwa mezani, ndani yake mlikuwa na chai ya maziwa na soseji mbili, akatengewa na kukorogewa…

“Karibu mume wangu mpendwa,” alisema dada mtu.
“Ooo! Asante my wife. Kweli wewe ni mke mwema,”
“Umeona ee? Wengine watasubiri.”
“Watasubiri sana tu.”
Beka aliipiga chai hiyo nzito, alipomaliza alisimama kumfuata shemeji yake chumbani ambapo alimkuta ametoka kuoga sasa anajifuta maji kwa upande wa khanga…
“Karibu baby.”

“Asante, nimekumisi sana ndiyo maana nimekuja.”
“Mimi je? Hivi hapa nilikuwa navaa ili nije unitendee haki.”
“Kwa hiyo nikakusubiri sebuleni,” alisema Beka huku akimshikashika shemeji yake sehemu mbalimbali za mwili hali iliyomfanya atoe mlio wa kama mtu anayetoneshwa.
Aliacha kuendelea kujifuta na kumgeukia Beka, wakatazamana kwa macho ya kurembua huku wote wakianza kuhema.

***

Aisha alipofika nyumba ya nne aliingia kwa rafiki yake mmoja aitwaye Diana. Akamsimulia hali ilivyo nyumbani kwake na kile anachokifikiri…

“Hivi hapa siendi kwenye shughuli zangu, baada ya nusu saa narudi, najua tu kama kuna kitu nitawakuta katika mazingira tata,” Aisha alimwambia Diana.

Itandelea

Chanzo globalpublishers

No comments:

 
 
Blogger Templates