Baada ya wawili hao kuondoka, meneja akamgeukia Faidha…
“Faidha.”“Ndiyo bosi wangu.” RUKA NAYO SASA…“
Unajua ni jambo la ajabu sana limetokea?”
“Sijaelewa bosi.”“Mwanamke kuja kufanya fujo hapa kazini!”
Faidha aliposikia hivyo alibaki amejiinamia tu kwa aibu kwani hata dhamira yake ilimwambia kilichotokea si cha kawaida.
“Ni kweli bosi.”
“Kama ni kweli itabidi uandike barua ya kujieleza kwa nini uongozi usikuadhibu?”
“Samahani bosi.”“Mimi langu ni hilo tu,” alisema bosi huyo huku akitoka kwa hasira.
Faidha alikaa na kujiinamia. Mawazo kibao kichwani yalimpata. Alianza kukasirika na yeye akiamini bila Aisha yasingetokea yale yote…
“Dawa yake yule kumchukulia mume wake moja kwa moja sasa,” alisema moyoni Faidha akijiapisha kwa dhati.Akina Salma nao walirejea baada ya kumuona bosi wao ametoka…
“Kwani dada Faidha vipi? Yule mwanamke ana akili timamu kweli?” walimuuliza…
“Ah! Yule kachanganyikiwa, kabip akapigiwa sasa anatapatapa tu…yeye angedili na mumewe si kuja ofisini kwa watu.”
“Ni kweli dada Faidha, sisi wenyewe tumemshangaa sana. Halafu hata wewe huna kosa kwani ulimuita aje hapa?”“Si ndiyo hapo sasa!”
“Mh! Wanawake wengine bwana, ni wa ajabu sana,” alisema Salma…
“Wa ajabu wa ajabu,” alimalizia Faidha.
***
Beka na Aisha walifika nyumbani, kila mmoja alitaka kumsikia mwenzake anasema nini kuhusu lilitokea lakini Beka akaonekana kutosubiri, akaanza…
“Mwezi ujao nafunga ndoa na Faidha.”
“Si alisema pale hataki uke wenza, hukumsikia?”
“Hatakuwa mke wenza, wewe nakupa talaka yako sasa hivi, sitaki ujinga mimi!”
“Unipe talaka nimekukosea nini mimi?”
“Hujui ee?” Basi subiri utajua tu.
Haiwezekani uwe mwanamke wa fujo, hekima imekupitia pembeni wewe,” alifoka Beka, akaenda kununua karatasi dukani na kumwandikia talaka Aisha.
Siku ya pili, Aisha alirudi kwa wazazi wake na kusimulia yaliyompata akaambulia kupewa pole nyingi. Alikaa kwao kwa mwezi mmoja akarudi mjini kuanza maisha yake mwenyewe, Beka akafunga ndoa na Faidha.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment