Social Icons

Saturday, 4 October 2014

Muingereza mwingine akatwa kichwa na IS

Alan Henning kushoto mda mchache tu kabla ya kukatwa kichwa na mtu aliyesimama kando yake.

Kundi la wanamgambo wa kiislamu la Islamic state limetoa ukanda wa video unaoonyesha mateka Alan Henning raia wa Uingereza akikatwa kichwa.

Henning mwenye umri wa miaka 47 ambaye ni dereva wa texi kutoka kaskazini mwa Uingereza alitekwa nyara mwezi Disemba mwaka uliopita alipokuwa akilifanyia kazi shirika moja la kutoa huduma za misaada kwa wakimbizi nchini Syria.

Kundi la Islamic State ambalo limechukua udhibiti kwenye maeneo ya mpaka kati ya Syria na Iraq tayari lishawaua waandishi wa habari raia wa Marekani James Foley na Steven Sotlof pamoja na mfanyikazi wa kutoa huduma za misaada kutoka Scotland David Haines.

Mapema babake John Cantlie raia wa Uingereza ambaye anashikiliwa mateka na wanamgambo wa Islamic State aliomba kuachiliwa kwa mwanawe.

Chanzo BBC

No comments:

 
 
Blogger Templates