Social Icons

Saturday, 7 February 2015

Hadithi: Familia tata - 16


“HEBU punguza munkari mtoto mzuri, mbona una haraka?” Festo alimwambia Asfat, ambaye kwa maneno hayo akajisogeza karibu zaidi, sasa wakawa wanapumuliana.
Sasa endelea..Katika hali ya ulevi, Festo alijikuta akilegea, kifua cha Asfat kilimpa ushawishi mpya, akajikuta akihemka.

Mikono yake ikafanya ziara isiyo rasmi katika maeneo kadhaa ya binti huyo, ambaye miaka yake minne aliyoishi na kusoma Ulaya ilimfanya azidi kuvutia, akionekana msichana wa makamo, wakati ukweli ni kwamba alikuwa bado mdogo.

“Asfat,” Festo hatimaye aliita, akiwa amemsogeza jirani zaidi, vifua vyao vikiwa vimegusana. Moyoni, msichana akajikuta akiangua kicheko cha ushindi, kasi ya kisasi ikazidi mapigo yake ya moyo.
“Abeee,” Asfat aliitika kimahaba, kitu kilichomuongeza munkari Festo.

“Sikuwahi kufikiria kama tungeweza kufanya hivi, wewe ni msichana, kwa kuwa umeridhia mwenyewe jambo hili, sina kipingamizi, nadhani ulichelewa kuniambia hata hivyo, unaonekana ni hot kweli kama ulivyosema, ooh, I love you,” Festo, asijue alikuwa ameingia kirahisi katika mtego wa Asfat, alijikuta akisema maneno hayo.

“Me too,” Asfat alijibu, naye huku akijiweka karibu zaidi, akiruhusu mwili wake laini uwe mali ya Festo.
Ni saa nne kasoro robo usiku. Mwili wa Festo ulishaanza kuchemka, kinywaji kile kikali, kilionekana kumzidi nguvu. Joto la msichana mzuri kama aliyekuwa pembeni yake, lilimfanya auruhusu mwili wake ufikie tamati ya matamanio yake. Hakudhani kama alihitaji ufundi zaidi, kilichokuwa mbele yake ni kumalizia kazi ndogo iliyoanzishwa na Asfat.

“Nadhani tuondoke, twende zetu sehemu mara moja halafu turudi home, au?” Festo alimwambia Asfat, aliyejibu kwa kutikisa kichwa. Wakainuka, wakalipa fedha walizokuwa wakidaiwa, wakaingia ndani ya gari, Festo akakanyaga mafuta, gari likaserereka na kutokomea kwa kasi.

Vijana kadhaa waliokuwepo wakashangilia kama kawaida yao kila Festo alivyozoea kuendesha kwa manjonjo, wazee wazima wawili watatu waliokuwepo wakatingisha vichwa vyao kwa masikitiko.

Gari likasimama nje ya Hoteli ya Flamingo, iliyopo eneo linalojulikana kama Madale kwa Kawawa. Mhudumu mmoja wa kiume alilifahamu gari la Festo na alimjua fika kijana huyo mpenda mabibi. Akamfuata na kumsalimia.

“Kama kawaida?” alimuuliza baada ya kumsalimia na msichana aliyekuwa naye.
“Unauliza majibu,” Festo alimwambia huku akiweka vitu sawa ndani ya gari lake.
“Inaonekana wewe ni mteja mzuri hapa,” Asfat alimuuliza Festo.

“Nilishakuambia mimi kijana, niliogopa tokea awali kukukwaza, lakini umesema nitatulia, hebu twende ukanitulize,” Festo alisema huku akimpiga  busu Asfat, wakashuka garini, wakatokomea ndani.

***
Saa moja baadaye, Festo na Asfat waliibuka kutoka ndani, kila mmoja akionekana kufurahia nafsi yake. Wakatafuta kiti kilichokuwa pembeni kidogo, wakakaa na kuagiza chakula, Festo akiletewa mchemsho wa nyama ya ng’ombe, huku Asfat akila ndizi za kuchoma na mishikaki.

Ilikuwa ni moja ya siku chache ambazo Festo aliwahi kujisikia vizuri baada ya kuwa na mwanamke. Ni kweli, Asfat alikuwa hot. Alihisi kukosa mambo mengi kwa msichana huyu, na kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya kimapenzi, akahisi wivu.

Na hata Asfat, alimsifu Festo. Siku zote alimuona kijana mlevi, asiye na dira kimaisha na aliamini kabisa, kwa vyovyote pombe zingemfanya kuwa goigoi kitandani. Alikosea, jamaa alikuwa fundi, muwajibikaji. Akajihisi kumpenda pia, alitamani aanze maisha rasmi na kijana huyo.

Lakini upendo wake kwa mdogo wake Santo, ulilifukuza haraka wazo na kuishi kimapenzi na Festo, alitamani kumuangamiza, wakati wowote akipata nafasi, hata leo hii. Kwa hasira, akaagiza bia!!
Na festo akalazimika kuagiza mzinga mdogo wa konya, wakanywa huku wakihimizana kumaliza ili wawahi nyumbani.

Wakamaliza vinywaji vyao, wakaanza kulielekea gari. Asfat akaomba aendeshe yeye, Festo akamruhusu, akazunguka kushoto, akimuacha msichana akielekea kulia.

Nini kiliendelea? Festo na Asfat wamepona? Usikose kufuatilia muendelezo wa simulizi hii katika toleo lijalo.


Chanzo Globalpublishers

No comments:

 
 
Blogger Templates