Wakulima wakisubili wateja kuja kununua ndizi katika soko la Tandale |
Mkulima wa ndizi akiwasili katika soko la Tandale mjini Tukuyu. |
Mama huyu akiangalia mikungu ya ndizi zake, bila ya kujua hatma yake |
Mnunuzi wa maparachichi akiwa pembeni ya mzigo wake tayari kuusafirisha |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Mwakasangula Mwakipiki, ambaye Halmashauri yake ina wajibu wa kuwatafutia wakulima wake wanunuzi wa mazao yao. |
Soko kuu la wakulima Tandale mjini Tukuyu Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya limekosa wateja wa mazao ya chakula na kusababisha kushuka kwa bei ya mazao hayo hasa mazao ya ndizi, maparachichi na mazao ya mbogamboga ambayo hutegemewa sana kununuliwa na wanunuzi kutoka nje ya wilaya ya Rungwe na nje ya mkoa wa Mbeya.
Wakizungumza sokoni hapo wakulima wa mazao ya chakula wamesema kwamba wateja wao wanaokuja kununua mazao yao kwa kipindi hiki wamepungua sana, ukilinganisha na vipindi vingine na bei ya mazao imeshuka tofauti na vipindi vingine. Bei ya mazao sokoni hapo hutegemea sana wingi wa wanunuzi wa mazao wanaofika sokoni hapo.
Upungufu wa wanunuzi wa mazao yao umesababisha wakulima kuuza mazao yao kwa bei ya hasara na kufuata bei anayoitaka mnunuaji kwa kuogopa kubakiwa na mzigo mkubwa ambapo kwa sasa mkungu mzuri wa ndizi katika soko la Tandale unafikia shilingi elfu tatu.
“Kipindi hiki bei imeshuka kabisa na kumumiza mkulima wa mazao ya chakula hasa zao la ndizi na maparachichi ndiyo yamekuwa na bei ya chini sana kwani mkungu mkubwa moja wa ndizi aina ya mzuzu, unauzwa kwa shilingi elfu tatu mpaka elfu nne na ndizi aina ya malindi na aina zingine zinauzwa kwa shilingi elfu moja mpaka elfu moja mia tano kwa mkungu uliokomaa vizuri. Tofauti na wakati ambao wateja wa ndizi wanapokuwa wengi ndizi mkungu mmoja huuzwa kati ya Shilingi elfu saba mpaka elfu nane.
Upande wa maparachichi ujazo wa gunia moja limeuzwa kwa shilingi elfu ishirini na tano, wakati kipindi kukiwa na wateja wengi, gunia moja la maparachichi huuzwa kati ya shilingi elfu therathini na tano mpaka elfu arobaini.
Wakulima wa ndizi wanaouza ndizi katika soko la Tandale wameuomba uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kuwatafutia soko la mazao yao katika maeneo mengine ya nchi yetu na nchi jirani kama Zambia na Malawi.
Akiongea na mwandishi wa blog hii Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. mwakasangula Mwakipiki amesema Halmashauri yake imeshaanza kuwatafutia masoko wakulima wa halmashauri yake, na kwa kuanzia wameshaanza mazungumzo na Manispaa ya Kinondoni ili kupata eneo la kuuzia mazao toka katika halmashauri yake.
Na Basahama blogspot
No comments:
Post a Comment