Social Icons

Friday 27 November 2015

Maana jina Kaizari na historia yake

Kaizari

(Elekezwa kutoka Kaisari)
Julius Caesaralikuwa asili ya cheo cha Kaizari
Mtawala waUfaransa Napoleon Bonapartealiyejiwekea taji la Kaizari 1804
Kaizari Bokassa 1977

Kaizari ni cheo cha mfalme mkuu. Neno la Kiswahili limetokana na lugha ya Kijerumani "Kaiser" lakini asili yake ni Kilatini "Caesar".

Do you want to try some new features? By joining the beta, you will get access to experimental features, at the risk of encountering bugs and issues.

Asili ya KiromaEdit

Asili ya cheo ni Julius Caesar aliyekuwa kiongozi wa Dola la Roma hadi kuuawa kwake na wapinzani mwaka 44 KKWatawala waliomfuata walianza kutumia jina la Caesar kwa heshima yake hadi jina lilikuwa cheo.

Cheo cha Kaizari kiliendelea kutumika katika eneo la Dola la Roma ya Mashariki (Bizanti) hadi 1453.

UlayaEdit

Katika Ulaya yenyewe mfalme wa Wafaranki Karolo Mkuu alipokea cheo cha "Caesar" au Kaizari. Baadaye wafalme Wajerumani waliomfuata Karolo Mkuu katika sehemu ya mashariki ya ufalme wake waliendelea kutumia cheo hiki cha Caesar au Kaizari.

Neno la Kaizari liliingia katika lugha ya Kiswahili wakati wa ukoloni wa Kijerumani hukoTanzaniaAustria na Ujerumani zilitawaliwa hadi mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia1918 na wafalme wenye cheo cha "Kaizari" (kijer.: Kaiser).

Vilevile mfalme wa Urusi alikuwa na cheo kilekile kilichoitwa "Tsar" kwa Kirusi, ilhali neno hili limeundwa pia kutoka kwa "Caesar".

Lugha za Kiingereza na Kifaransa zilitumia cheo tofauti cha macaesar wa Kiroma ndicho "Imperator" (=mwenye amri, mwenye mamlaka, jemadari) kilichokuwa "Emperor" (Kiing.) au "Empereur" (Kifaransa).

Nje ya UlayaEdit

Kaizari ni cheo cha mfalme aliye juu ya wafalme wengine. Kutokana na uzuefu huu hata Shah wa Uajemi, Tenno wa Japani, Huangdi wa China na Negus Negesti wa Ethiopiahutajwa kwa cheo cha "Kaizari".

Malkia Viktoria alitumia cheo cha Kaizari ("empress") kama mtawala wa Uhindi tangu 1877.

Wakati wa ukoloni mtawala mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani alikuwa Kaizari Wilhelm II wa Ujerumani; kwenye sarafu ya rupia alionyeshwa pamoja cheo kwa lugha yaKilatini "imperator".

Rais Jean-Bedel Bokassa alijitangaza kuwa Kaizari ("empereur") wa Afrika ya Kati mwaka1977 akiiga mfano wa Napoleon Bonaparte aliyejiwekea taji la Kaizari ya Ufaransa mwaka1804. Bokassa alipinduliwa 1979 na nchi kuwa jamhuri tena.

No comments:

 
 
Blogger Templates