Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutuglu, ameahidi kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wauaji wa wakili mashuhuri anayetetea masilahi ya Wakurdi.
Wakili Tahir Elci alipigwa risasi jana katika mji wa Kusini Mashariki wa Diyarbakir.
Wakili huyo alikuwa akihutubia mkutana wa wanahabari alipopigwa risasi shingoni akafa.
Afisa mmoja wa polisi pia alifariki katika makabiliano hayo.
Bwana Elci alipigwa risasi alipokuwa akitoa wito wa amani kati ya wapiganaji Wakurdi wanaotaka kujitenga na maafisa wa usalama
Watu wanaounga mkono makundi ya Kikurdi walisema kuwa mauaji yake yalipangwa kikamilifu.
Polisi wa Uturuki walitumia mifereji ya maji na kutifua moshi wa kutoa machozi kuwatawanya mamia ya waandamanaji mjini Istanbul waliokuwa wakipinga mauaji ya mwanasheria hiyo.
Chanzo: bbc
No comments:
Post a Comment