Social Icons

Wednesday 27 January 2016

Dunia yakumbuka maangamizi ya Wayahudi

Watu duniani kote leo wanaadhimisha mwaka wa 71 tangu kukombolewa kwa kambi ya maangamizi ya Auschwitz nchini Poland. Ni katika kambi hiyo ambamo mafashisti wa kijerumani waliwaangamiza wayahudi.

Polen Ausschwitz Gefangene 70 Jahre Befreiung

Katika kuwakumbuka wayahudi na watu wengine waliongamizwa na mafashisti katika kambi Auschwitz, Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesisitiza umuhimu wa kupambana na aina zote za ubaguzi.

Waziri Steinmeier amesema ikiwa wayahudi na watu wengine wenye maoni tofauti ,barani Ulaya kote, hawatahisi kuwa salama, basi hapatakuwapo tena mtu yeyote ataekahisi kuwa salama.

Waziri Steinmeier amekumbusha juu ya wayahudi Milioni sita na watu wengine waliouliwa na mafashisti. Amesema watu wote, na siyo viongozi tu, wanao wajibu wa kuutimiza katika kupinga aina zote za ubaguzi.

Bunge la Ujerumani leo linaadhimisha mwaka wa 71 tangu kukombolewa na majeshi ya Umoja wa Kisoviet, kwa kambi ya maangamizi ya Auschwitz kwa maonyesho yatakayofunguliwa na Spika wa Bunge hilo Nobert Lammert mjini Berlin.

Mgeni wa heshima atakuwa mtaalamu Ruth Klüger atakeotoa hotuba.Mtaalamu huyo ni miongoni mwa watu wachache walionusurika maangamizi kwenye kambi ya Auschwitz nchini Poland.

Kansela Merkel ahimiza mafunzo ya historia kwa vijana

Kansela Angela Merkel na Ernst Cramer alienusurika maangamizi

Kansela Angela Merkel na Ernst Cramer alienusurika maangamizi

Ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha ukombozi huo, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mapema wiki hii alifungua maonyesho ya kazi za sanaa za watu waliofungwa kwenye kambi hiyo. Kansela Merkel amesema maonyesho hayo yanapaswa kuwa mafunzo muhimu ya historia kwa vijana.

Amesema mafunzo hayo ni muhimu hasa wakati huu ambapo Ujerumani inapokea idadi kubwa ya wakimbizi hasa kutoka Mashariki ya Kati. Kiongozi huyo wa Ujerumani amesema mkazo unapaswa kuwekwa hasa juu ya vijana wanaotoka katika nchi ambako chuki dhidi ya Wayahudi imeenea.

Katika kuwakumbuka watu walioangamizwa na mafashisti kwenye kambi ya Auschwitz, Rais Obama leo atawaenzi watu wanne ikiwa pamoja na Wamarekani kutoka majimbo ya Indiana na Tennessee waliohatarisha maisha yao ili kuwalinda wayahudi .

Rais Obama ameungana na viongozi wa wayahudi kwenye ubalozi wa Israel mjini Washington ili kuwakumbuka mamilioni ya watu waliongamizwa na mafashisti. Watu zaidi ya 1,300,000 waliangamizwa na mafashisti kwenye kambi ya Auschwitz kabla ya kukombolewa na majeshi ya Umoja wa Kisoviet.

Mwandishi Mtullya Abdu.

Picha na michoro imepelekwa kwenye maonyesho hayo kwenye nyumba ya historia ya Ujerumani.Makumbusho ya


Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank - Walter Steinmeier amese

Chanzo, Dw.de

No comments:

 
 
Blogger Templates