Social Icons

Wednesday 27 January 2016

TRL yasitisha safari zake Dar, yazihamishia Dodoma

KAMPUNI ya Reli nchini (TRL)imetangaza kuhamisha huduma zake za usafirishaji kutoka mkoani Dar es Salaam hadi mkoani Dodoma kutakana na Tatizo la miundomi ya Reli iliyoaribika kutokana na Mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni mkoani Morogoro.
TREEN 2

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam afisa habari wa TRL, midraji Mahezi kwaniaba ya Kaimu mkurugenzi mtendaji wa TRL, Mhandisi Elias Mshana, amesema TRL wamefikia hatua hiyo ili kupisha ukarabati wa tuta la reli lilopo kati ya stesheni za Kidete na Kilosa zote mkoani Morogoro.

“Kutokana na Mafuriko ya eneo la Kidete na Kilosa kutojulikana lini yataisha ,uongozi umeamua kwa sasa kusitisha zoezi la ukarabati ili kuokoa rasilima zilizotumika katika eneo hili,hata hivyo kazi ya kuzuia uharibifu zaidi dhidi ya tuta la reli inaendelea kulingana na hali inavyojitokeza” amesema Mahezi.
MAHEZI TRL
Mahezi,amefafanua kuwa japo hatua hiyo itaongeza gharama lakini ni muhimu kwa huduma za usafirishaji ziendelee ili kuwasaidia watanzania kiuchumi na kijamii kadri inavyowezekana akieleza kuwa huduma ya reli inapunguza kasi ya uharibifu wa barabara zetu ambazo sio mda mrefu zimejengwa kwa gharama kubwa,

Hata hivo,Mahezi amewaomba radhi watumiaji wa huduma hiyo kwa kuwataka kuwa wavumilivu mpaka huduma hiyo itakaorejeshwa tena mkaoni hapa,

Vilevile,Mahezi amesema uzoefu unaonyesha kuwa sio mara ya kwanza kusitisha huduma hiyo kwa madai kuwa katikakiindi cha mwaka 1998 na 2010 huduma za reli zilihamia mkoani Dodoma ,wakati viindi hivyo maeneo ya Kidete na Kilosa yalipokutwa na mafuriko kama ya mwaka huu.

No comments:

 
 
Blogger Templates