Social Icons

Tuesday 26 April 2016

Kamanda wa Machar awasili Juba


  • 25 Aprili 2016
Image copyrightGetty
Image captionKamanda wa Machar awasili Juba

Mkuu wa jeshi linalomuunga mkono kiongozi wa waasi Riek Machar, bwana Simon Gatwech Dual amewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba.

Kuwasili kwake kunaibua matumaini ya kufufuka kwa harakati za kutekelezwa kikamilifu kwa mkataba wa amani uliotiwa sahihi yapata miezi 8 iliyopita.

Kamanda huyo Gatwech Dual aliwasili kutoka Ethiopia akiandamana na kikosi cha wanajeshi 100.

Hiki kilionekana kuwa ni kikwazo kikubwa kwa kiongozi wa waasi kuweza kurejea Juba ambapo alisisitiza kuwa lazima kwanza awasili Gatwech, wanajeshi pamoja na silaha.

Msemaji wa waasi alisema Machar sasa atarejea Juba kesho

Machar, ambaye aliondoka juba wakati vita vya wenywe ka wenyewe vilipoanza Desemba mwaka wa 2013, anatarajiwa kuunda serikali ya umoja na mpinzani wake mkuu Rais Salva Kiir.

Image copyrightReuters
Image captionUjio wake unafufua matumaini ya utekelezwaji wa mkataba uliotiwa sahihi miezi 8 iliyopita

Machar anatarajiwa kurejea na kukabidhiwa wadhfa wa makamu wa rais baada ya kufutwa na rais Kiir miezi michache kabla ya machafuko ya wenyewe kwa wenyewe kutibuka.

Kwa sasa, Machar yuko katika kambi ya waasi karibu na mpaka wa Ethiopia.

Itambidi avuke hadi Ethiopia, kwa uwanja wa ndege ambao uko karibu, katika maeneo ya Gambela, ili aweze kupanda ndege ya kuelekea Juba

Msemaji wa waasi William Ezekiel amenukuliwa akisema kwamba wapiganaji wa Machar wapatao 195 pamoja na mkuu wa majeshi Simon Gatwech Dual amabao wamewekwa chini ya vikwazo na Marekani na Umoja wa Mataifa, pia walikuwa wanatarajiwa kurejea Juba hii leo.

Ezekiel amelaumu kuchelewa kurejea kwa Machar mjini Juba kutokana na wahisani ambao walikuwa wanafadhili msafara wake kujiondoa.

Maelfu ya watu wameuawa na zaidi ya milioni mbili kutoroka makwao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Image copyrightReuters
Image captionKwa sasa, Machar yuko katika kambi ya waasi karibu na mpaka wa Ethiopia.

Vita hivyo vimeibua uhasama mkubwa wa kikabila na ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Marekani, Uingereza na Norway ziliungana kupitia mchakato maarufu kama Troika, na wamekuwa wakitoa misaada kwa ajili ya amani nchini Sudan Kusini, zikisema kwamba pande zote mbili lazima zionyeshe nia ya dhati ya kuleta amani.

Ubalozi wa Uingereza unasisitiza kwamba kurejea kwa Machar ni muhimu sana katika mchakakato wa kuunda serikali ya Umoja

Chanzo. bbc


No comments:

 
 
Blogger Templates