Social Icons

Friday, 12 August 2016

Jaribio la mapinduzi lilivyozimwa Uturuki


  • Habari NO : 766242
  • Rejea : abna.ir
Brief

Baadhi ya Viongozi hususan wale wanaoshirikiana na Uturuki katika kuleta machafuko nchini syria wametowa wito wa kuwepo utulivu nchini humo ambapo Rais Barack Obama wa Marekani na nchi nyengine za magharibi wamehimiza kuungwa mkono kwa serikali ya nchi hiyo ambayo wamesema imechaguliwa kwa njia ya demokrasia.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Vikosi tiifu kwa rais wa Uturuki vimezima jaribio la mapinduzi usiku wa Ijumaa  ya jana tarege 15 mwezi wa 07 mwaka 2016 kufuatia mashambuliano ya risasi yaliyohusisha pia ndege za kivita na kugharimu maisha ya zaidi ya watu 250.

Kufuatia upinzani wa umwagaji damu kwa utawaka wake wa miaka 13 Rais Recep Tayyip Erdogan amewataka wafuasi wake kuendelea kubakia mitaani kuzuwia kuibuka upya kwa machafuko ya Ijumaa usiku katika nchi hiyo mwanachama muhimu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO ambayo imekuwa ikidhamini machafuko na mapinduzi nchini Syria.

Uturuki ni moja kati ya nchi zinazosaidia magaidi na waasi nchini Syria ili kuangusha utawala halali wa Bashar asad na kwa sasa nchi hiyo imejikuta ikiwa kwenye matatizo kama yale inayoyasababisha nchini Syria.

Baada ya kukamatwa kwa takriban wanajeshi 2,839 katika msako wa waliohusika na njama hiyo ya mapinduzi serikali inamtupia lawama Sheikh Fethullah Gulen anayeishi Marekani ambaye ni hasimu mkuu wa Erdogan kwa kuhusika na njama hiyo ya mapinduzi.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema Jumamosi kwamba Marekani itaisaidia Uturuki katika uchunguzi kuhusu jaribio hilo la mapinduzi lililoshindwa na imeitaka serikali ya nchi hiyo kuwasilisha ushahidi ilio nao dhidi ya sheikh huyo anayeishi Marekani.

Hataru kubwa kwa demokrasia

Waziri Mkuu Binali Yildrim amesema akiwa nje ya ofisi zake mjini Ankara akiandamana na mkuu wa majeshi wa Uturuki ambaye mwenyewe alikuwa akishikiliwa mateka na wahusika wa njama hiyo kwamba "serikali inaidhibiti hali hiyo kikamilifu.

"Akilielezea jaribio hilo la mapinduzi kuwa ni "doa jeusi" kwa demokrasia ya Uturuki Vildrim amesema watu 161 wameuwawa katika machafuko hayo ya usiku na wengine 1,400 wamejeruhiwa.

Idadi hiyo inaonekana kutojumuisha wanajeshi101 walioasi waliouwawa usiku na hiyo kufanya jumla ya watu waliouwawa katika mchafuko hayo kufikia 265.

Wakati madaraka ya nchi yalipokuwa mashakani wakati wa usiku umati mkubwa wa watu wafuasi wa chama tawala cha Haki na Maendeleo (AKP)cha Rais Erdogan waliokuwa wakipeperusha bendera walikaidi amri ya kutotoka nje na kuandamana mitaani kuzuwia jaribio hilo la kuipindua serikali.

Erdogan alitumia mtandao wake wa Twitter kuwahimiza watu wajitokeze mitaani kuhakikisha hakuna upinzani zaidi kwa madaraka yake.

Hali ilivyokuwa

Wakati kulipokucha picha za televisheni zilionyesha uharibifu mkubwa wa jengo la bunge mjini Ankara ambalo lilishambuliwa na ndege za kivita za wanajeshi walioasi.

Jaribio hilo la mapinduzi la Ijumaa lilianza kwa ndege za kivita chapa F-16 kuruka chini chini katika mji mkuu wa Ankara na wanajeshi na vifaru kuingia mitaani mbapo milio ya miripuko ilihanikiza usiku kucha katika mji mkuu huo pamoja na katika mji mkubwa kabisa nchini humo wa Istanbul. Ndege za kivita za jeshi la Uturuki chapa F-16 zilifanya mashambulizi ya anga dhidi vifaru vilivyowekwa na wahusika wa njama ya mapinduzi nje ya kasri la rais mjini Ankara.

Wakati umma ulipowageukia wanajeshi kadhaa waliokuwa wakiunga mkono mapinduzi hayo walisalimu amri karika daraja la Bosphorus mjini Istanbul waliokuwa wakilishikilia wakati wa usiku ambapo picha za televiheni zimewaonyesha wakinyoosha mikono yao juu kuashiria kusalimu amri wakati wakitiwa nguvuni.

Wahusika kukiona cha moto

Erdogan ambaye anadhamini mapinduzi nchini Syria amelaani jaribio hilo la mapinduzi kuwa ni usaliti kwa taifa na kwamba wahusika watalipa kwa gharama kubwa kwa kitendo chao hicho cha uhaini.

Sheik Gulen rafiki aliyegeuka kuwa hasimu wa Erdogan anayetuhumiwa kuhusika na njama hiyo amekanusha vikali kuhusika kwa njia yoyote ile na njama hiyo kwa kusema kwamba tuhuma hizo dhidi yake ni "matusi".

Uturuki imetaka kurudishwa nchini humo kwa watu wanane wanaodaiwa kuhusika na njama hiyo ya mapinduzi ambao wamewasili Ugiriki kwa kutumia helikopta ya kijeshi chapa ya Black Hawk.

Baadhi ya viongozi wa Dunia wataka kuungwa mkono kwa serikali

Baadhi ya Viongozi hususan wale wanaoshirikiana na Uturuki katika kuleta machafuko nchini syria wametowa wito wa kuwepo utulivu nchini humo ambapo Rais Barack Obama wa Marekani na nchi nyengine za magharibi wamehimiza kuungwa mkono kwa serikali ya nchi hiyo ambayo wamesema imechaguliwa kwa njia ya demokrasia.

Kiongozi wa Jumuiya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amekaribisha kile alichokiita "uungaji mkono madhubuti ulioonyeshwa na wananchi na vyama vya kisiasa kwa demokrasia na kwa serikali ilioyochaguliwa kidemokrasia ya Uturuki mwanachama muhimu wa Jumuiya ya NAO."

Msemaji wa Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema "inapaswa kuchukuliwa hatua zote kuhakikisha maisha ya binaadamu yanalindwa" wakati waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault amesema anataraji demokrasia ya Uturuki "itaibuka ikiwa madhubuti zaidi.

Jeshi la Uturuki ambalo liliwahi kuwa na ushawishi mkubwa nchini humo kwa muda mrefu limekuwa likijihesabu kama mlezi wa taifa hilo lilisilo jifungamanisha katika misimamo ya kidini lililoasisiwa na Kemal Ataturk hapo mwaka 1923. Jeshi liliwahi kufanya mapinduzi mara tatu nchini humo tokea mwaka 1960 na iliiondoa madarakani serikali ya sera kali za Kiislamu hapo mwaka 1997.

Wanajeshi 8 waliokimbia Uturuki waomba hifadhi Ugiriki

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema wanajeshi wa kituruki waliokimbia na helkopita na kutua nchini Ugiriki baada ya kushindwa kwa jaribio la mapinduzi wanapaswa kurejeshwa nchini mwao. Wanajeshi hao wanane walitua katika mji wa Alexandroupolis ulio mpakani na Uturuki kuomba hifadhi ya kisiasa. Rubani wa helkopita hiyo aliomba kibali cha kutua kwa dharura na baadae walikamatwa na polisi. Vyombo vya habari vya Ugiriki vimeripoti kuwa wanajeshi hao wanaaminika kuwa wameshiriki jaribio la mapinduzi la nchini Uturuki kwa kuwa walikuwa katika sare za kijeshi walipowasili. Wapo mameja watatu, makapteni watatu na sajenti meja wawili. Ugiriki imesema inaagalia suala la kuwapatia hifadhi ya kisiasa kulingana na sheria za kimataifa.

Mwisho wa habari/ 291


No comments:

 
 
Blogger Templates