- Awaonya na kuwataka kuacha mara moja wanaochochea Mgogoro wa kisiasa Mbalizi
- Alipatia ufumbuzi tatizo la Maji mbalizi
- Awapa wiki mbili halmashauri kumaliza sintofahamu kati yao na bodaboda na wafanyabiashara wa masoko
- Serikali inakusudia kufufua viwanda vya Tanganyika Packers na Mbeya textile
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amosi Makala
Mamia ya wakazi wa mji wa Mbalizi wamejitokeza kueleza Kero mbalimbali kwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Amosi Makala huku Kero Nyingi zikihusisha tatizo la maji, Mgogoro wa kisiasa ndani ya Mamlaka ya mji Mdogo, mvutano wa halmashauri na wafanyabiashara wa masoko A&B , ufufuaji viwanda na ujenzi wa ofisi ya halmashauri
Akijibu Kero za wananchi Mkuu wa Mkoa amekwenda na kuwaonya wote wanaochochea Mgogoro wa kisiasa ndani ya mamlaka vya mji mdogo na amemwagiza Mkuu wa wilaya, mkurugenzi na viongozi wa Mamlaka kukaa pamoja na kuelekezana majukumu yao , kuelewa sheria na kutekekeza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na si kwa mihemuko ya kiitikadi.
Mwanachi wa mji wa Mbalizi akieleza kero, Mbele ya Mkuu wa Mkoa
Amehaidi kumchukulia hatua kali yeyote atakayekiuka miongozo itakayotolewa na amewataka wanasiasa kutokuendekeza Siasa kwani kufanya hivyo ni kuwagawa wananchi na kuwacheleweshea maendeleo yao.
Amehaidi kumchukulia hatua kali yeyote atakayekiuka miongozo itakayotolewa na amewataka wanasiasa kutokuendekeza Siasa kwani kufanya hivyo ni kuwagawa wananchi na kuwacheleweshea maendeleo yao.
Kuhusu tatizo la maji katika mji wa Mbalizi amewaagiza Mamlaka ya Maji Mbeya kukaa na Mamlaka ya mji Mdogo mbalizi na kuingia makubaliano ili Mamlaka ya Maji Mbeya wahudumiwe eneo la jiji na Mamlaka ya Mbalizi na kwa kufanya hivyo tatizo la maji litakuwa limekwisha kwani Mamlaka ya Maji Mbeya wana Maji ya kutosha, watalaam, vitendea kazi vya kuboresha huduma ya maji.
Mamia ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Kuhusu viwanda vya Tanganyika Packers na Mbeya Textile amesema nia ya serikali ni kuvifufua na kazi iliyopo ni kutafuta wawekezaji . Kufufuliwa kwa viwanda hivyo kutaongeza ajira na masoko kwa zao la Pamba na mifugo.

Kuhusiana na azma ya halmashauri kuwachukulia hatua bodaboda na wafanyabiashara kutakiwa kuachia vyumba sokoni amewagiza kukaa na kufikia muafaka ikiwemo kutoa elimu kwanza kabla ya kuchukulia hatua.
Mwandishi Bashiru Madodi.
No comments:
Post a Comment