Kijungu jiko hupatikana katika mto kiwira maeneo ya Magereza Kiwira eneo hili lipo katika wilaya ya Rungwe mkoani mbeya.
Eneo hili la kijungu jiko lipo umbali mdogo kutoka eneo lilipo Daraja la Mungu (God's bridge), ambapo uwapo ukanda huu hususani kuanzia katika ile mitelemko ilipoanzia lami ielekeayo chuo cha mafunzo cha magereza huwa na hali joto kiasi, pia mandhari yake huvutia sana kwa muonekano wa milima milima na ukijani mzuri sana.
kwa mujibu wa mwenyeji wetu mzee Eliah Kabhagase alisema mto huu hutililisha maji yake kutoka katika chanzo huko mlima Rungwe kisha kumwaga maji yake ziwa Nyasa wiayani Kyela,
Maji ya mto huu yanapoingia katika kijungu yanaingia kwa kasi sana kisha kutokea upande wa pili yake, yakitoka ndani ya kijungu huendelea na safari zake ambapo ni umbali mdogo kutoka eneo la kijungu mpaka lilipo daraja la mungu katika mto Kiwira
Kijungu jiko ni eneo lenye kustaajabisha sana kwa sababu kimeumbwa kwa mwamba na kufanya umbo la kama la chungu, ambacho hupokea maji yote ya mto huo na kuyapeleka chini bila kuyapitisha juu ya mwamba huo. Lakini pia kama kutakuwa na jua basi ukitizama ndani ya kijungu utaona upinde wa mvua.
Inaelezwa kwamba ili mtu uvuke kwa
usalama kwenye mwamba juu ya kijungu kutoka upande wa mashariki lazima utumie mguu mmoja wa kulia kisha kuusogega taratibu mpaka ukimaliza kuvuka, na ukitoka magharibi utatakiwa kutumia mguu wa kushoto na kuusogeza taratibu huku mguu wa kulia ukifuata nyuma, kwa kufuata hayo hutatumbukia.
Kitu kingine ni uwepo wa imani kuwa endapo mtu akizama katika mto huo,
lazima afuatwe na mzamiaji (mtoto wa chief) aliyerithi kazi hiyo kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa kimila na kwamba bila huyo basi aliyezama atakaa katika shimo (mbako) kwa muda wa siku kadhaa kulingana na uzito kama mnene atachelewa mpaka siku saba na kama mwembamba anaweza chukua siku nne kwa muda wote huo ndugu wakiwa mtoni usiku na mchana ndipo atakuja kuonekana.
Mzee eliah alieleza kuwa lile pango maji yanaingia ni kubwa kiasi cha kufika mbele zaidi ya tunapo park magari, ilitubidi kuthibitisha hilo kwa kwenda mpaka lilipokuwapo shimo ambalo watoto na ng'ombe walikuwa wakizama wanatokea huku kwenye karibu na kijungu, ambalo uongozi wa kijiji ulifanya juhudi la kuziba.
Wazee wanaamini chini ya kijungu yupo nyoka mkubwa mwenye vichwa saba ajulikanae kama NYAFWILA ambae hukaa chini ya ardhi na likitokea tetemeko la ardhi wazee huamini nyoka huyo anajigeuza au anasogea kutoka sehemu moja kwenda nyingine
No comments:
Post a Comment