Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Tunatekeleza kilichorushwa na TBC 1,chenye lengo la Mawaziri kueleza umma namna wanavyotekeleza majukumu.
“Muswada huu mzuri na utasaida kuleta suluhishi la malalamiko ya kuwepo kwa sheria kandamizi,pia itasaidia kukuza tansia ya habari pamoja na kuifanya tasnia ya habari kuheshimiwa kama tansia nyingine”,alisema Waziri Nnauye.
Waziri Nnauye alisisitiza kuwa uandaaji wa Muswada ulishirikisha wadau mbalimbali na kuzingatia maoni yao na serikali itaendelea kupokea maoni ya wadau hata mara baada ya kusomwa kwake.
Pamoja na hayo Waziri huyo mwenye dhamana na sekta ya habari nchini kupitishwa kwa Muswada huo kutasaidia kutoa suluhisho la kuwepo na changamoto katika sekta ya utangazaji ambayo kwa sasa inaonekana kupoteza mulekeo.
Aidha,Waziri Nnauye alisema kuwa serikali inataka kuipeleka tansia ya habari mbali na kupitia Muswada huo utasaidia kufanikisha hilo kwani umeeleza kuwa mwandishi anahitajika kuwa na digrii na hii ni kwalengo la kuweka heshima ya taaluma kama ilivyokwa taaluma nyingine mfano sheria.
Halikadhalika Waziri huyo alizungumzia kuwepo na changamoto katika Sheria ya Utangazaji kwani imekuwa haionyeshi Mtangazaji anaporusha kipindi hewani kilicho kinyume na maadili ni adhabu gani apewe,
“Tungependa sheria ijayo iweze kumbana mwandishi pale anapokosa maadili na kumchukulia hatua kama ilivyo kwa tansia nyingine kama uhandisi na sheria kufikia hatua kufutiwa utoaji wa huduma hiyo”,alisisitiza Mhe.Nnauye.
Akizungumza kuhusu changamoto ya upatikanaji wa taarifa kutoka kwa wasemaji wa taasisi za Serikali Waziri Nape alisema tayari ametoa agizo kwa watendaji kuwashirikisha wasemaji katika vikao vya maamuzi ili waweze kuwa na taarifa za pamoja na kuwapa nafasi ya kusema ikiwa na sehemu ya kazi yao.
Hata hivyo Mheshimiwa Waziri ameliahidi Shirika la Utangazaji nchi kulisaidia kutatua changamoto zinazolikabili ikiwemo uhaba wa vifaa,pamoja na kuboresha maslai ya watumishi wake.Pia ameeleza Bodi mpya ya TBC 1 iliyoundwa imepitia mkataba wa TBC 1 na STARTIMES kwa lengo la kutaka kuiboreshea mazingira shirika hilo na tayari imekwisha maliza kazi na kuwasilisha mapendekezo.
Chanzo. Raia mwema
No comments:
Post a Comment