Na Bashiru Madodi
Washiriki waliopanda mlima Rungwe wakiwa katika kilele cha mlima Rungwe
Safari ya kupanda Mlima Rungwe wenye sifa madhubuti nchini Tanzania uliratibiwa na Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa kushirikiana na taasisi mbali mbali kama vile Wildlife conservation society (WCS), African wildlife Foundation (AWF), Mount Rungwe Nature Reserve (MRNR), Tanzania forest services (TFS), Waheshimiwa madiwani wa wilaya ya Rungwe, Kamati ya utalii ya wilaya, Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na Uyole cultural tourism enterprises.
Hili ni eneo la msitu mwembamba katika mlima Rungwe
Safari hii ilikuwa na jumla ya washiriki sabini na nne (74) ambao kila mmoja alielezea ni kwa namna gani ameifurahia safari hii, Tulipozungumza na Afisa utalii Dada Levina wa jiji la Mbeya alisema “amefurahishwa sana na mapokeo ya watu juu ya umuhimu utalii wa ndani hivyo anawasihi watu kuendelea kuwa na moyo wa kupenda safari hizi” Lakini pia Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe pamoja na Afisa mali asili na Afisa utalii wakasema upo mpango madhubuti wa kufanya safari nyingi katika vivutio vya kitalii vipatikanavyo wilaya ya Rungwe ikiwezekana angalau kila mwisho wa mwezi kuwe na safari moja.
Wapanda mlima Rungwe wakiwa katika eneo la msitu mnene
Mlima Rungwe una aina kama tatu (3) za uot0, unapoanza mlima kuna msitu mnene, na mkipanda zaidi kuna msitu mwembamba na juu kabisa ni nyasi. juu ya mlima kuna baridi sana maana unakuwa juu umbali wa Mita 2981 kutoka katika usawa wa bahari
Kwa taarifa zaidi Piga simu namba 0783 545464/0766422703
No comments:
Post a Comment