Profesa Muhungo alisema Serikali bado inasisitiza kwamba tatizo la upungufu wa umeme lazima liiishe ndiyo maana inafanya jitihada mbalimbali za kuongeza uzalishaji wa umeme.
“Mradi wa Kinyerezi IV utazalisha umeme Megawati 330 na utagharimu Dola za Marekani milioni 350.
“Mradi wa Kinyerezi IV ni mradi wa nne wa kuzalisha umme ukitanguliwa na Kinyerezi I utakaozalisha Megawati 150, Kinyerezi II Megawati 240 na Kinyerezi III ambao kwa kuanzia utazalisha Megawati 300,” alisema Profesa Muhongo.
Alisema mradi huo wa Kinyerezi IV pia utazalisha umeme kwa kutumia nguvu ya gesi asilia na kwamba ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka kesho.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Felchesmi Mramba alisema kipindi cha watanzania kukaa bila umeme kimekwisha.
Chanzo:- Mtanzania
No comments:
Post a Comment