Akizungumza na MTANZANIA, Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, alisema Sugu pamoja na wabunge wengine wa chama chake waliamua kwenda polisi wenyewe kuondoa sintofahamu iliyokuwapo.
Miongoni mwa wabunge walioongozana na Sugu, ni na Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.
Mnyika alisema wakiwa kituoni hapo, Sugu aliandika maelezo kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma akisaidiwa na wakili wake, Lissu.
“Hajakamatwa, bali tumekwenda naye polisi kuripoti, Mwenyekiti Mbowe, Wakili Lissu, Nassari na mimi, na muda huu ndiyo anamalizia kuandikisha maelezo,” alisema Mnyika.
Chanzo:- Mtanzania
No comments:
Post a Comment