Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa msingi wa wodi ya wazazi ya kituo cha afya kata ya Lubanda wilayani Ileje.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akishirikiana na wananchi wa kata ya Lubanda kujenga msingi wa wodi ya akina mama katika kituo cha afya cha kata hiyo wilaya ya Ileje mkoani Mbeya.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akiwa nyumbani kwa Balozi wa Shina namba 1 Balozi Nosadi Edward (mwenye fulana kulia),Katibu Mkuu amekuwa na utamaduni wa kutembelea mabalozi katika ziara zake .
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akisalimiana na wakazi wa shina namba 1 kata ya Sange ,wilaya ya Ileje mkoan Mbeya.
Wasanii wa ngoma wakicheza ngoma ya Ibandi ngoma maarufu ya kabila la Wandari wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana Ujumbe wake ambao walitembelea kata ya Kalembo ,wilaya ya Ileje mkoani Mbeya.
Diwani wa Kata ya Isongole Ndugu Gwalusako Kapesa akielezea namna gani wananchi wa ilaya ya Ileje wamechoshwa na taratibu za serikali za kuwalazimisha kununua mbolea za ruzuku za Minjingu kwani zimekuwa hazina faida kwao kama wakulima na zimewaletea hasara kubwa sana, wananchi hao wameiomba serikali na viongozi wake kuwasikiliza zaidi wao katika kutatua kero zao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Kalembo na kuwaambia kilio cha wakulima kinafanana karibia nchi nzima hasa kuhusu matatizo ya mbolea na kusema CCM itachukua hatua kwa kukutana na waziri husika kwenye kamati kuu itakayofanyika mapema mwezi ujao.
Wananchi wa Kata ya Kalembo wakiwa wamejifunika miamvuli kujikinga na mvua wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake ambao upo ziarani mkoani Mbeya.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa salaam za kumbukumbu za kifo cha marehemu Steven Kibona kwa wananchi wa kata ya Kalembo, kushoto ni mjane wa marehemu Mama Kibona.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje Ndugu Rosemary Sinyamule kwenye daraja la mto Songwe mpakani mwa Tanzania na Malawi,Mkuu wa Wilaya alimueleza Katibu Mkuu kuwa kuna eneo hilo lina fursa nyingi kibiashara na kiuchumi kama barabara ya lami itajengwa na ikiwa pamoja na ofisi za kudumu za uhamiaji zitajengwa katika kata ya Isongole.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro wakizungumza na wananchi wa kata ya Isongole wilaya ya Ileje mpakani mwa Tanzania na Malawi.
Katibu Mkuu wa CCM akiwa nje ya ofisi ya uhamiaji ya kata ya Isongile wilaya ya Ileje mkoani
Mbeya,kushoto ni mkuu wa kituo hicho cha uhamiaji Ndugu Fredrick Luhanga.
Habari na basahama
No comments:
Post a Comment