Kwa mbali dada mtu huyo akaanza kuwaza kuhusu ndoa yake maana tangu amepigwa chini na mumewe hakuwaambia wazazi wake…
“Mimi mama sijafanya kwa nia mbaya.”
“Hapana, ulipoona shemejiyo kakwambia hivyo na umemshauri mdogo wako hataki, ungetuletea habari sisi.”
“Nisamehe mimi mama.”
Mara mlango ukafunguliwa, Aisha akatoka huku akimwaga machozi.
JIACHIE MWENYEWE…“
Nini wewe?” aliuliza mama mtu huyo.
“Mama mimi nasafiri usiku huuhuu.”
“Kwenda wapi?”
“Kurudi kwangu.”
“Nini kimetokea, mbona unalia?”
“Nimekumbuka mengi mama. Ni kweli nilikuwa nakosea kumkatalia unyumba mume wangu…amekuwa akinisema sana kuhusu hilo sikuwa namsikia, sasa najuta mama.”
“Huwezi kupata gari muda huu! Nadhani unajua.”
“Hata malori nitapanda mama.”
Mara, baba mtu naye akatoka baada ya kumsikia Aisha akitangaza kuondoka usiku huohuo kurudi kwa mume wake, Dar es Salaam…
“Kama amelijua kosa lake na kuamua aende sawa tu, nenda. Ukipata gari wasalimie, ukikosa rudi ulale kesho uondoke,” alisema baba mtu huyo huku akirudi ndani. Sauti yake haikuonesha uzembe wakati wa kuzungumza.
***
Asubuhi Aisha aliwaaga wazazi wake kurudi Dar kwa mume wake baada ya jana yake kukosa usafiri.
“Sisi wazazi wako Aisha tunakutaka ukaishi kwa mumeo ukijua yeye ndiye kichwa cha nyumbani kwako. Kama utataka kujifanya mko sawa hamtafika mbali, ukweli tunakwambia.”
“Sawa mama, mimi nimeelewa lakini pia naamini mnajua nilivyotendewa na dada yangu,” alisema Aisha huku akimwangalia dada yake kwa jicho baya!
“Tunajua, hilo tuachie sisi tutajua jinsi ya kufanya, wewe nenda salama na uwe na amani. Yote yatoe moyoni mwako ili uishi kwa amani.”
***
Ilikuwa jioni baada ya Aisha kuondoka, baba yao alipokuwa amerudi kutoka kwenye mihangaiko yao, alimwita mkewe na kumwambia wamuweke chini dada wa Aisha na kumuuliza kuna nini nyumbani kwake mpaka akaenda Dar kuishi kwa mdogo wake yakatokea ya kutokea…
“Tumekuita hapa Ime, tunataka kujua na wewe nyumbani kwako kuna nini mpaka ukaenda kuishi kwa mdogo wako Dar es Salaam?” aliuliza baba mtu kwa sauti isiyotaka utani wale kucheleweshewa majibu…
“Mimi nimeachika!”
“Umeachika! Ime, unasema kweli unanitania?” alidakia mama mtu huku akikaa sawasawa.
“Nimeachika mama,” alisema dada mtu huyo huku akianza kulia.
“Nyamaza! Umeachika kwa sababu gani?” baba mtu alikuja juu…
“Mume wangu alisema amechoka tu kuishi na mimi, akanipa nauli niondoke.”
“Siyo kweli, mimi si mtoto wa kunidanganya Ime,” alikataa baba mtu. Mama naye akasema…
“Au ulifanya umapepe wako huko?”
“Hapana mama.”
Baba mtu huyo alichukua simu yake na kumpigia mkwewe lakini huku naye akishangaa kwamba kama ni kweli kwa nini mkwewe huyo hajamwambia?
“Hujambo baba?”
“Sijambo baba shikamoo?”
“Marhaba, mzima?”
“Mimi mzima kiasi, habari za hapo nyumbani?”
“Njema. Tumeona kimya, nikasema ngoja nikupigie.”
“Nipo baba.”
“Sasa eti huyu mwenzako alipatwa na nini? Maana kaja hapa tunamuuliza kwa mumeo vipi anasema umemwacha.”
“Baba kwani hajawapa barua yangu?”
“Barua! Wala hajatupa, ulimpa barua?”
“Nilimpa barua yenye maelezo ya kutosha kabisa, akasema anaanzia Dar kwa Aisha halafu anakuja huko. Nikajua ni kweli, jana tu nikasikia kaharibu Dar, nikashangaa kugundua kumbe alikuwa bado Dar muda wote huo.”
“Mh! Baba mimi nashukuru sana. Kwa sababu umesema kuna barua ngoja nimwambie anipe niisome kwanza halafu nitawasiliana na wewe baba.”
“Sawa baba.”
Baba mtu alimgeukia binti yake…
“Eti barua yangu iko wapi?”
“Ilipotea baba.”
Mzee huyo alisimama na kumfuata mwanaye ili amchape makofi, lakini mama mtu akajitahidi kumzuia asifanye hivyo.
“Mjinga sana huyu mtoto. Kenge mkubwa kasoro mkia wewe. Unataka kutufanya sisi watoto wadogo? Barua haikupotea bali umeipoteza wewe makusudi ili tusijue kilichoandikwa ndani yake, mimi nampigia mumeo aniambie kisa,” alisema baba huyo kwa sauti yenye ukali.
***
Aisha alifika nyumbani kwake lakini hakumkuta mume wake, Beka. Akachukua funguo mahali na kuzama ndani bila kumwambia kwamba amerudi.
Beka siku hiyo alikuwa kwa demu wake mpya ambaye alianza kuwa na uhusiano naye siku mbili kabla ya fumanizi lake na shemejiye. Kwa hiyo alikuwa nyumbani kwa demu huyo ambapo si mbali sana kutokea kwake.
“Baby, kwa hiyo ni kweli kabisa mkeo anaweza kukunyima unyumba?”
“Si anaweza, ananinyimaga sana tu.”
“Daa! Anakosea sweet,” alisema demu huyo anayeitwa Faidha huku akimlalia kifuani Beka na kumkumbatia kwa staili ya mahaba mazito.
“Basi kwangu umefika, hata akikunyima mwaka mzima, mimi nipo dear,” alisema Faidha huku akifungu vifungo vya shati la Beka.
No comments:
Post a Comment