Social Icons

Sunday, 14 September 2014

HADITHI: Missed call ya shemeji -18


“Basi baby kwangu umefika, hata akikunyima mwaka mzima, mimi nipo dear,” alisema Faidha huku akifungua vifungo vya shati la Beka. Songa nayo...

eka alikuwa akipumua kwa nguvu, kila alipokuwa akimwangalia demu wake mpya, Faidha alivyokuwa akifungua vifungo vya shati lake, akabaki akitweta tu.
“Yule mwanamke alinikera sana,” alisema Beka.

“Achana naye bwana, hajui jinsi ya kumuhendo mwanaume, ngoja nimuonyeshe,” alisema Faidha, alijua fika kwamba alikuwa mwizi, hivyo alitaka kufanya vitu kwa nguvu zote ili aweze kumchukua Beka jumla.
Kwa sababu alisoma alama zote za nyakati hasa kile kilichokuwa kikitaka kutokea mahali hapo, Beka akachukua simu yake na kuizima kabisa, hakutaka kusumbuliwa kwani aliona muda mchache baadaye angekuwa bize.

“Una kifua kizuri, yaani nashangaa alikuachaje miezi yote hiyo jamani, hana hata huruma,” alisema Faidha.“We acha tu, hebu endelea kwanza, yule mjinga sitaki hata kumsikia.”

Faidha alitumia ujuzi wake wote, mara aukandekande mgongo wa Beka, mara ampeleke huku na kule, yaani kila kitu alichokuwa akikifanya mahali hapo kilikuwa ni kumfanya Beka amuone kuwa bora zaidi, alijua kwamba yeye ni mwizi, hivyo alihakikisha kwamba wizi wake unafanikiwa.

* * *
Aisha alitulia chumbani, kichwa chake kilikuwa na mawazo tele, alikuwa akijuta juu ya kile alichokuwa amekifanya cha kumnyima unyumba mume wake kwa muda mrefu.
“Mimi mwanamke kwa nini nimefanya vile? Hivi kama ningefanyiwa mimi ingekuwaje?” alijiuliza Aisha.
Wakati huo, hakujua kwamba mume wake alikuwa kwa demu wake mpya baada ya kuona kwamba mke wake huyo alikuwa akimletea mapozi. Aisha aliendelea kumsubiri mume wake arudi ili akae naye chini na kuyazungumza.

“Kwanza yupo wapi? Mbona anachelewa hivyo? Au kapata demu mwingine?” alijiuliza Aisha lakini hakutaka kukubaliana na mawazo yake, alijua kwamba mumewe ni mwaminifu sana japokuwa alimsaliti kwa dada yake, Ime.

***
Baba Aisha hakutaka kukubali, alijua kwamba Ime alipoteza barua ile kwa ajili ya kupoteza ushahidi juu ya kile kilichokuwa kimeandikwa, hivyo alitaka kumpigia mume wa Ime ili amwambie ukweli.
“Niambie baba.”

“Huyu mkeo kapoteza barua, hebu niambie ilikuwaje.”
“Unaona baba, nilijua tu hataifikisha, huyo mwanamke mpumbavu sana.”


Hebu niambie ilikuwaje.”
“Ime si mwaminifu kabisaaa, yaani japokuwa nilimuoa, alikuwa akitoka nje ya ndoa bila mimi kujua.”
“Unasema kweli?”

“Ndiyo, wewe si umeona hata ule ujinga alioufanya kwa mdogo wake, umekuwa gumzo jiji zima.”
“Aiseeee, yaani kumbe ndiyo aliyokuwa akiyafanya?”
“Ndiyo baba. Wakati mwingine anachelewa kurudi, nimemfumania mara kibao tu, akawa ananipiga saundi kwamba alikuwa kwa marafiki zake.”
“Kumbeeeee.”

“Ndiyo, huyo hafai kuwa mke wangu. Na ndiyo maana hata hiyo barua hakutaka kuileta kwenu.”
“Sawa, tutaongea zaidi.”
Baba Aisha akakata simu na kuanza kumwangalia Ime, kwa jinsi alivyoonekana tu, alikuwa na hasira tele.

* * *
Mlango ukafunguliwa, Beka akaingia chumbani, macho yake hayakuonyesha mshtuko wala tabasamu, kitendo alichofanyiwa na mke wake, Aisha kilimuuma, sasa alikuwa amefika hapo wayamalize.
“Karibu mume wangu.”
“Asante,” alisema Beka huku akikaa kitandani, bado alionekana kuwa na kitu moyoni.
“Naomba unisamehe.”

“Nikusamehe! Umefanya nini?”
Aisha akanyamaza kwa muda.
“Nilikuwa nakunyima unyumba.”
“Kwa hiyo leo ndiyo umeamua kuniomba msamaha baada ya kugundua kwamba lile lilikuwa kosa?”
“Hapana, siyo hivyo, naomba unisamehe tu.”

Aisha akaona hiyo haitoshi, alichokifanya ni kumsogelea Beka na kuanza kumshikashika mgongoni, Beka mwenyewe wala hakutaka kushoboka, kila kitu alikimalizia kwa demu mpya, Faidha.
“Sawa, tutaangalia.”


Jamani, sasa tutaangalia nini baby?”
Beka hakutaka kuongea sana, kile alichokisema kilitosha kabisa, akasimama na kulifuata kabati, akavua nguo, akavaa nyingine na kutulia kitandani.
“Naomba unisamehe mpenzi.”
“Mbona yameshakwisha, si umeamua kurudi, yameshakwisha kitambo tu.”
“Sawa. Nashukuru.”

Wala Beka hakuwa na mawazo na huyo mke wake, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria Faidha tu, kwake, kipya kilikuwa kinyemi, hivyo demu huyo alionekana kuwa na nguvu kuliko Aisha.

***

Haya sasa endelea kutudanganya, yote yashawekwa kweupeeeee, nimeshayajua,” alisema baba Aisha huku akimwangalia Ime.
“Amesemaje?” aliuliza mama.

“Kumbe alikuwa akimsaliti mwenzake, hakuwa akitulia, keshazoea ule mchezo na ndiyo maana akaenda kuurudia hata kwa shemeji yake, yaani hata aibu haoni.”
“Nisameheni,” alisema Ime huku akijitahidi kuyatafuta machozi.
“Wewe si umejifanya mjanja kupoteza barua, kiko wapi sasa, tumeshajua ujinga wako. Unapata mume wa kuishi naye, unafanya ujinga, hujui kama kuolea dili.”

“Nisameheni.”
“Kwani umetukosea sisi? Nenda kamwambie mumeo kwamba ulimkosea.”

* * *

Mapenzi ya Faidha yalimchanganya Beka, japokuwa alimpiga kalenda mke wake kwamba angemwambia kama alimsamehe au la, lakini bado naye alikuwa na mchepuko wake uliokuwa ukimliwaza.

Beka akabadilika kabisa, akawa anakaa sana kwa mchepuko wake Faidha huku wakati mwingine akilala hukohuko kwa kisingizio cha kazi nyingi.

Aisha akavumilia, hakuwa na jinsi, hakuweza kuondoka nyumbani hapo, ila pamoja na yote hayo, makosa yalikuwa kwake, alilikoroga weee, sasa alitakiwa kulinywa.
“Jamani mume wangu unanitesa.”
“Nakutesa?”

“Ndiyo. Kila siku unachelewa kurudi.”
“Kazi zimekuwa nyingi mno.”
“Sasa mbona hauniambiagi?”
Beka hakutaka kuendelea kujibu maswali zaidi kwani yalimchosha. Alikuwa radhi kukaa kimya na kuanza kuufikiria mchepuko wake kuliko kumjibu Aisha ambaye kwake alionekana muuaji, miezi miwili hadi mitatu bila unyumba, ilikuwa ni shiiiiiida.

Inaendelea 

Chanzo globalpublishers 

No comments:

 
 
Blogger Templates