Wenzake miguu chini ya meza ilikuwa ikiwasiliana ile mbaya, miguu ya dada mtu ilipanda hadi karibu ya magoti ya Beka, naye akarudishia
ilikuwa kama wanacheza. Kitendo cha kufumba na kufumbua Aisha aliinamisha kichwa na kuchungulia chini. Dondoka nayo...
Wote walishtuka kwa kitendo cha Aisha kuchungulia chini, wakajibalaguza na kujifanya na wao wameshtuka kwa sababu yake…
“Vipi mwenzetu?” aliuliza Beka huku akimwangalia shemeji yake badala ya aliyekuwa akimuuliza.
“Hamna kitu, nimehisi naguswa na mguu wa mtu.”
“Utakuwa mguu wa nani?” aliuliza dada mtu huku akionesha kuhofia.
“Sijamjua.”
Kwa namna moja au nyingine, Aisha ni kama alishtuka. Alihisi kuna kilichokuwa kikiendelea kwenye miguu ya watu wawili hao.
“Au wanachezeana miguu nini?” alijiuliza Aisha.
Siku hiyo ilipita bila Beka na shemeji yake kukutana wala kutumiana meseji, ingawa kila mmoja alimtamani mwenzake kwamba wangekuwa pamoja.
Dada wa Aisha aliamini kule kufuatwa chumbani alfajiri ilikuwa sawa na kuonjeshwa nyama bila supu yake, alitamani kukutana na shemeji yake
huyo lakini nje ya nyumba hiyo ili aweze kufaidi nyama na supu yake moja kwa moja.
kwa upande mwingine, aliamini anatenda uovu mkubwa kwa kutembea na mume wa mdogo wake akasema moyoni…
“Lakini sasa nitafanyaje na mimi ni binadamu, natamani, napenda, nahisi na nataka kama yeye…
“Isitoshe mambo mengine anayasababisha mwenyewe Aisha, miaka ya sasa ni ya kumnyima unyumba mwanaume kweli? Maana mji kama huu wa Dar esSalaam kuna wanawake wa kila umbile, rangi, mwendo, mikogo. Unaweza kujikuta unampoteza hivihivi unaona.”
Siku ya tatu yake, Beka akiwa njiani kurejea nyumbani kwake alitumiwa meseji na shemeji yake…
“Jamani shemeji mbona kimya sana?”
“Mimi wewe shemeji?”
“Wewe bwana.”
“Wewe hapo bwana.”
“Tuyaache hayo, uko wapi muda huu?”
“Njiani.”
“Kwenda wapi?”
“Ndiyo nakuja.”
“Je, nikisema usije nyumbani ili tukutane mahali hukohuko, maana leo nimekukumbuka sana, utakubali?”
Ilikuwa kama bahati njema kwa Beka kwani hata yeye alisema moyoni kwamba lazima siku hiyo amalize kiu yake kwa shemeji yake huyo…
“Wewe tu, mimi niko sawa. Mdogo wako amerudi?”
“Bado.”
“Sasa utaondokaje?”
“Nitamtumia meseji.”
“Kwamba unakwenda wapi?”
“Kusuka.”
“Atakuelewa?”
“Juu yake bwana, kwani mi mtoto wake?”
“Basi njoo hadi mahali panaitwa Sakafuni Gesti.”
“Mh!Ndiyo wapi hapo?”
“Ukiwa unakwenda stendi. ulipokuja siku ile lazima ulipitia hapa.”
“Oke, nakuja. nikipotea nitakwambia. Chukua chumba kabisa. Siyo nifike hapo ning’aeng’ae macho tu.”
Dada mtu huyo alijiandaa kwa kuoga na kuvaa kwa mtoko ambapo alifunga mlango na funguo kuziweka chini ya kapeti mlangoni, akatimka huku
akiangalia kona zote kama Aisha atatokea na kuvuruga dili lake…
“Asije akatokea huyu fisadi wa mapenzi dili likafa bure,” alisema moyoni akikaribia barabarani.
Aisha alipofika nyumbani alishangaa sana kutokumkuta dada yake…
“Khaaa! Huyu atakuwa amekwenda wapi tena, mbona hatujaambiana sasa?” alijiuliza mwenyewe Aisha.
alimpigia simu mume wake ili kumwambia kituko hicho cha dada yake kuondoka bila kusema wakati si mwenyeji kwenye Jiji la Dar.
“Haya, mke mwenzio anapiga sasa,” alisema Beka akimwangalia shemeji yake.
“Pokea halafu weka loud speaker.’
“Haloo.”
“Baby maajabu ya mwaka nimeyakuta hapa home.”
“Yapi tena?”
“Shemeji yako kafunga mlango kaondoka.”
“Kaenda wapi?” alihoji Beka huku akimshikashika wowowo shemeji yake ndani ya chumba cha gesti huku akionekana hana wasiwasi wowote ule, ndiyo
muda wake wa kufaidi matunda mawili kutoka kwenye mti mmoja uliomea kwenye mbolea.
“Sijui, hata funguo sijui kaiweka wapi!”
“Au ameenda kijijini kwa kutoroka?” aliuliza Beka…
“Kisa cha kutoroka asiage kiwe nini? Wala hajaondoka, si ajabu yupo kwenye michepuko yake na nina wasiwasi ameachika kwa mumewe kwa sababu
hiyohiyo ya michepuko.”
“Inawezekana,”
Beka alishtukia ameporwa simu na shemeji yake, ikaanguka chini…
“Hawezi kunitukana namna hii, mimi nachepuka mimi? Mkeo amenikosea sana tena sana, aniombe radhi kabla jua halijazama,”
Beka aliogopa sana kwani aliamini kitendo cha kuporwa simu na kuanguka chini kisha shemeji mtu huyo kusema kitakuwa kimejulikana kwa mkewe,
Aisha…
“Khaa!” alishangaa Beka na kujikuta ameirukia lakini kumbe ilipoanguka ilitawanyika kava na betri.
“Khaa! Huyu vipi, kapata ajali au?” alijiuliza Aisha kule upande wa pili baada ya simu ya mumewe kukata ghafla na pia akawa hapatikani.
“Tena tumalize mambo yetu ndiyo uwashe hiyo simu yako,” alisema shemeji huyo akimwambia Beka aliyekuwa bado kwenye mshangao mkubwa.
“Tena umwambie mke wako kwamba ilikuwa nikuache siku mbili hizi na yeye ili afaidi lakini sasa sikuachii ng’oo mpaka ajute kuzaliwa na mimitumbo moja.”
“Yaishe baby, achana naye yule.”
Ili kumkomoa mdogo wake, shemeji huyo alisimama katikati ya chumba na kuvua nguo zake zote kisha akawa kama alivyozaliwa mbele ya shemeji
yake akijitingishatingisha, akapanda kitandani na kumvuta shemeji yake, Beka ili naye apande…
“Tena leo utainjoi sana kuliko kule chumbani. kila hatua nitakuwa nahakikisha inakuwa kisasi kwa mkeo, malaya mkubwa yule, anataka kucheza na
mimi mtoto wa mjini siyo.”
Je, nini kilitokea? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda, Jumatatu ijayo.
“Shemeji usimtukane hivyo mdogo wako, hata mimi naumia sasa,” alisema Beka.
“Njoo bwana shemejim ndiyo mida yenyewe hii ya kujifaidi.”
Ni kweli dada mtu huyo aliamua kusaliti kikwelikweli kwani hata mapigo yenyewe kwa shemeji yake siku hiyo yalikuwa ya kushangaza, kuna wakati
alionesha dalili za kupanda kwenye ukuta.
Aisha alitaka kuingia ndani akampigia simu dada yake lakini haikupokelewa.
Inaendelea
Chanzo Globalpublishers
No comments:
Post a Comment